Migogoro Mashariki Kati
Na Cantona Joseph Julai 02, 2026 08:40 (EAT)
Wapatamishi wa mzozo wa Mashariki ya Kati Qatar na Pakistan wamesema kuwa Marekani na Iran zimepiga hatua katika mazungumzo yao yasiyo ya moja kwa moja.

Wapatanishi wasema Marekani na Iran zimepiga hatua katika mazungumzo ya DohaPicha: Jacquelyn Martin/AP Photo/dpa/picture alliance
Wapatamishi wa mzozo wa Mashariki ya Kati Qatar na Pakistan wamesema kuwa Marekani na Iran zimepiga hatua katika mazungumzo yao yasiyo ya moja kwa moja. Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Qatar Majed al-Ansari amesema kwamba “maendeleo chanya” yamepatikana kuhusu masuala yanayohusiana na makubaliano ya mfumo yaliyofikiwa wiki mbili zilizopita ili kukomesha vita vya Iran. Mazungumzo hayo katika mji mkuu wa Qatar, Doha, yalifanyika katika nyakati tofauti na wapatanishi kutoka pande mbili za mzozo huo.
Al-Ansari amesema pande hizo zimekubaliana kuendelea na majadiliano katika kipindi kijacho, huku mkutano unaofuata ukitarajiwa kupangwa haraka iwezekanavyo baada ya shughuli za mazishi ya kiongozi mkuu wa zamani wa Iran Ayatollah Ali Khamenei, ambaye aliuawa katika shambulio la anga la Israelmwishoni mwa Februari. Kulingana na ripoti za Iran, shughuli hizo zitaanza Julai 4 katika mji mkuu Tehran na mji wa hija wa Qom. Maziko yanatarajiwa kufanyika Julai 9 katika eneo alikozaliwa Khamenei, la Mashhad, kaskazini mashariki mwa nchi.
Wapatamishi wa mzozo wa Mashariki ya Kati Qatar na Pakistan wamesema kuwa Marekani na Iran zimepiga hatua katika mazungumzo yao yasiyo ya moja kwa moja.
Asili na Mazingira Ivory Coast
Mvua kubwa yasababisha mafuriko pwani ya Afrika Magharibi
Mvua kubwa imesababisha mafuriko makubwa katika nchi kadhaa za pwani ya Afrika Magharibi, ikiwa ni pamoja na Ivory Coast, Ghana na Benin. Watu 59 wamekufa Ivory Coast na 12 katika nchi jirani Ghana.

Nyumba iliyoharibiwa na maporomoko ya ardhi katika makazi yasiyo rasmi ya Attecoube, mjini AbidjanPicha: Diomande Ble Blonde/AP Photo/picture alliance
Nchini Ivory Coast watu 59 wamekufa tangu kuanza kwa msimu wa mvua mwezi Mei. Akizungumza baada ya mkutano wa Baraza la Mawaziri, Msemaji wa serikali Amadou Coulibaly aliwaambia waandishi wa habari kwamba “baraza la mawaziri linasikishwa na idadi kubwa ya vifo vya watu 59 mwaka huu.” Katika nchi jirani ya Ghana, mamlaka zimesema watu 12 walikufa kutokana na mafuriko mwanzoni mwa wiki hii. Siku ya Jumatatu, mafuriko na maporomoko ya ardhi yaliyosababishwa na mvua kubwa ya siku kadhaa katika miji mikuu ya Ghana na Ivory Coast yalisababisha vifo vya watu wasiopungua 24 na wengine wengi kutoweka.
Mvua zaidi kubwa inatarajiwa katika pwani ya Afrika Magharibi katika siku zijazo. Kulingana na Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Uratibu wa Masuala ya Kibinadamu (OCHA), takriban watu milioni 7.5 wako hatarini kutokana na mafuriko. Msimu wa mvua katika nchi za pwani kwenye Ghuba ya Guinea kwa kawaida hudumu kuanzia Aprili hadi Agosti na Oktoba hadi Novemba. Katika nchi za Sahel kama vile Malina Senegal, karibu mvua zote za kila mwaka hutokea kati ya Juni na Septemba.
Migogoro Ukraine
Miji ya Ukraine yalengwa kwa mashambulizi ya droni za Urusi

