
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa
Na Cantona Joseph 10, 2026 06:00 (EAT)


Wanamgambo wa RSF wakiwa katika operesheni zake, El-Fasher Sudan.Picha: Rapid Support Forces (RSF)/AFP
Waathirika wa ukatili wa RSF Sudan wamewasilisha malalamiko Kenya, wakidai mateso makali na ukatili wa kingono.
Waathirika 12 wa ukatili unaodaiwa kufanywa katika vita vya Sudan wamefikisha malalamiko nchini Kenya wakitaka uchunguzi dhidi ya wanamgambo wa RSF.
Malalamiko hayo, yaliyowasilishwa na shirika la kimataifa Legal Action Worldwide, yanadai mateso na ukatili wa kingono uliofanywa na RSF katika maeneo ya Khartoum kati ya Aprili 2023 na Machi 2025, kipindi ambacho mji mkuu ulikuwa chini ya wanamgambo hao.
Waathiriwa wanamtaka Mkurugenzi wa Mashtaka Kenya kuidhinisha mashitaka dhidi ya wanachama 10 wa RSF, baadhi yao wakiaminika kuishi Kenya.
Aidha wanadai kwamba walishikiliwa katika mazingira ya kinyama, wakipigwa, kuchomwa, kunyimwa chakula na maji, kuteswa kwa umeme na kubakwa. Baadhi walilazimishwa kubeba miili ya waliouawa.
Shirika hilo linataka Kenya kutumia Sheria ya Uhalifu wa Kimataifa ya 2008, likisema Sudan haiwezi kutoa haki kwa sasa. RSF, iliyoibuka kutoka wanamgambo wa Janjaweed, imekuwa ikituhumiwa na mashirika ya haki za binadamu na Umoja wa Mataifa kwa uhalifu wa kivita, hasa Darfur.
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.