Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Na Cantona Joseph Imechapishwa : February 27, 2026 06:00 (EAT)

Vita vya uvamizi wa Urusi dhidi ya Ukraine vimedumu kwa miaka minne sasa na bado hakuna dalili ya kumalizika hivi karibuni.Picha: Vyacheslav Madiyevskyy/REUTERS
Afrika Kusini imeripoti raia wake wawili kuuawa Ukraine, huku mahakama ya Nairobi ikimshtaki mshukiwa kwa kusafirisha Wakenya 25 kwenda Urusi kupigana, katika ishara ya kuongezeka kwa athari za vita hivyo barani Afrika.
Serikali ya Afrika Kusini imethibitisha kuwa raia wake wawili wameuawa katika vita vya Ukraine. Wizara ya Mambo ya Nje imesema watu hao ni tofauti na kundi la Waafrika Kusini 17 waliodanganywa kujiunga na jeshi la Urusi na ambao wengi wao tayari wamerudishwa nyumbani. Haijafafanuliwa ni lini au kwa mazingira gani vifo hivyo vilitokea.
Wizara hiyo imesema inaendelea kuchunguza mitandao inayohusika na uajiri wa raia kwa njia ya udanganyifu. Urusi kwa upande wake imekanusha kuhusika katika uajiri haramu wa raia wa Afrika kupigana nchini Ukraine. Hata hivyo, Kyiv imekuwa ikidai kuwa maelfu ya Waafrika wamejiunga na majeshi ya Moscow.
Onesha maudhui ya nyongeza?
Maudhui haya ni sehemu ya matini unayoyasoma. Mtumaji Facebook (Meta) anatoa maudhui haya na anaweza kukusanya data za matumizi moja kwa moja unapobonyeza “Onesha maudhui”.Daima onesha maudhui kutoka kwa Facebook (Meta)
Nchini Kenya, Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma imemshtaki Festus Arasa Omwamba kwa tuhuma za kusafirisha Wakenya 25 kwenda Urusi kwa madhumuni ya unyonyaji. Kulingana na mashtaka, 22 waliokolewa kabla ya kusafiri huku watatu waliokwenda walijeruhiwa katika mapigano kabla ya kurejea nyumbani. Mshtakiwa amekana mashtaka hayo.
Ripoti ya Idara ya Kitaifa ya Ujasusi ya Kenya imeeleza kuwa mawakala wa uajiri walishirikiana na baadhi ya maafisa wa viwanja vya ndege na wahamiaji kuwezesha safari hizo. Ubalozi wa Urusi mjini Nairobi umekanusha kuhusika katika uajiri huo, lakini umesema raia wa kigeni wanaweza kujiunga kwa hiari na majeshi ya Urusi.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya, Musalia Mudavadi, amesema Wakenya 27 wameokolewa baada ya kukwama Urusi. Ameeleza kuwa anapanga kufanya ziara nchini Urusi mwezi Machi kujadili suala hilo. Tukio hili limeongeza wasiwasi kuhusu usalama na ulinzi wa vijana wa Afrika wanaovutwa katika vita vya kigeni.
Familia ya Francesca Albanese yaushtaki utawala wa Trump

Francesca Albanese amekuwa mkosoaji mkubwa wa sera za Israel katika maeneo ya Wapalestina, hatua iliyopelekea Marekani kumuwekea vikwazo.Picha: Jean Marc Ferré/MAXPPP/dpa/picture alliance
Familia ya mchunguzi wa Umoja wa Mataifa Francesca Albanese yashtaki utawala wa Trump, ikidai vikwazo vya Marekani dhidi yake vinakiuka uhuru wa kujieleza na kuathiri maisha yao binafsi.
Familia ya Francesca Albanese imewasilisha kesi katika Mahakama ya Wilaya ya Marekani mjini Washington kupinga vikwazo vilivyowekwa dhidi yake mwaka jana. Mume wake na mtoto wao mdogo wanasema hatua hiyo imeharibu maisha ya familia na kuzuia upatikanaji wa mali zao nchini Marekani. Wanadai kuwa vikwazo hivyo vinakiuka Marekebisho ya Kwanza ya Katiba ya Marekani.
Katika hati ya madai, familia hiyo inasema maoni ya Albanese kuhusu mzozo wa Israel na Palestina ni sehemu ya haki yake ya kikatiba ya kujieleza. Pia wanarejelea kazi yake inayohusiana na Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu, ICC, ambayo imetoa hati za kukamatwa kwa maafisa wa Israel akiwemo Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu. Wanasema serikali haiwezi kumuadhibu mtu kwa sababu ya maoni yake.