Mashuhuda wamesema milipuko kadhaa imesikika katika mji mkuu wa Ukraine KyivPicha: Thomas Peter/REUTERS
Miji kadhaa ya Ukraine imekumbwa na wimbi kubwa la mashambulizi ya makombora na ndege zisizo na rubani za Urusi usiku kucha. Vyombo vya habari vimeripoti mtu mmoja aliuawa na karibu wengine 11 wakajeruhiwa katika Kiev.
Vyombo vya habari vya ndani vikiwanukuu maafisa vimeripoti Alhamisi kwamba mtu mmoja aliuawa na karibu wengine 11 wakajeruhiwa katika mji mkuu wa Ukraine, Kiev. Majengo ya makazi, ikiwa ni pamoja na hoteli, yaliripotiwa kuwaka moto katika mji mkuu, huku majengo mengi ya ghorofa yakiharibiwa. Ripoti hizo zimesema makombora kadhaa yalirushwa. Kiwango kamili cha uharibifu hakijawekwa wazi mara moja, na ripoti za awali hazikuweza kuthibitishwa kwa njia huru.
Gazeti la Kyiv Independent lilielezea shambulio hilo kuwa mojawapo ya mashambulizi makali zaidi tangu kuanza kwa uvamizi kamili wa Urusi mwaka wa 2022. Ving’ora vya tahadhari za mashambulizi ya anga na milipuko pia vilisikika katika maeneo mengine ya nchi, ikiwa ni pamoja na Zaporizhzhya na Pavlohrad kusini-mashariki, pamoja na Sumy na Kharkiv kaskazini-mashariki.
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky alikuwa ameonya Jumatano kuhusu shambulio kubwa linalokaribia kufanywa nchini Ukraine. Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari huko Dublin wakati wa ziara ya kuadhimisha Ireland kuchukua urais wa kupokezana wa Umoja wa Ulaya, Zelensky alisema Urusi ilifanya mashambulizi makubwa kwa kutumia mamia ya droni na makombora kadhaa kila baada ya wiki moja hadi mbili.
Sheria na HakiKenya
Wanafunzi wanane washitakiwa kwa mauaji Kenya

