RDC: Jukwa la C64 linamtaka Rais Félix Tshisekedi kujiuzulu

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Na Cantona Joseph June 17, 2026 06:00 (EAT)

Jukwaa la kisiasa linalojumuisha vyama vya upinzani vinavyopinga mpango wa kufanyika kwa marekebisho ya katiba nchini DRC la C64 sasa limeandaa maandamano ya nchi nzima tarehe 08 mwezi Julai, kumtaka rais Félix Tshisekedi kuondoka madarakani.

Félix Tshisekedi - Rais wa DRC.
Félix Tshisekedi – Rais wa DRC. © Evan Vucci / AP

Tangazo hili la Jukwaa la C64 lilitolewa hapo jana siku ya jumanne baada ya kutamatika kwa mkutano wa viongozi wa vyama vya upinzani, mkutano uliolenga kutathmini matukio ya Juni 12, kuhusu mwitikio mkubwa wa maandamano yao yaligubikwa na vurugu jijini Kinshasa, ambapo watu kadhaa waliripotiwa kujeruhiwa miongoni delly sessanga na Martin Fayulu pamoja na wafuasi wao.

Maandamano haya mapya ya Julai 08 yanatarajiwa kufanyika Jijini Kinshasa mbele ya Ikulu ya rais Félix Tshisekedi kumtaka ajiuzulu, upinzani ukimtuhumu kwa uhaini na kutoilinda Katiba.

Martin Fayulu - Mwanasiasa wa upinzani nchini DRC.
Martin Fayulu – Mwanasiasa wa upinzani nchini DRC. AP – Mosa’ab Elshamy

Promesse Matofali mwakilishi wa chama cha upinzani cha ensemble pour la République kutoka mashariki mwa DRC.

‘‘Huo ni utawala ambao ulitoka kwenye uchaguzi na inaonekana vuguvugu hili lina agenda moja na waasi wa M23 wanaoungwa mkono na Rwanda.’’ Amesema Promesse Matofali.

Hata hivyo upande wa Chama tawala cha UDPS wao wamepuuzilia mbali juhudi hizi za upinzani. Lwanzo kasonia Jean de Dieu, ni mwakilishi wa chama hicho akiwa Kinshasa.

‘‘Tumeamua kuandamana tarehe nane mwezi Julai kwa sababu wakati wa kutoa ushauri wa Rais umefika na yeye hapendi kusikia.’’ Amesema Lwanzo kasonia Jean de Dieu.

Maandamano ya kupinga wito wa kufanyiwa katiba marekebisho yaliofanyika jijini Kinshasa.
Maandamano ya kupinga wito wa kufanyiwa katiba marekebisho yaliofanyika jijini Kinshasa. AP – Mosa’ab Elshamy

Siku ya Jumatatu, Juni 15, Baraza la Seneti lilipitisha muswada unaoelezea taratibu za kufanyika kwa kura ya maoni, Maseneta walirekebisha muundo wa Bunge Maalumu la Katiba lililopewa jukumu la kuandaa mageuzi yatakayowasilishwa kwa kura ya wananchi.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2026