Francesca Albanese (wa pili kulia) akitoa hotuba wakati wa Kongamano la Umoja wa Mataifa kuhusu Palestina katika Ukumbi wa Baraza la Udhamini la Umoja wa Mataifa, New York, Marekani, tarehe 18 Mei 2018.Picha: Atilgan Ozdil/AA/picture alliance
Marekani yasisitiza vikwazo dhidi ya Albanese ni halali
Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani imekataa madai hayo, ikiita kesi hiyo “lawfare isiyo na msingi.” Imesema vikwazo vilivyowekwa dhidi ya Albanese ni vya kisheria na vinastahili. Serikali ya Marekani imemshutumu kwa kile ilichokiita kampeni ya kisiasa dhidi ya maslahi ya Marekani na Israel.
Albanese ni mtaalamu wa haki za binadamu aliyeteuliwa na United Nations Human Rights Council kuchunguza ukiukwaji wa haki katika Ukingo wa Magharibi na Gaza. Amekuwa akidai kuwa Israel inatekeleza “mauaji ya kimbari” dhidi ya Wapalestina, madai ambayo Israel na Marekani wamekanusha vikali. Licha ya vikwazo, ameendelea kutoa ripoti kali dhidi ya sera za Israel.
Msemaji wa Umoja wa Mataifa, Stephane Dujarric, amesema taasisi hiyo inafahamu kuhusu kesi hiyo na itaendelea kuwasiliana na mamlaka za Marekani kutafuta suluhu. Wakati huo huo, Ikulu ya Marekani haijatoa maoni rasmi. Kesi hiyo inatarajiwa kuchochea mjadala mpana kuhusu uhuru wa kujieleza na mamlaka ya serikali kuweka vikwazo.
Afghanistan yashambulia Pakistan, milipuko yasikika Kabul

Magari ya kijeshi yakisafiri barabarani katika eneo lililotajwa kuwa Nangarhar, Afghanistan, katika picha hii ya video iliyotolewa tarehe 26 Februari 2026.Picha: Afghanistan’s Ministry of Defense/REUTERS
Mvutano kati ya Afghanistan na Pakistan umeongezeka baada ya Kabul kufanya mashambulizi ya kulipiza kisasi, huku milipuko ikisikika mjini Kabul na pande zote zikitoa taarifa kinzani kuhusu vifo na majeruhi.
Mvutano kati ya Afghanistan na Pakistan umeongezeka baada ya Kabul kutangaza mashambulizi ya kulipiza kisasi kufuatia mashambulizi ya anga yaliyofanywa na Islamabad mapema wiki hii.
Milipuko mitatu ilisikika katika mji mkuu wa Afghanistan mapema Ijumaa, huku sauti za ndege zikirindima angani. Hakukuwa na taarifa za haraka kuhusu mahali halisi pa milipuko hiyo au idadi ya majeruhi.
Msemaji wa serikali ya Afghanistan, Zabihullah Mujahid, alisema operesheni kubwa zilianzishwa dhidi ya vituo vya kijeshi vya Pakistan kando ya mpaka wa Durand Line. Wizara ya Ulinzi ya Afghanistan ilisema mashambulizi yalifanyika katika majimbo matano ya mpakani. Kabul inadai kuwa iliteka zaidi ya vituo kumi vya jeshi la Pakistan.
Kwa upande wake, Waziri wa Habari wa Pakistan, Attaullah Tarar, alipinga madai hayo akisema wanajeshi wawili wa Pakistan waliuawa na watatu kujeruhiwa. Aliongeza kuwa wapiganaji 36 wa Afghanistan waliuawa katika mapigano hayo. Serikali ya Pakistan imesema itachukua hatua zote kulinda mipaka yake na usalama wa raia wake.

Wapiganaji wa Taliban wa Afghanistan wakifanya doria karibu na mpaka wa Afghanistan na Pakistan mjini Spin Boldak, Mkoa wa Kandahar, kufuatia mashambulizi ya risasi kati ya vikosi vya Pakistan na Afghanistan nchini Afghanistan, Oktoba 15, 2025.Picha: Stringer/REUTERS
Chanzo cha mvutano
Mapigano pia yaliripotiwa katika eneo la Torkham, mojawapo ya vivuko vikuu vya mpaka kati ya nchi hizo mbili. Wakazi katika pande zote waliondoka katika makazi yao kwa hofu ya mashambulizi zaidi. Maafisa walisema makombora yalirushwa na kuangukia katika vijiji vya karibu, ingawa hakuna vifo vya raia vilivyoripotiwa mara moja.
Mpaka wa kilomita 2,611 unaojulikana kama Msitari wa Durand umekuwa chanzo cha mvutano wa muda mrefu, huku Afghanistan ikiukataa rasmi. Licha ya usitishaji mapigano uliopatanishwa na Qatar, mapigano ya hapa na pale yamekuwa yakiripotiwa. Kuongezeka kwa mashambulizi ya wanamgambo nchini Pakistan, ambayo Islamabad inailaumu TTP, kumeendelea kuzidisha hali ya sintofahamu katika eneo hilo.
Zelensky atarajia mazungumzo mapema Machi Abu Dhabi

