Ruto awaalika Arsenal Kenya baada ya sherehe za kukata na shoka

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Na Cantona Joseph June 18, 2026 06:00 (EAT)



Rais William Ruto amewaalika mabingwa wa Ligi Kuu ya Uingereza Arsenal kutembelea Kenya kufuatia sherehe zilizojumuisha shangwe, nderemo na vifijo kutoka kwa mashabiki wao baada ya klabu hiyo kumaliza kiu ya muda mrefu kwa kupata ushindi wa taji la ligi.

Rais alisema alishangazwa na ukubwa wa sherehe zilizoshuhudiwa jijini Nairobi baada ya Arsenal kutwaa ubingwa.

Akizungumza na Reuters wakati wa Mkutano wa G7 nchini Ufaransa, Rais alibainisha kuwa msisimko miongoni mwa mashabiki wa Kenya ulimfanya afuatilie uwezekano wa kuileta klabu hiyo ya Kaskazini mwa London nchini humo mwaka ujao.

abu hiyo.

.

“Arsenal hatimaye ilipata ubingwa, na kuwa sherehe kubwa. Nilishangaa sana kilichotokea jijini Nairobi,” Ruto alisema.

“Ilikuwa sherehe kubwa, najaribu kufuatilia kama Arsenali wanaweza kuja nchini mwaka ujao. Nimetuma mwaliko kwa sababu nafikiria itakuwa wakati mzuri kwa Arsenal kuja Kenya. Wana mashabiki wa kipekee.”

Kenya ni mojawapo ya nchini zenye mashabiki wengi wa Arsenal barani Afrika na mashabiki hukusanyika mara kwa mara katika miji mikubwa mbalimbali kutazama mechi za kl

.
Maelezo ya picha,Shabiki wa Arsenal

Ushindi wa taji la Gunners ulisababisha sherehe kote nchini Kenya, huku mashabiki wakijitokeza mitaani, katika mitandao ya kijamii na sehemu za burudani kuadhimisha ushindi wa kihistoria wa klabu hiyo.

Urusi na Ukraine zashambuliana huku Zelensky akizungumza na Trump, Ulaya

.

Urusi imeshambulia Kyiv kwa makombora na ndege zisizo na rubani za Ukraine katika kiwanda cha kusafishia mafuta cha Moscow huku nchi zote mbili zikishambuliana saa chache baada ya Rais Volodymyr Zelensky kuzungumza na Rais wa Marekani Donald Trump na viongozi wa Ulaya.

Kwa mujibu wa Reuters alisikia milipuko huko Kyiv na mamlaka katika mji wa Sumy kaskazini mashariki mwa Ukraine zilisema mtu mmoja aliuawa katika shambulio la ndege isiyo na rubani.

Tahadhari za mashambulizi ya anga zilitolewa kwa eneo kubwa la Ukraine.

“Adui anashambulia mji mkuu kwa makombora ya balestiki. Kaeni katika maeneo salama hadi tahadhari ya uvamizi wa anga itakapoondolewa!” Tymur Tkachenko, mkuu wa utawala wa kijeshi wa Kyiv, alisema katika chapisho la Telegram mapema Alhamisi.

Shambulio dhidi ya Kyiv ni la pili wiki hii na limetokea huku Zelensky akijaribu kuongeza shinikizo kwa Urusi ili kujadili kukomesha vita vyake vya miaka minne.

Katika mji mkuu wa Urusi, ndege zisizo na rubani zilishambulia kiwanda cha kusafishia mafuta cha Moscow, Meya Sergei Sobyanin alisema kwenye Telegram, akiashiria shambulio la pili kwenye kituo hicho ndani ya wiki moja.

Trump na rais wa Iran watia saini mkataba wa awali unaolenga kumaliza vita

.

Viongozi wa Marekani na Iran wamesaini makubaliano ya awali ya amani yanayolenga kukomesha vita hivyo, na kuanza kutekelezwa mara moja.

Mkataba huo unajumuisha kufungua tena Mlango-Bahari wa Hormuz, mpango wa dola bilioni 300 (£224bn) kwa ajili ya “ujenzi mpya” wa Iran, na Marekani kukomesha “aina zote za vikwazo” dhidi ya Iran.

Lakini suala la mpango wa nyuklia wa Iran, sababu kuu iliyotajwa na Marekani kwa mzozo huo, bado halijajadiliwa kwa muda wa siku 60 za kusitisha mapigano ulioongezwa.

Rais wa Marekani Donald Trump, ambaye alisaini makubaliano hayo nchini Ufaransa wakati wa mkutano wa kilele wa G7, alitetea pendekezo hilo, akisema litaepusha “janga la kiuchumi”. Hata hivyo, alionya kwamba Marekani “itaishambulia” Iran ikiwa hakuna makubaliano ya mwisho yatakayofikiwa.

Rais wa Iran Masoud Pezeshkian pia alisaini hati hiyo Jumatano, Tehran ilithibitisha.

Spika wa bunge la Iran na mjumbe mkuu wa mazungumzo Mohammad Bagher Ghalibaf aliviambia vyombo vya habari vya serikali kwamba imani yake kwa Marekani bado ipo, na Iran “iko katika hali ya tahadhari”.

“Ikiwa adui haelewi lugha ya mantiki, tutaingia tena na lugha ya nguvu,” aliambia chombo cha habaro cha serikali cha Fars.

