Mazungumzo kati ya Marekani na Iran yamalizika kwa maendeleo makubwa

Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Vocalize Pre-Player Loader

Na Cantona Joseph Imechapishwa : February 27, 2026 06:00 (EAT)

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Abbas Araghchi, ambaye aliongoza ujumbe wa nchi yake, amesema “maendeleo mazuri” yamepatikana na ingawa kumekuwa na makubaliano kuhusu baadhi ya masuala, bado kuna tofauti kuhusu masuala mengine.

Mazungumzo kati ya Marekani na Iran yamalizika kwa maendeleo makubwa

o
Maelezo ya picha,Waziri wa Mambo ya Nje wa Oman Badr Albusaidi amesema Marekani na Iran zimeonyesha “uwazi” baada ya kukutana na Jared Kushner na Steve Witkoff

Waziri wa mambo ya nje wa Oman amesema maafisa wa Marekani na Iran wamepata “maendeleo makubwa” katika mazungumzo ya nyuklia huko Geneva, lakini uwezekano wa kuwepo kwa makubaliano ambayo yanaweza kuzuia vita bado hauko wazi.

Badr Albusaidi, ambaye alikuwa mpatanishi, amesema pande hizo mbili zimepanga kuanza tena mazungumzo “hivi karibuni,” na majadiliano ya ngazi ya kiufundi yatafanyika wiki ijayo huko Vienna.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Abbas Araghchi, ambaye aliongoza ujumbe wa nchi yake, amesema “maendeleo mazuri” yamepatikana, ingawa kuna makubaliano kuhusu baadhi ya masuala, bado kuna tofauti kuhusu masuala mengine.

Amesema duru inayofuata ya mazungumzo itafanyika katika kipindi cha chini ya wiki moja.

Matarajio ya kuwepo kwa mazungumzo zaidi yanaweza kupunguza uwezekano wa Rais Donald Trump kuishambulia Iran.

Trump ameamuru kupelekwa wanajeshi wengi wa Marekani katika Mashariki ya Kati, ikiwa ni idadi kubwa tangu uvamizi wa Marekani nchini Iraq mwaka 2003, huku Iran ikiapa kujibu shambulio lolote.

Kwa miongo kadhaa, Marekani na Israeli zimeishutumu Iran kwa kujaribu kutengeneza silaha ya nyuklia kwa siri. Iran imekana mara kwa mara kwamba inaunda bomu hilo na inasema mpango wake ni wa amani tu, ingawa nchi hiyo ndiyo taifa pekee lisilo na silaha za nyuklia ambalo limeongeza urani katika kiwango cha karibu cha silaha.

Kulingana na vyombo vya habari vya serikali ya Iran, wapatanishi walisisitiza kwamba Iran ina haki ya kuwa na nishati ya nyuklia ya amani na walikataa madai ya Marekani ya kusimamisha kabisa urutubishaji wa urani na kuhamisha akiba yake ya kilo 400 (880lb) ya urani iliyorutubishwa kutoka nchini humo.

Ingawa mapendekezo hayo hayajawekwa wazi lakini mojawapo ya chaguzi zilizoripotiwa ni Iran kuruhusiwa kurutubisha urani kwa kiwango kidogo chini ya ufuatiliaji wa kimataifa.

Na kwa upande wa Iran, Araghchi ameiambia televisheni ya Iran kwamba wapatanishi wao wanataka kuondolewa kwa vikwazo ambavyo vimedhoofisha uchumi wa Iran.

Mazungumzo hayo yasiyo ya moja kwa moja yalifanyika katika vikao viwili. Kipindi kimoja asubuhi, ambacho kilidumu kwa saa tatu, na kingine, kifupi jioni. Hakuna kauli ya Marekani kuhusu matokeo ya mkutano huo.

Kama ilivyokuwa katika raundi zilizopita, Marekani iliwakilishwa na mjumbe maalum Steve Witkoff na mkwe wa Trump, Jared Kushner. Rafael Grossi, mkuu wa shirika la kimataifa la ulinzi wa nyuklia, Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki (IAEA), pia alijiunga na mazungumzo hayo.

Iran tayari imekataa kujadili mipaka ya mpango wa makombora ya balestiki na kukomesha uungaji mkono wake kwa washirika wake katika eneo hilo, ikiwa ni pamoja na Hamas huko Gaza, Hezbollah huko Lebanon, wanamgambo nchini Iraq, na Houthi huko Yemen.

Pakistan yaishambulia Afghanistan

p

Pakistan imethibitisha kufanya mashambulizi katika miji ya Afghanistan ya Kabul na Kandahar, kulingana na afisa wa serikali, katika kile alichosema ni kulipiza kisasi kwa mashambulizi ya awali.

Imekuja saa chache baada ya Pakistan kusema wanajeshi wake wawili wameuawa baada ya operesheni ya Taliban wa Afghanistan kando ya mpaka.

Kulingana na Mosharraf Zaidi, msemaji wa waziri mkuu wa Pakistan, jumla ya Taliban 133 wa Afghanistan wameuawa na zaidi ya 200 wamejeruhiwa hadi sasa na vikosi vya Pakistan.

Lakini Zabihullah Mujahid, msemaji wa Taliban ya Afghanistan, aliandika kwenye X kwamba “hakuna mtu aliyejeruhiwa” katika mashambulizi hayo ya hivi karibuni ya Pakistan.

Wakati wa uhasama huu, pande zote mbili zimedai kusababisha hasara kubwa kwa upande mwingine huku zikipata uharibifu mdogo kwa upande wao.

