Iran, Marekani na Israel zasitisha mapigano kwa wiki mbili

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Na Cantona Joseph April 08, 2026 16:08 (EAT)

Vocalize Pre-Player Loader

Iran, Marekani na Israel zasitisha mapigano kwa wiki mbiliPicha: DW

Iran, Marekani na Israel zimefikia makubaliano ya kusitisha mapigano kwa muda wa wiki mbili. Hata hivyo, bado kuna mkanganyiko kuhusu vipengee vya mpango huo.

Iran imekubali kuufungua Mlango-Bahari wa Hormuz na ikasisitiza kuwa itazitoza ushuru meli zitakazopita eneo hilo na kwamba itaendelea pia kurutubisha madini yake ya urani na kwamba adui amepata pigo kubwa la kihistoria.

Kwa upande wake, Rais Donald Trump amesema Marekani imepata ushindi kwa kufikia makubaliano hayo na kwamba lengo kuu la vita hivyo ni kuusambaratisha kabisa mpango wa nyuklia wa Iran.

Israel imetangaza  kuunga mkono makubaliano hayo  lakini Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu amesema hatositisha mapigano dhidi ya kundi la Hezbollah nchini Lebanon, kauli inayokinzana na tamko la Pakistan, ambayo ndiyo mpatanishi katika mzozo huo.

Mataifa yapongeza usitishaji mapigano katika vita vya Iran

Ufaransa na Saudi Arabia ni miongoni mwa nchi zilizopongeza hatua ya usitishwaji mapigano kati ya Iran, Marekani na Israel.Picha: NICOLAS TUCAT/AFP/Getty Images

Nchi za kiarabu, Umoja wa Ulaya, China, Uturuki, Japan na nyinginezo zimepongeza hatua ya Iran, Marekani na Israel kusitisha mapigano kwa muda wa wiki mbili.

Mataifa hayo yametaka kuheshimiwa kwa makubaliano hayo huku Saudi Arabia ikitumai kuwa mpango huo utawezesha kurejesha utulivu kamili na wa kudumu Mashariki ya Kati.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amesema diplomasia pekee ndio njia sahihi ya kufikia amani na usalama  na kwamba kutangazwa huku kwa usitishaji mapigano ni jambo zuri sana.

Hata hivyo, Kiongozi mkuu wa upinzani wa Israel, Yair Lapid, amekosoa vikali hatua ya Netanyahu kuunga mkono usitishaji vita na kuitaja kuwa “janga la kisiasa” huku akimtuhumu Waziri Mkuu huyo kwa kushindwa kufikia malengo ya vita na kutokomeza kabisa kitisho kwa Israel.

Waziri wa Mambo ya Nje wa China kusafiri Korea Kaskazini

Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang YiPicha: Mandel Ngan/AP/picture alliance

Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi atasafiri siku ya Alhamisi kuelekea Korea Kaskazini, ziara inayolenga kuimarisha mahusiano kati ya majirani hao.

China ni mshirika mkubwa wa kibiashara wa Korea Kaskazini na imekua ikitoa msaada muhimu katika masuala ya kidiplomasia, kiuchumi na kisiasa kwa taifa hilo lililotengwa.

Ziara ya siku mbili ya Wang Yi inachukuliwa kama hatua “muhimu” katika kudumisha na  kuendeleza uhusiano kati ya China na Korea Kaskazini. 

Wiki iliyopita, shirika la ndege la “Air China” lilianzisha tena safari za moja kwa moja kati ya Beijing na Pyongyang baada kuzisitisha kwa miaka sita kutokana na janga la UVIKO-19.

Ukraine yasema kuwa tayari kwa makubaliano ya kumaliza vita

Picha: Tetiana Dzhafarova/AFP

Rais Volodymyr Zelensky wa Ukraine amesema nchi yake iko tayari kwa mpango wa usitishaji mapigano na Urusi, huku akimtolea wito rais wa Marekani Donald Trump kuishinikiza Moscow kusitisha uvamizi wake.

Aidha, Waziri wa Mambo ya Nje wa Ukraine Andriy Sybiha amesema makubaliano ya kusitisha mapigano kati ya Marekani na Iran yanaonyesha mafanikio ya “uamuzi” wa Marekani na kuitaka Washington isiupuuze mzozo wa Ukraine.