Rais Volodymyr Zelenskiy ameeleza matumaini ya kukutana siku moja ana kwa ana na Rais wa Urusi Vladmir Putin.Picha: Kuba Stezycki/REUTERS
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky asema duru ijayo ya mazungumzo na Urusi itafanyika mapema Machi Abu Dhabi, huku mashambulizi ya droni na makombora yakiendelea kuathiri maeneo kadhaa nchini Ukraine.
Rais Volodymyr Zelensky amesema ana matumaini kuwa duru ijayo ya mazungumzo kati ya Ukraine na Urusi itafanyika mapema Machi mjini Abu Dhabi. Kauli hiyo imefuatia mkutano wa maafisa wa Kyiv na wajumbe wa Marekani mjini Geneva. Zelensky amesema kuna utayari mkubwa zaidi wa mfumo wa mazungumzo ya pande tatu.
Amesema lengo ni kukamilisha masuala ya dhamana za usalama na kuandaa mkutano wa ngazi ya juu. Kyiv imekuwa ikisisitiza kuwa mkutano wa ana kwa ana kati ya Zelensky na Vladimir Putin unaweza kuvunja mkwamo wa muda mrefu. Viongozi hao wawili walikutana mara ya mwisho mwaka 2019.
Malengo mapana ya mazungumzo ya Geneva
Mjadiliana mkuu wa Ukraine, Rustem Umerov, alisema mazungumzo ya Geneva yalizingatia pia ujenzi upya wa Ukraine baada ya vita. Aliongeza kuwa pande hizo zimekubaliana misingi itakayounda makubaliano yajayo. Mazungumzo hayo yalihudhuriwa pia na wajumbe wa Marekani.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy na viongozi wa Umoja wa Ulaya wakihudhuria mkutano wa “Muungano wa Hiari,” wakati wa mashambulizi ya Urusi dhidi ya Ukraine, mjini Kyiv, Ukraine, Februari 24, 2026.Picha: Ukrainian Presidential Press Service/Handout via REUTERS
Kwa upande wake, Urusi imesema ni mapema kutabiri tarehe ya makubaliano. Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi, Sergei Lavrov, amesema Moscow haina muda maalum bali inalenga kutimiza malengo yake, ikiwemo udhibiti kamili wa eneo la Donetsk mashariki mwa Ukraine.
Wakati juhudi za kidiplomasia zikiendelea, mashambulizi ya kijeshi hayajasimama. Maafisa wa Ukraine walisema Urusi ilirusha mamia ya droni na makombora, na kusababisha majeruhi na uharibifu katika maeneo kadhaa. Licha ya hali hiyo, Zelensky amesema anaamini mkutano wa Abu Dhabi unaweza kuwa hatua muhimu kuelekea kumaliza vita.
Marekani na Iran zakubaliana kuendelea kuzugumza