afghanistanafricaalbaniaalgeriaAmericaamerican-samoaandorraangolaanguillaantarcticaantigua-and-barbudaargentinaarmeniaarubaarushaaustraliaaustriaazerbaijanbahamasbahrainbangladeshbarbadosbelarusBelgiumbelizebeninbermudabhutanboliviabosnia-and-herzegovinabotswanaBoukinafasobrazilbrunei-darussalambulgariaburkina-fasoburmaburundicaliforniacambodiacamerooncanadacape-verdecayman-islandscentral-african-republicChadchicagochilechinachristmas-islandcocos-keeling-islandscolombiacomoroscongocook-islandscosta-ricacote-divoire-ivory-coastCroatiacubacyprusczech-republicdarsalaamdemocratic-peoples-rep-north-koreademocratic-republic-of-the-congo-kinshasadenmarkdjiboutidodomadominicadominican-republicdr-congodubaieast-timor-timor-lesteecuadoregyptegyptyel-salvadorenglandequatorial-guineaequitorial-guineaeritreaestoniaeswatiniethiopiafalkland-islandsfaroe-islandsfederal-states-of-moldovafijifinlandFloridafrancefrench-guianafrench-polynesiafrench-southern-territoriesgabongazageorgiagermanyghanagibraltargomaGreecegreenlandgrenadaguadeloupeguamguatemalaguineaguinea-bissauguyanahabarihaitiholy-seehondurashong-konghoustonhungaryicelandindiaindonesiaIowairaniran-islamic-republic-ofiraqirelandisraelitaliaitalyivory-coastjamaicajapanjordankaratukazakhstankilimanjarokinshasakiribatikiswahilikoreakosovokuwaitkyrgyzstanlaolatvia-lebanon-lesotho-liberia-libya-liechtenstein-lithuania-luxembourgLebanonliberiamacaumadagascarmalawimalaysia-maldivesMalimaltamarshall-islands-martinique-mauritania-mauritiusmassechutesmayottemazingirambeyamerumexicomiamimicronesiamonaco-mongolia-montenegromontserratmoroccomozambique-myanmarmtwaramwanzanamibianaurunepalnetherlandsnetherlands-antillesnevadanew-caledonianew-zealandnewyorknicaraguanigernigerianiuenorth-macedonianorthern-mariana-islandsnorwayomanpakistanpalaupalestinepalestinian-territoriespanamapapua-new-guineaparaguaypeoples-democratic-republicperuphiladhephiaphilipiansPhilippinespitcairn-islandpolandpoliticsPortugalpuerto-ricoqatarrepublic-ofrepublic-of-brazzavillerepublic-of-south-koreareunion-islandromaniaRussiarussian-federationrwandasahara-occidentalsaint-kitts-and-nevissaint-luciasaint-vincent-and-the-grenadinessamoasan-marinosao-tome-and-principesaudi-arabiasaudiarabiascotlandSenegalserbiaseychellessierra-leoneSingaporesingidaslovakia-slovak-republicsloveniasolomon-islandssomaliasouthafricaspainsri-lankasudansurinameswaziland-eswatiniswedenswitzerlandsyriasyrian-arab-republictaborataiwan-republic-of-chinatajikistantanzaniatexasthailandthe-gambiatibettimor-leste-east-timortogotokelautongatorontotrinidad-and-tobagotunisiaturkeyturkmenistanturks-and-caicos-islandstuvaluugandaunited-arabs-emiratesunited-kingdomunited-statesuruguayuzbekistanvancovervanuatuvatican-city-state-holy-seevenezuelavietnamvirgin-islands-britishvirgin-islands-u-swallis-and-futuna-islandswallis-and-futuna-islandswallis-et-futunawashington-dcwestern-saharayemenzambiazambiezimbabwe

CantonaDigital
CantonaDigital

Listen Live Radio Fortune Africa
Ukweli Na Burudani.

-Be ready to be Impacted, Inspired & Empowered.

-Keep watching our Channels

Cantona Cast Television,

Fortune Television Network (FTN)

Donation
Paypal https://www.paypal.com/donate/?hosted_button_id=6EKXMLNW8W6A2&fbclid=IwY2xjawQxeChleHRuA2FlbQIxMABicmlkETFRdkNBRndpclRDQTB5bXZZc3J0YwZhcHBfaWQQMjIyMDM5MTc4ODIwMDg5MgABHq960uGsyU3ABRIBc2h-iXGhHATvuEqe55gFsQ-rDb0fT-Z7SIQ3TV8LnkpD_aem_ybU2SvBlvyqrVsS9NAczRw

An attitude determines an altitude.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025

5,411 posts
0 followers

Fediverse Followers


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a Reply