Marekani na Israel zilianzisha vita dhidi ya Iran mnamo tarehe 28 Februari, na kumuua Kiongozi Mkuu Ayatollah Ali Khamenei na maafisa wakuu wa kijeshi siku ya kwanza.

Trump aliwaambia waandishi wa habari nchini Ufaransa katika eneo la mapumziko la Evian-les-Bains kando ya ziwa, ambapo mkutano wa kilele wa G7 uliandaliwa, kwamba mpango huo utaepusha ” dhiki kwa dunia nzima”.

“Sikutaka kuona janga la kiuchumi,” Trump aliwaambia waandishi wa habari. “Kama ungeendelea hivi, hilo lingetokea.”

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2026

afghanistanafricaalbaniaalgeriaAmericaamerican-samoaandorraangolaanguillaantarcticaantigua-and-barbudaargentinaarmeniaarubaarushaaustraliaaustriaazerbaijanbahamasbahrainbangladeshbarbadosbelarusBelgiumbelizebeninbermudabhutanboliviabosnia-and-herzegovinabotswanaBoukinafasobrazilbrunei-darussalambulgariaburkina-fasoburmaburundicaliforniacambodiacamerooncanadacape-verdecayman-islandscentral-african-republicChadchicagochilechinachristmas-islandcocos-keeling-islandscolombiacomoroscongocook-islandscosta-ricacote-divoire-ivory-coastCroatiacubacyprusczech-republicdarsalaamdemocratic-peoples-rep-north-koreademocratic-republic-of-the-congo-kinshasadenmarkdjiboutidodomadominicadominican-republicdr-congodubaieast-timor-timor-lesteecuadoregyptegyptyel-salvadorenglandequatorial-guineaequitorial-guineaeritreaestoniaeswatiniethiopiafalkland-islandsfaroe-islandsfederal-states-of-moldovafijifinlandFloridafrancefrench-guianafrench-polynesiafrench-southern-territoriesgabongazageorgiagermanyghanagibraltargomaGreecegreenlandgrenadaguadeloupeguamguatemalaguineaguinea-bissauguyanahabarihaitiholy-seehondurashong-konghoustonhungaryicelandindiaindonesiaIowairaniran-islamic-republic-ofiraqirelandisraelitaliaitalyivory-coastjamaicajapanjordankaratukazakhstankilimanjarokinshasakiribatikiswahilikoreakosovokuwaitkyrgyzstanlaolatvia-lebanon-lesotho-liberia-libya-liechtenstein-lithuania-luxembourgLebanonliberiamacaumadagascarmalawimalaysia-maldivesMalimaltamarshall-islands-martinique-mauritania-mauritiusmassechutesmayottemazingirambeyamerumexicomiamimicronesiamonaco-mongolia-montenegromontserratmoroccomozambique-myanmarmtwaramwanzanamibianaurunepalnetherlandsnetherlands-antillesnevadanew-caledonianew-zealandnewyorknicaraguanigernigerianiuenorth-macedonianorthern-mariana-islandsnorwayomanpakistanpalaupalestinepalestinian-territoriespanamapapua-new-guineaparaguaypeoples-democratic-republicperuphiladhephiaphilipiansPhilippinespitcairn-islandpolandpoliticsPortugalpuerto-ricoqatarrepublic-ofrepublic-of-brazzavillerepublic-of-south-koreareunion-islandromaniaRussiarussian-federationrwandasahara-occidentalsaint-kitts-and-nevissaint-luciasaint-vincent-and-the-grenadinessamoasan-marinosao-tome-and-principesaudi-arabiasaudiarabiascotlandSenegalserbiaseychellessierra-leoneSingaporesingidaslovakia-slovak-republicsloveniasolomon-islandssomaliasouthafricaspainsri-lankasudansurinameswaziland-eswatiniswedenswitzerlandsyriasyrian-arab-republictaborataiwan-republic-of-chinatajikistantanzaniatexasthailandthe-gambiatibettimor-leste-east-timortogotokelautongatorontotrinidad-and-tobagotunisiaturkeyturkmenistanturks-and-caicos-islandstuvaluugandaunited-arabs-emiratesunited-kingdomunited-statesuruguayuzbekistanvancovervanuatuvatican-city-state-holy-seevenezuelavietnamvirgin-islands-britishvirgin-islands-u-swallis-and-futuna-islandswallis-and-futuna-islandswallis-et-futunawashington-dcwestern-saharayemenzambiazambiezimbabwe

CantonaDigital
CantonaDigital

Listen Live Radio Fortune Africa
Ukweli Na Burudani.

-Be ready to be Impacted, Inspired & Empowered.

-Keep watching our Channels

Cantona Cast Television,

Fortune Television Network (FTN)

Donation
Paypal https://www.paypal.com/donate/?hosted_button_id=6EKXMLNW8W6A2&fbclid=IwY2xjawQxeChleHRuA2FlbQIxMABicmlkETFRdkNBRndpclRDQTB5bXZZc3J0YwZhcHBfaWQQMjIyMDM5MTc4ODIwMDg5MgABHq960uGsyU3ABRIBc2h-iXGhHATvuEqe55gFsQ-rDb0fT-Z7SIQ3TV8LnkpD_aem_ybU2SvBlvyqrVsS9NAczRw

An attitude determines an altitude.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025

5,421 posts
0 followers

Fediverse Followers


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a Reply