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araghchi (kushoto), akikutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Oman, Badr Albusaidi (kulia), mjini Geneva.Picha: Omani Foreign Ministry/AFP
Mazungumzo ya nyuklia kati ya Marekani na Iran yamemalizika Geneva bila makubaliano ya mwisho, huku Trump akiongeza shinikizo la kijeshi na Congress ikitaka ufafanuzi kabla ya hatua yoyote ya vita.
Mazungumzo ya hivi karibuni kati ya Marekani na Iran kuhusu mpango wa nyuklia wa Tehran yamefanyika mjini Geneva chini ya usimamizi wa Oman. Ingawa hakukuwa na makubaliano ya mwisho, wapatanishi walisema kulikuwa na maendeleo muhimu. Pande zote zimekubaliana kuendelea na majadiliano ya kiufundi wiki ijayo mjini Vienna.
Rais Donald Trump amesema anapendelea suluhisho la kidiplomasia lakini yuko tayari kuamuru mashambulizi iwapo mazungumzo yatashindwa. Marekani imekusanya meli za kivita na ndege za kijeshi katika eneo la Ghuba kama ishara ya shinikizo. Hatua hiyo imeongeza hofu ya mzozo mpana wa kikanda.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Oman, Sayyid Badr bin Hamad Al Busaidi (kulia), akikutana na mjumbe maalum wa Ikulu ya Marekani, Steve Witkoff (katikati), pamoja na Jared Kushner.Picha: Foreign Ministry of Oman/AP Photo/picture alliance
Araghchi asifu hatua iliyofikiwa na Marekani
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araghchi, amesema mazungumzo yalikuwa miongoni mwa yaliyo makali zaidi kuwahi kufanyika. Alisema baadhi ya masuala yamepata mwafaka huku mengine yakisalia na tofauti. Iran inasisitiza kuwa mpango wake wa nyuklia ni wa amani na kwa matumizi ya kiraia pekee.
Ndani ya Marekani, wabunge wa Democratic wanahoji malengo ya utawala wa Trump. Wanasema Congress, ambayo ina mamlaka ya kutangaza vita, inapaswa kupewa nafasi ya kujadili kabla ya hatua yoyote ya kijeshi. Mjadala huo umeongeza presha ya kisiasa ndani ya Washington.
Macho sasa yanaelekezwa Vienna ambako mazungumzo ya kiufundi yataanza chini ya usimamizi wa wataalamu wa kimataifa. Hatma ya makubaliano mapya inaweza kuamua iwapo eneo la Mashariki ya Kati litaepuka vita au la.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2026
afghanistan, africa, albania, algeria, America, american-samoa, andorra, angola, anguilla, antarctica, antigua-and-barbuda, argentina, armenia, aruba, arusha, australia, austria, azerbaijan, bahamas, bahrain, bangladesh, barbados, belarus, Belgium, belize, benin, bermuda, bhutan, bolivia, bosnia-and-herzegovina, botswana, Boukinafaso, brazil, brunei-darussalam, bulgaria, burkina-faso, burma, burundi, california, cambodia, cameroon, canada, cape-verde, cayman-islands, central-african-republic, Chad, chicago, chile, china, christmas-island, cocos-keeling-islands, colombia, comoros, congo, cook-islands, costa-rica, cote-divoire-ivory-coast, Croatia, cuba, cyprus, czech-republic, darsalaam, democratic-peoples-rep-north-korea, democratic-republic-of-the-congo-kinshasa, denmark, djibouti, dodoma, dominica, dominican-republic, dr-congo, dubai, east-timor-timor-leste, ecuador, egypt, egypty, el-salvador, england, equatorial-guinea, equitorial-guinea, eritrea, estonia, eswatini, ethiopia, falkland-islands, faroe-islands, federal-states-of-moldova, fiji, finland, Florida, france, french-guiana, french-polynesia, french-southern-territories, gabon, gaza, georgia, germany, ghana, gibraltar, goma, Greece, greenland, grenada, guadeloupe, guam, guatemala, guinea, guinea-bissau, guyana, habari, haiti, holy-see, honduras, hong-kong, houston, hungary, iceland, india, indonesia, Iowa, iran, iran-islamic-republic-of, iraq, ireland, israel, italia, italy, ivory-coast, jamaica, japan, jordan, karatu, kazakhstan, kilimanjaro, kinshasa, kiribati, kiswahili, korea, kosovo, kuwait, kyrgyzstan, lao, latvia-lebanon-lesotho-liberia-libya-liechtenstein-lithuania-luxembourg, Lebanon, liberia, macau, madagascar, malawi, malaysia-maldives, Mali, malta, marshall-islands-martinique-mauritania-mauritius, massechutes, mayotte, mazingira, mbeya, meru, mexico, miami, micronesia, monaco-mongolia-montenegro, montserrat, morocco, mozambique-myanmar, mtwara, mwanza, namibia, nauru, nepal, netherlands, netherlands-antilles, nevada, new-caledonia, new-zealand, newyork, nicaragua, niger, nigeria, niue, north-macedonia, northern-mariana-islands, norway, oman, pakistan, palau, palestine, palestinian-territories, panama, papua-new-guinea, paraguay, peoples-democratic-republic, peru, philadhephia, philipians, Philippines, pitcairn-island, poland, politics, Portugal, puerto-rico, qatar, Norrbottens lan, republic-of-brazzaville, republic-of-south-korea, reunion-island, romania, Russia, russian-federation, rwanda, sahara-occidental, saint-kitts-and-nevis, saint-lucia, saint-vincent-and-the-grenadines, samoa, san-marino, sao-tome-and-principe, saudi-arabia, saudiarabia, scotland, Senegal, serbia, seychelles, sierra-leone, Singapore, singida, slovakia-slovak-republic, slovenia, solomon-islands, somalia, southafrica, spain, sri-lanka, sudan, suriname, swaziland-eswatini, sweden, switzerland, syria, syrian-arab-republic, tabora, taiwan-republic-of-china, tajikistan, tanzania, texas, thailand, the-gambia, tibet, timor-leste-east-timor, togo, tokelau, tonga, toronto, trinidad-and-tobago, tunisia, turkey, turkmenistan, turks-and-caicos-islands, tuvalu, uganda, united-arabs-emirates, united-kingdom, united-states, uruguay, uzbekistan, vancover, vanuatu, vatican-city-state-holy-see, venezuela, vietnam, virgin-islands-british, virgin-islands-u-s, wallis-and-futuna-islands
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.