Wizara ya ulinzi ya Taliban amesema iliteka vituo 19 vya kijeshi vya Pakistan na kambi mbili Alhamisi usiku na jumla ya wanajeshi 55 wa Pakistani waliuawa

Kama ukumbusho, ni vigumu kuthibitisha takwimu hizi.

Mashambulizi dhidi ya Kabul na Kandahar ni ya hivi karibuni katika mfululizo wa mapigano kati ya Pakistan na Afghanistan, licha ya mataifa yote mawili kukubaliana kusitisha mapigano kwa muda mfupi Oktoba 2025.

Wiki iliyopita, Pakistan ilifanya mashambulizi mengi ya anga usiku dhidi ya Afghanistan, ambayo Taliban ilisema yaliwaua watu wasiopungua 18, wakiwemo wanawake na watoto.

Islamabad ilithibitisha mashambulizi hayo yalilenga kambi saba zinazodaiwa kuwa za wanamgambo karibu na mpaka wa Pakistan na Afghanistan, na ikasema yalizinduliwa kufuatia mashambulizi ya ya mabomu ya kujitoa mhanga nchini Pakistan.

Taliban ya Afghanistan ilisema imeanzisha operesheni “kubwa” kujibu, na siku ya Alhamisi ilidai kwamba mashambulizi yao yaliwaua wanajeshi “wengi” wa Pakistan.

Hili lilikataliwa na msemaji wa waziri mkuu wa Pakistan, ambaye pia alipinga madai ya msemaji wa Taliban kwamba vituo 15 vya kijeshi vilitekwa.

Baadaye siku hiyo, Pakistan ilithibitisha kwamba wanajeshi wake wawili waliuawa na wengine watatu kujeruhiwa, baada ya wanajeshi kujibu “mashambulizi ya risasi ” kando ya mpaka wao wa pamoja.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2026

afghanistanafricaalbaniaalgeriaAmericaamerican-samoaandorraangolaanguillaantarcticaantigua-and-barbudaargentinaarmeniaarubaarushaaustraliaaustriaazerbaijanbahamasbahrainbangladeshbarbadosbelarusBelgiumbelizebeninbermudabhutanboliviabosnia-and-herzegovinabotswanaBoukinafasobrazilbrunei-darussalambulgariaburkina-fasoburmaburundicaliforniacambodiacamerooncanadacape-verdecayman-islandscentral-african-republicChadchicagochilechinachristmas-islandcocos-keeling-islandscolombiacomoroscongocook-islandscosta-ricacote-divoire-ivory-coastCroatiacubacyprusczech-republicdarsalaamdemocratic-peoples-rep-north-koreademocratic-republic-of-the-congo-kinshasadenmarkdjiboutidodomadominicadominican-republicdr-congodubaieast-timor-timor-lesteecuadoregyptegyptyel-salvadorenglandequatorial-guineaequitorial-guineaeritreaestoniaeswatiniethiopiafalkland-islandsfaroe-islandsfederal-states-of-moldovafijifinlandFloridafrancefrench-guianafrench-polynesiafrench-southern-territoriesgabongazageorgiagermanyghanagibraltargomaGreecegreenlandgrenadaguadeloupeguamguatemalaguineaguinea-bissauguyanahabarihaitiholy-seehondurashong-konghoustonhungaryicelandindiaindonesiaIowairaniran-islamic-republic-ofiraqirelandisraelitaliaitalyivory-coastjamaicajapanjordankaratukazakhstankilimanjarokinshasakiribatikiswahilikoreakosovokuwaitkyrgyzstanlaolatvia-lebanon-lesotho-liberia-libya-liechtenstein-lithuania-luxembourgLebanonliberiamacaumadagascarmalawimalaysia-maldivesMalimaltamarshall-islands-martinique-mauritania-mauritiusmassechutesmayottemazingirambeyamerumexicomiamimicronesiamonaco-mongolia-montenegromontserratmoroccomozambique-myanmarmtwaramwanzanamibianaurunepalnetherlandsnetherlands-antillesnevadanew-caledonianew-zealandnewyorknicaraguanigernigerianiuenorth-macedonianorthern-mariana-islandsnorwayomanpakistanpalaupalestinepalestinian-territoriespanamapapua-new-guineaparaguaypeoples-democratic-republicperuphiladhephiaphilipiansPhilippinespitcairn-islandpolandpoliticsPortugalpuerto-ricoqatar Norrbottens lanrepublic-of-brazzavillerepublic-of-south-koreareunion-islandromaniaRussiarussian-federationrwandasahara-occidentalsaint-kitts-and-nevissaint-luciasaint-vincent-and-the-grenadinessamoasan-marinosao-tome-and-principesaudi-arabiasaudiarabiascotlandSenegalserbiaseychellessierra-leoneSingaporesingidaslovakia-slovak-republicsloveniasolomon-islandssomaliasouthafricaspainsri-lankasudansurinameswaziland-eswatiniswedenswitzerlandsyriasyrian-arab-republictaborataiwan-republic-of-chinatajikistantanzaniatexasthailandthe-gambiatibettimor-leste-east-timortogotokelautongatorontotrinidad-and-tobagotunisiaturkeyturkmenistanturks-and-caicos-islandstuvaluugandaunited-arabs-emiratesunited-kingdomunited-statesuruguayuzbekistanvancovervanuatuvatican-city-state-holy-seevenezuelavietnamvirgin-islands-britishvirgin-islands-u-swallis-and-futuna-islands


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a Reply