Kombe la dunia: Ghana yapata ushindi wa 1- 0 dhidi ya Panama

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Na Cantona Joseph June 18, 2026 06:00 (EAT)

Ghana ilipata bao lake muhimu dhidi ya Panama katika dakika ya 95.
Ghana ilipata bao lake muhimu dhidi ya Panama katika dakika ya 95. IMAGN IMAGES via Reuters – KEVIN SOUSA

Mshambuliaji wa Ghana Caleb Yirenkyi, alifungia bao katika ya 95 na kuipa Ghana ushindi wa 1-0 dhidi ya Panama katika mchezo wa Kombe la Dunia uliochezwa Toronto, Canada na kuwanyima Panama alama katika historia ya mashindano ya kombe la Dunia.

Bao hilo lilipatikana katika dakika sita za nyongeza, ambapo Brandon Thomas Asante alikimbia upande wa kushoto, akamzidi beki wake na kutoa pasi ya mwisho iliyomfikia Yirenkyi, ambaye alimalizia kwa urahisi na kuamua matokeo ya mchezo.

Mechi ya Ghana dhidi ya Panama katika uwanja wa Toronto, Canada.
Mechi ya Ghana dhidi ya Panama katika uwanja wa Toronto, Canada. REUTERS – Piroschka Van De Wouw

Matokeo hayo yalikuwa ya maumivu kwa Panama, ambao walionyesha ushindani mkubwa dhidi ya mabingwa hao wa Afrika mara nne katika mashindano yao ya nne ya Kombe la Dunia tangu mwaka 2018.

Katika mechi hiyo Panama walikaribia kufunga mapema baada ya Cecilio Waterman kupiga shuti lililookolewa na kipa wa Ghana, Lawrence Ati Zigi dakika za mwanzo. Kipindi cha pili Cristian Martinez alikosa nafasi nzuri baada ya kupiga mpira uliogonga pembeni ya lango akiwa karibu kabisa na goli.

Mashabiki wa timu ya taifa ya Ghana wakati wa mechi ya kombe la dunia dhidi ya Panama.
Mashabiki wa timu ya taifa ya Ghana wakati wa mechi ya kombe la dunia dhidi ya Panama. IMAGN IMAGES via Reuters – KEVIN SOUSA

Isitoshe Ghana ambayo ilicheza bila kiungo Thomas Partey baada ya kuzuiwa kuingia Canada kutokana na kesi inayoendelea nchini Uingereza, ilipata ushindi huo wa kuchelewa ambao ni bao la ushindi lililofungwa kwa muda wa juu zaidi katika Kombe la Dunia la mwaka huu.

Timu hiyo sasa itamenyana na England katika mchezo wake ujao wa Kundi L mjini Boston, huku Panama ikitarajia kurekodi matokeo bora dhidi ya Croatia katika mchezo wao unaofuata Toronto.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2026

afghanistanafricaalbaniaalgeriaAmericaamerican-samoaandorraangolaanguillaantarcticaantigua-and-barbudaargentinaarmeniaarubaarushaaustraliaaustriaazerbaijanbahamasbahrainbangladeshbarbadosbelarusBelgiumbelizebeninbermudabhutanboliviabosnia-and-herzegovinabotswanaBoukinafasobrazilbrunei-darussalambulgariaburkina-fasoburmaburundicaliforniacambodiacamerooncanadacape-verdecayman-islandscentral-african-republicChadchicagochilechinachristmas-islandcocos-keeling-islandscolombiacomoroscongocook-islandscosta-ricacote-divoire-ivory-coastCroatiacubacyprusczech-republicdarsalaamdemocratic-peoples-rep-north-koreademocratic-republic-of-the-congo-kinshasadenmarkdjiboutidodomadominicadominican-republicdr-congodubaieast-timor-timor-lesteecuadoregyptegyptyel-salvadorenglandequatorial-guineaequitorial-guineaeritreaestoniaeswatiniethiopiafalkland-islandsfaroe-islandsfederal-states-of-moldovafijifinlandFloridafrancefrench-guianafrench-polynesiafrench-southern-territoriesgabongazageorgiagermanyghanagibraltargomaGreecegreenlandgrenadaguadeloupeguamguatemalaguineaguinea-bissauguyanahabarihaitiholy-seehondurashong-konghoustonhungaryicelandindiaindonesiaIowairaniran-islamic-republic-ofiraqirelandisraelitaliaitalyivory-coastjamaicajapanjordankaratukazakhstankilimanjarokinshasakiribatikiswahilikoreakosovokuwaitkyrgyzstanlaolatvia-lebanon-lesotho-liberia-libya-liechtenstein-lithuania-luxembourgLebanonliberiamacaumadagascarmalawimalaysia-maldivesMalimaltamarshall-islands-martinique-mauritania-mauritiusmassechutesmayottemazingirambeyamerumexicomiamimicronesiamonaco-mongolia-montenegromontserratmoroccomozambique-myanmarmtwaramwanzanamibianaurunepalnetherlandsnetherlands-antillesnevadanew-caledonianew-zealandnewyorknicaraguanigernigerianiuenorth-macedonianorthern-mariana-islandsnorwayomanpakistanpalaupalestinepalestinian-territoriespanamapapua-new-guineaparaguaypeoples-democratic-republicperuphiladhephiaphilipiansPhilippinespitcairn-islandpolandpoliticsPortugalpuerto-ricoqatarrepublic-ofrepublic-of-brazzavillerepublic-of-south-koreareunion-islandromaniaRussiarussian-federationrwandasahara-occidentalsaint-kitts-and-nevissaint-luciasaint-vincent-and-the-grenadinessamoasan-marinosao-tome-and-principesaudi-arabiasaudiarabiascotlandSenegalserbiaseychellessierra-leoneSingaporesingidaslovakia-slovak-republicsloveniasolomon-islandssomaliasouthafricaspainsri-lankasudansurinameswaziland-eswatiniswedenswitzerlandsyriasyrian-arab-republictaborataiwan-republic-of-chinatajikistantanzaniatexasthailandthe-gambiatibettimor-leste-east-timortogotokelautongatorontotrinidad-and-tobagotunisiaturkeyturkmenistanturks-and-caicos-islandstuvaluugandaunited-arabs-emiratesunited-kingdomunited-statesuruguayuzbekistanvancovervanuatuvatican-city-state-holy-seevenezuelavietnamvirgin-islands-britishvirgin-islands-u-swallis-and-futuna-islandswallis-and-futuna-islandswallis-et-futunawashington-dcwestern-saharayemenzambiazambiezimbabwe

CantonaDigital
CantonaDigital

Listen Live Radio Fortune Africa
Ukweli Na Burudani.

-Be ready to be Impacted, Inspired & Empowered.

-Keep watching our Channels

Cantona Cast Television,

Fortune Television Network (FTN)

Donation
Paypal https://www.paypal.com/donate/?hosted_button_id=6EKXMLNW8W6A2&fbclid=IwY2xjawQxeChleHRuA2FlbQIxMABicmlkETFRdkNBRndpclRDQTB5bXZZc3J0YwZhcHBfaWQQMjIyMDM5MTc4ODIwMDg5MgABHq960uGsyU3ABRIBc2h-iXGhHATvuEqe55gFsQ-rDb0fT-Z7SIQ3TV8LnkpD_aem_ybU2SvBlvyqrVsS9NAczRw

An attitude determines an altitude.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025

5,458 posts
0 followers

Fediverse Followers


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a Reply