Na Cantona Joseph Julai 02, 2026 08:40 (EAT)

Spika wa Bunge la Iran, Mohammad Baqer Qalibaf, amesema wakaguzi wa Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki (IAEA) hawataruhusiwa kuingia katika vituo vya nyuklia vya Iran vilivyoharibiwa na mashambulizi.
“Kwa mujibu wa sheria iliyopitishwa na Bunge na kuidhinishwa na Baraza Kuu la Usalama wa Taifa, hakuna mazingira yatakayoruhusu ufikiaji wa maeneo yaliyoshambuliwa na kuharibiwa,” alisema Qalibaf.
Kauli hiyo imekuja wakati Qatar ikitangaza kumalizika kwa duru nyingine ya mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja kati ya Iran na Marekani yaliyofanyika mjini Doha.
https://www.youtube.com/live/vAQcNqKrrjQ?si=V9tmnZAdZE8u9p0r
Mashambulizi ya makombora na droni za Urusi mjini Kyiv yaua watu 10

Takriban watu 10 wameuawa katika mashambulizi ya makombora na ndege zisizo na rubani ya Urusi dhidi ya mji mkuu wa Ukraine, Kyiv, usiku wa kuamkia Alhamisi.
Milipuko zaidi ya kumi ilisikika katika maeneo ya kati na mashariki mwa Kyiv, huku wakazi wakikimbilia vituo vya metro vilivyotumika kama makazi ya kujikinga.
Meya wa Kyiv alisema kupitia Telegram kuwa mji huo ulikuwa ukishambuliwa kwa makombora ya balestiki na droni, huku milipuko ikisikika katika sehemu mbalimbali za jiji.
Mashambulizi hayo yalifuatia onyo la Jeshi la Anga la Ukraine kuhusu makombora ya balestiki yaliyokuwa yakielekea mji mkuu.
Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky, alifupisha ziara yake nchini Ireland Jumatano baada ya kupokea taarifa za kijasusi kwamba Urusi ilikuwa ikijiandaa kufanya shambulio jipya dhidi ya nchi yake.
“Nawasihi wananchi kuwa waangalifu sana, wawalinde watoto na familia zao, na wakimbilie kwenye makazi ya kujikinga,” Zelensky alisema katika mkutano na waandishi wa habari.
Aliongeza kuwa Urusi imekuwa ikijiandaa kwa muda mrefu kutekeleza shambulio hilo kubwa dhidi ya Ukraine.
Urusi imeendelea kushambulia miji ya Ukraine, ikiwemo Kyiv, kwa makombora na ndege zisizo na rubani tangu ilipoanzisha uvamizi wake wa kijeshi nchini humo mwezi Februari mwaka 2022.
Zaidi ya watu 900 wakamatwa katika maandamano dhidi ya wahamiaji Afrika Kusini