Wasichana 16 walifariki baada ya moto kuteketeza bweni katika Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Utumishi huko Gilgil.Picha: Simon Maina/AFP
Mahakama ya Kenya imewashtaki wasichana wanane wa shule kwa mauaji. Wameshtakiwa kwa kusababisha vifo vya wanafunzi wenzao 16 katika moto wa bweni kwenye shule moja ya jimbo la Bonde la Ufa mwishoni mwa mwezi Mei.
Mahakama ya Kenya imewashtaki wasichana wanane wa shule jana Jumatano kwa mauaji. Wameshtakiwa kwa kusababisha vifo vya wanafunzi wenzao 16 katika moto wa bweni kwenye shule moja ya jimbo la Bonde la Ufa nchini Kenya mwishoni mwa mwezi Mei. Wasichana hao walifariki baada ya moto kuteketeza bweni katika Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Utumishi huko Gilgil, Kaunti ya Nakuru, na kuwajeruhi wanafunzi wengine 79. Wanafunzi katika shule hiyo wana umri wa kuanzia miaka 15 hadi 18.
Washtakiwa hao wanane walifika mbele ya Jaji wa Mahakama Kuu ya Kibera jijini Nairobi, Diana Kavedza na wote walikana mashtaka hayo. Waendesha mashtaka hawajatoa maelezo mengine kuhusu kesi hiyo hadi sasa. Watoto waliwahi kushtumiwa kwa kuanzisha moto shuleni kimakusudi nchini Kenya hapo awali. Ripoti moja iligundua kuwa kulikuwa na visa 63 vya uchomaji moto shuleni katika mwaka wa 2018 pekee. Wanafunzi walishtakiwa baada ya moto wa bweni mwaka 2001 katika kaunti ya kusini mwa nchi ya Machakos kuua watu 67. Moto wa bweni mwaka 2024 katika Shule ya Hillside Endarasha, kaunti ya Nyeri uliwaua wavulana 21.
afghanistan, africa, albania, algeria, America, american-samoa, andorra, angola, anguilla, antarctica, antigua-and-barbuda, argentina, armenia, aruba, arusha, australia, austria, azerbaijan, bahamas, bahrain, bangladesh, barbados, belarus, Belgium, belize, benin, bermuda, bhutan, bolivia, bosnia-and-herzegovina, botswana, Boukinafaso, brazil, brunei-darussalam, bulgaria, burkina-faso, burma, burundi, california, cambodia, cameroon, canada, cape-verde, cayman-islands, central-african-republic, Chad, chicago, chile, china, christmas-island, cocos-keeling-islands, colombia, comoros, congo, cook-islands, costa-rica, cote-divoire-ivory-coast, Croatia, cuba, cyprus, czech-republic, darsalaam, democratic-peoples-rep-north-korea, democratic-republic-of-the-congo-kinshasa, denmark, djibouti, dodoma, dominica, dominican-republic, dr-congo, dubai, east-timor-timor-leste, ecuador, egypt, egypty, el-salvador, england, equatorial-guinea, equitorial-guinea, eritrea, estonia, eswatini, ethiopia, falkland-islands, faroe-islands, federal-states-of-moldova, fiji, finland, Florida, france, french-guiana, french-polynesia, french-southern-territories, gabon, gaza, georgia, germany, ghana, gibraltar, goma, Greece, greenland, grenada, guadeloupe, guam, guatemala, guinea, guinea-bissau, guyana, habari, haiti, holy-see, honduras, hong-kong, houston, hungary, iceland, india, indonesia, Iowa, iran, iran-islamic-republic-of, iraq, ireland, israel, italia, italy, ivory-coast, jamaica, japan, jordan, karatu, kazakhstan, kilimanjaro, kinshasa, kiribati, kiswahili, korea, kosovo, kuwait, kyrgyzstan, lao, latvia-lebanon-lesotho-liberia-libya-liechtenstein-lithuania-luxembourg, Lebanon, liberia, macau, madagascar, malawi, malaysia-maldives, Mali, malta, marshall-islands-martinique-mauritania-mauritius, massechutes, mayotte, mazingira, mbeya, meru, mexico, miami, micronesia, monaco-mongolia-montenegro, montserrat, morocco, mozambique-myanmar, mtwara, mwanza, namibia, nauru, nepal, netherlands, netherlands-antilles, nevada, new-caledonia, new-zealand, newyork, nicaragua, niger, nigeria, niue, north-macedonia, northern-mariana-islands, norway, oman, pakistan, palau, palestine, palestinian-territories, panama, papua-new-guinea, paraguay, peoples-democratic-republic, peru, philadhephia, philipians, Philippines, pitcairn-island, poland, politics, Portugal, puerto-rico, qatar, republic-of, republic-of-brazzaville, republic-of-south-korea, reunion-island, romania, Russia, russian-federation, rwanda, sahara-occidental, saint-kitts-and-nevis, saint-lucia, saint-vincent-and-the-grenadines, samoa, san-marino, sao-tome-and-principe, saudi-arabia, saudiarabia, scotland, Senegal, serbia, seychelles, sierra-leone, Singapore, singida, slovakia-slovak-republic, slovenia, solomon-islands, somalia, southafrica, spain, sri-lanka, sudan, suriname, swaziland-eswatini, sweden, switzerland, syria, syrian-arab-republic, tabora, taiwan-republic-of-china, tajikistan, tanzania, texas, thailand, the-gambia, tibet, timor-leste-east-timor, togo, tokelau, tonga, toronto, trinidad-and-tobago, tunisia, turkey, turkmenistan, turks-and-caicos-islands, tuvalu, uganda, united-arabs-emirates, united-kingdom, united-states, uruguay, uzbekistan, vancover, vanuatu, vatican-city-state-holy-see, venezuela, vietnam, virgin-islands-british, virgin-islands-u-s, wallis-and-futuna-islands, wallis-and-futuna-islands, wallis-et-futuna, washington-dc, western-sahara, yemen, zambia, zambie, zimbabwe

Leave a Reply