Hayo yakiripotiwa, Urusi na Ukraine zimeendelea kushambuliana usiku kucha,  huku shambulizi la droni la Moscow likisababisha uharibifu mkubwa kwenye bandari ya mji wa Izmail iliyopo kwenye mto Danube kusini-magharibi mwa Ukraine.

afghanistanafricaalbaniaalgeriaAmericaamerican-samoaandorraangolaanguillaantarcticaantigua-and-barbudaargentinaarmeniaarubaarushaaustraliaaustriaazerbaijanbahamasbahrainbangladeshbarbadosbelarusBelgiumbelizebeninbermudabhutanboliviabosnia-and-herzegovinabotswanaBoukinafasobrazilbrunei-darussalambulgariaburkina-fasoburmaburundicaliforniacambodiacamerooncanadacape-verdecayman-islandscentral-african-republicChadchicagochilechinachristmas-islandcocos-keeling-islandscolombiacomoroscongocook-islandscosta-ricacote-divoire-ivory-coastCroatiacubacyprusczech-republicdarsalaamdemocratic-peoples-rep-north-koreademocratic-republic-of-the-congo-kinshasadenmarkdjiboutidodomadominicadominican-republicdr-congodubaieast-timor-timor-lesteecuadoregyptegyptyel-salvadorenglandequatorial-guineaequitorial-guineaeritreaestoniaeswatiniethiopiafalkland-islandsfaroe-islandsfederal-states-of-moldovafijifinlandFloridafrancefrench-guianafrench-polynesiafrench-southern-territoriesgabongazageorgiagermanyghanagibraltargomaGreecegreenlandgrenadaguadeloupeguamguatemalaguineaguinea-bissauguyanahabarihaitiholy-seehondurashong-konghoustonhungaryicelandindiaindonesiaIowairaniran-islamic-republic-ofiraqirelandisraelitaliaitalyivory-coastjamaicajapanjordankaratukazakhstankilimanjarokinshasakiribatikiswahilikoreakosovokuwaitkyrgyzstanlaolatvia-lebanon-lesotho-liberia-libya-liechtenstein-lithuania-luxembourgLebanonliberiamacaumadagascarmalawimalaysia-maldivesMalimaltamarshall-islands-martinique-mauritania-mauritiusmassechutesmayottemazingirambeyamerumexicomiamimicronesiamonaco-mongolia-montenegromontserratmoroccomozambique-myanmarmtwaramwanzanamibianaurunepalnetherlandsnetherlands-antillesnevadanew-caledonianew-zealandnewyorknicaraguanigernigerianiuenorth-macedonianorthern-mariana-islandsnorwayomanpakistanpalaupalestinepalestinian-territoriespanamapapua-new-guineaparaguaypeoples-democratic-republicperuphiladhephiaphilipiansPhilippinespitcairn-islandpolandpoliticsPortugalpuerto-ricoqatarrepublic-ofrepublic-of-brazzavillerepublic-of-south-koreareunion-islandromaniaRussiarussian-federationrwandasahara-occidentalsaint-kitts-and-nevissaint-luciasaint-vincent-and-the-grenadinessamoasan-marinosao-tome-and-principesaudi-arabiasaudiarabiascotlandSenegalserbiaseychellessierra-leoneSingaporesingidaslovakia-slovak-republicsloveniasolomon-islandssomaliasouthafricaspainsri-lankasudansurinameswaziland-eswatiniswedenswitzerlandsyriasyrian-arab-republictaborataiwan-republic-of-chinatajikistantanzaniatexasthailandthe-gambiatibettimor-leste-east-timortogotokelautongatorontotrinidad-and-tobagotunisiaturkeyturkmenistanturks-and-caicos-islandstuvaluugandaunited-arabs-emiratesunited-kingdomunited-statesuruguayuzbekistanvancovervanuatuvatican-city-state-holy-seevenezuelavietnamvirgin-islands-britishvirgin-islands-u-swallis-and-futuna-islandswallis-and-futuna-islandswallis-et-futunawashington-dcwestern-saharayemenzambiazambiezimbabwe

CantonaDigital
CantonaDigital

Listen Live Radio Fortune Africa
Ukweli Na Burudani.

-Be ready to be Impacted, Inspired & Empowered.

-Keep watching our Channels

Cantona Cast Television,

Fortune Television Network (FTN)

Donation
Paypal https://www.paypal.com/donate/?hosted_button_id=6EKXMLNW8W6A2&fbclid=IwY2xjawQxeChleHRuA2FlbQIxMABicmlkETFRdkNBRndpclRDQTB5bXZZc3J0YwZhcHBfaWQQMjIyMDM5MTc4ODIwMDg5MgABHq960uGsyU3ABRIBc2h-iXGhHATvuEqe55gFsQ-rDb0fT-Z7SIQ3TV8LnkpD_aem_ybU2SvBlvyqrVsS9NAczRw

An attitude determines an altitude.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025

5,415 posts
0 followers

Fediverse Followers


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a Reply