Zaidi ya watu 900 wamekamatwa kufuatia maandamano ya kitaifa dhidi ya wahamiaji yaliyofanyika Jumanne nchini Afrika Kusini, ambayo kwa kiasi kikubwa yalikuwa ya amani lakini katika baadhi ya maeneo yaligeuka kuwa ya vurugu na kusababisha uporaji wa maduka.
Naibu Kamishna wa Kitaifa wa Polisi, Tebello Mosikili, amesema maandamano 108 kati ya 120 yaliyofanyika nchini yalikuwa ya amani, huku maandamano 12 yakihitaji polisi kuingilia kati.
Amesema sababu za kukamatwa kwa watu hao zinajumuisha ukiukaji wa sheria za uhamiaji, kufanya vurugu hadharani, kuwaficha wahamiaji wasio na nyaraka halali na wizi.
Polisi pia wamesema mtu mmoja alipigwa risasi na kuuawa usiku wa Jumanne katika kitongoji cha Alexandra, mjini Johannesburg, ambako wakazi walikuwa wakipora maduka madogo maarufu kama spaza shops yanayomilikiwa na raia wa kigeni.
Mamlaka zilisambaza askari wa ziada katika majimbo matano kati ya tisa ya nchi hiyo usiku kucha, huku wanajeshi wakipelekwa katika eneo la Hillbrow katikati mwa Johannesburg, ambako watu wawili walijeruhiwa kwa kupigwa risasi.
Katika mji wa bandari wa Durban, polisi wameanza uchunguzi kuhusu kifo cha raia mmoja wa kigeni ambaye inadaiwa alijirusha kutoka ghorofa ya nane ya jengo moja usiku kabla ya maandamano, akiamini alikuwa analengwa.
Maandamano ya Jumanne yaliandaliwa kuashiria mwisho wa muda uliowekwa na kundi linalopinga wahamiaji, lililokuwa limetaka wahamiaji wasiokuwa na vibali halali vyaondoke Afrika Kusini.
afghanistan, africa, albania, algeria, America, american-samoa, andorra, angola, anguilla, antarctica, antigua-and-barbuda, argentina, armenia, aruba, arusha, australia, austria, azerbaijan, bahamas, bahrain, bangladesh, barbados, belarus, Belgium, belize, benin, bermuda, bhutan, bolivia, bosnia-and-herzegovina, botswana, Boukinafaso, brazil, brunei-darussalam, bulgaria, burkina-faso, burma, burundi, california, cambodia, cameroon, canada, cape-verde, cayman-islands, central-african-republic, Chad, chicago, chile, china, christmas-island, cocos-keeling-islands, colombia, comoros, congo, cook-islands, costa-rica, cote-divoire-ivory-coast, Croatia, cuba, cyprus, czech-republic, darsalaam, democratic-peoples-rep-north-korea, democratic-republic-of-the-congo-kinshasa, denmark, djibouti, dodoma, dominica, dominican-republic, dr-congo, dubai, east-timor-timor-leste, ecuador, egypt, egypty, el-salvador, england, equatorial-guinea, equitorial-guinea, eritrea, estonia, eswatini, ethiopia, falkland-islands, faroe-islands, federal-states-of-moldova, fiji, finland, Florida, france, french-guiana, french-polynesia, french-southern-territories, gabon, gaza, georgia, germany, ghana, gibraltar, goma, Greece, greenland, grenada, guadeloupe, guam, guatemala, guinea, guinea-bissau, guyana, habari, haiti, holy-see, honduras, hong-kong, houston, hungary, iceland, india, indonesia, Iowa, iran, iran-islamic-republic-of, iraq, ireland, israel, italia, italy, ivory-coast, jamaica, japan, jordan, karatu, kazakhstan, kilimanjaro, kinshasa, kiribati, kiswahili, korea, kosovo, kuwait, kyrgyzstan, lao, latvia-lebanon-lesotho-liberia-libya-liechtenstein-lithuania-luxembourg, Lebanon, liberia, macau, madagascar, malawi, malaysia-maldives, Mali, malta, marshall-islands-martinique-mauritania-mauritius, massechutes, mayotte, mazingira, mbeya, meru, mexico, miami, micronesia, monaco-mongolia-montenegro, montserrat, morocco, mozambique-myanmar, mtwara, mwanza, namibia, nauru, nepal, netherlands, netherlands-antilles, nevada, new-caledonia, new-zealand, newyork, nicaragua, niger, nigeria, niue, north-macedonia, northern-mariana-islands, norway, oman, pakistan, palau, palestine, palestinian-territories, panama, papua-new-guinea, paraguay, peoples-democratic-republic, peru, philadhephia, philipians, Philippines, pitcairn-island, poland, politics, Portugal, puerto-rico, qatar, republic-of, republic-of-brazzaville, republic-of-south-korea, reunion-island, romania, Russia, russian-federation, rwanda, sahara-occidental, saint-kitts-and-nevis, saint-lucia, saint-vincent-and-the-grenadines, samoa, san-marino, sao-tome-and-principe, saudi-arabia, saudiarabia, scotland, Senegal, serbia, seychelles, sierra-leone, Singapore, singida, slovakia-slovak-republic, slovenia, solomon-islands, somalia, southafrica, spain, sri-lanka, sudan, suriname, swaziland-eswatini, sweden, switzerland, syria, syrian-arab-republic, tabora, taiwan-republic-of-china, tajikistan, tanzania, texas, thailand, the-gambia, tibet, timor-leste-east-timor, togo, tokelau, tonga, toronto, trinidad-and-tobago, tunisia, turkey, turkmenistan, turks-and-caicos-islands, tuvalu, uganda, united-arabs-emirates, united-kingdom, united-states, uruguay, uzbekistan, vancover, vanuatu, vatican-city-state-holy-see, venezuela, vietnam, virgin-islands-british, virgin-islands-u-s, wallis-and-futuna-islands, wallis-and-futuna-islands, wallis-et-futuna, washington-dc, western-sahara, yemen, zambia, zambie, zimbabwe

Leave a Reply