Taliban yavunja maandamano ya haki za wanawake Afghanistan

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Na Cantona Joseph 10, 2026 06:00 (EAT)

Vocalize Pre-Player Loader

Maandamano yalianza baada ya maafisa wa Wizara ya Maadili kujaribu kuwakamata wanawake waliopinga sheria za kuvaa hijabu.Picha: David Canales/SOPA Images/ZUMA/picture alliance

Maandamano ya wanawake yazimwa na maafisa wa usalama Herat. Mashuhuda wakiripoti mauwaji ya mtu mmoja na wengine wamejeruhiwa.

Maafisa wa usalama wa Afghanistan wamezima maandamano ya kutetea haki za wanawake katika mkoa wa Herat magharibi mwa nchi hiyo baada ya taarifa kwamba polisi wa maadili waliwakamata wanawake kwa tuhuma za kukiuka sheria za mavazi ya lazima.

Kwa mujibu wa mashuhuda mtu mmoja ameuwawa na wengine kadhaa wamejeruhiwa na watu kadhaa wakiwemo wanawake na wasichana wamekamatwa. Hata hivyo, mamlaka ya Taliban haijathibitisha vifo wala kamatakamata hizo.

Msemaji wa polisi wa Herat, Sayed Masoud Hossein amesema mkusanyiko huo uliharibu utulivu kwa kupinga vazi la hijabu, ambayo aliitaja kuwa wajibu wa kidini. Mashuhuda wanasema maandamano yalianza baada ya maafisa wa Wizara ya Maadili kujaribu kuwakamata wanawake waliopinga sheria hizo, huku baadhi ya waliolengwa wakiwa tayari wamefunika miili yao kikamilifu.

Video kutoka Herat inaonyesha maafisa wenye silaha wakitawanya waandamanaji, na milio ya risasi ikisikika.  Tangu Taliban ilipochukua madaraka mwaka 2021, imeweka vikwazo vikali kwa wanawake na wasichana katika elimu, ajira na michezo, jambo ambalo limeendelea kukosolewa kimataifa.

CantonaDigital
CantonaDigital

Listen Live Radio Fortune Africa
Ukweli Na Burudani.

-Be ready to be Impacted, Inspired & Empowered.

-Keep watching our Channels

Cantona Cast Television,

Fortune Television Network (FTN)

Donation
Paypal https://www.paypal.com/donate/?hosted_button_id=6EKXMLNW8W6A2&fbclid=IwY2xjawQxeChleHRuA2FlbQIxMABicmlkETFRdkNBRndpclRDQTB5bXZZc3J0YwZhcHBfaWQQMjIyMDM5MTc4ODIwMDg5MgABHq960uGsyU3ABRIBc2h-iXGhHATvuEqe55gFsQ-rDb0fT-Z7SIQ3TV8LnkpD_aem_ybU2SvBlvyqrVsS9NAczRw

An attitude determines an altitude.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025

5,388 posts
0 followers

Fediverse Followers


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a Reply