Na Cantona Joseph
HUENDA Kenya ikanyimwa mikopo baada ya kushushwa hadhi kwenye viwango vya Shirika la Kimataifa la kutathmini Madeni ya Mataifa na Utoaji Mikopo, Moody’s.
Ripoti ya Moody’s iliyotolewa Jumanne inaonyesha kuwa, kutotiwa saini kwa Mswada wa Fedha 2024/25 kumechangia Kenya kushuka viwango na kuwa kati ya nchi zinazoelekea kulemewa na madeni.
Kwa mujibu wa shirika hilo, inaonekana Kenya haitafanikiwa pakubwa kujiondoa hatarini hata katika mikakati ya kupunguza matumizi ya serikali.
Rais William Ruto aliondoa Mswada wa Fedha 2024 kutokana na wimbi la maandamano lililoshuhudiwa nchini kwa kuwa mapendekezo mengi ya ushuru yalikuwa katika mswada huo.
Kati ya sababu ambazo zilisababisha raia, hasa vijana wapinge mswada huo ni ushuru ambao ungeongezwa kwenye ununuzi na matumizi ya magari, kutuma na kutoa pesa na pia bei ya mkate kupanda maradufu.
Moody’s pia imeonya kuwa, huenda Kenya ikalemewa kuyalipa madeni yake na sasa imeorodheshwa miongoni mwa nchi hatari zaidi kupewa mikopo na mashirika ya kimataifa.
Mnamo Juni, shirika hilo lilitoa ripoti iliyoweka Ghana pabaya katika kuyalipa madeni yake. Nchi hiyo hatimaye ililemewa kabisa na sasa inashiriki mikakati ya kubana matumizi yake kulipa madeni mengi yanayoiandama.
Baada ya mswada wa fedha kuondolewa, serikali ya Kenya imeamua kupunguza malengo yake ya mapato ya ushuru mwaka wa fedha wa 2024/25 kwa Sh177 bilioni. Kando na hayo, pia imetangaza kuwa itapunguza matumizi katika afisi na idara mbalimbali za serikali kuanzia afisi ya Rais.
“Kushuka kwa nafasi ya Kenya kunaonyesha nchi haina uwezo wa kuyakusanya mapato ya kutosha ya kulipa madeni yake. Kwa hivyo, Kenya itakuwa ikitatizika sana kulipa madeni hayo kwa sababu ya kutaofikia mapato lengwa,” ikasema taarifa ya Shirika la Moody’s Jumanne.
Hasa shirika hilo lilisema kuwa, kupunguza matumizi hakutasaidia kwa sababu kiasi kikubwa cha ushuru kinaelekezwa katika kuyalipa madeni na hilo ni jambo ambalo haliwezi kuepukiwa kwa sasa.
Moja ya neno ambalo huwezi kuliepuka kwenye maisha yako ni kuambiwa “HAPANA”.
Unaweza kuomba kazi ukakataliwa, unaweza kumpenda mtu na ukamuambia akakupa jibu la HAPANA.
Kuna wakati unaweza kupambania fursa fulani, ukampigia mtu SIMU au ukaenda KUMUONA akakuambia HAPANA.
Jifunze, kuelewa unapoambiwa HAPANA. Haimaanishi kwamba umefika mwisho, ila inamaanisha TAFUTA NAMNA NYINGINE.
Unaeweza kumuomba MTU PESA, ukimuangalia unaona ANAZO, ila akakuambia HAPANA. Usijenge naye CHUKI.
Hapana ni sehemu ya maisha, ni jambo ambalo huwezi KULIEPUKA katika safari yako ya mafanikio.
Ukiambia HAPANA USISUSE, wala USIKASIRIKE.
Tafuta MBINU NYINGINE!
Natumai makala hii imekusaidia.
Kama imekusaidia na umeipenda na unataka ujifunze zaidi…
All Rights Reserved ©Cantona Group Ltd||2024
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.