Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa
Na Cantona Joseph Imechapishwa: March 24, 2026 06:32 (EAT)



Iran ilirusha makombora kuelekea Israel mapema Jumanne lakini mitambo ya Israel ya ulinzi wa anga iliyadunguaPicha: Jack Guez/AFP/Getty Images
Iran ilirusha makombora kuelekea Israel mapema Jumanne, saa chache baada ya Rais wa Marekani Donald Trump kutangaza kwamba Washington ilifanya mazungumzo na afisa wa Iran ambaye hakutajwa.
Jeshi lilisema shambulio la hivi karibuni la makombora ya Iran lililenga kaskazini mwa Israel na kwamba “linafanya juhudi za kuzuia tishio hilo”. Rais Trump Jumatatu alisifu kile alichokiita mazungumzo “mazuri sana” na afisa wa Iranambaye hakumtaja baada ya kuahirisha ghafla mipango ya mashambulizi mapya. “Nadhani kuna uwezekano mkubwa kwamba tutafikia makubaliano. Na kwa hivyo tunaipa siku tano, na kisha tutaona itakavyokuwa. Na naweza kusema, baada ya kipindi hiki, nadhani huenda tukawa na makubaliano mazuri sana.”
Ufichuzi huo wa kushangaza wa kuwepo mazungumzo — uliokanushwa na Tehran, ambayo ilimtuhumu Trump kwa kutaka kushawishi masoko ya nishati — ulijiri kabla ya muda wa mwisho wa Jumatatu usiku uliowekwa na Trump kwa Iran kufungua tena Mlango-Bahari wa Hormuz la sivyo Marekani “iiteketeze” mitambo yake ya umeme.

Trump alisifu mazungumzo “mazuri sana” na afisa wa Iran baada ya kuahirisha ghafla mipango ya mashambulizi mapyaPicha: Saul Loeb/AFP/Getty Images
Bei ya mafuta ilishuka na masoko ya hisa yakaimarika huku waangalizi wakijitahidi kutafsiri kauli za Trump licha ya Iran kukataa.
Tovuti ya Habari ya Axios nchini Marekani, ikimnukuu afisa mmoja wa Israel ambaye hakutajwa jina, ilimtaja mtu aliyezungumza na Trump kuwa ni Mohammad Bagher Ghalibaf, spika wa bunge la Iran na mmoja wa watu mashuhuri wasio na nafasi ya kidini.
Tovuti hiyo na shirika la Habari la habari la Reuters waliripoti kwamba wapatanishi wa Marekani Steve Witkoff na Jared Kushner wanaweza kukutana na ujumbe wa Iran kwa mazungumzo nchini Pakistani wiki hii, huku kukiwa na uwezekano wa Makamu wa Rais JD Vance kujiunga.
Waziri Mkuu wa Pakistan Shehbaz Sharif Jumatatu alisema alizungumza na Rais Masoud Pezeshkian wa Iran, akiahidi msaada wa Islamabad kuleta amani katika eneo hilo.
Lakini Ghalibaf alisema kwenye mtandao wa X kwamba “hakuna mazungumzo” yanayoendelea, akisisitiza kwamba Trump alikuwa akitaka “kudhibiti masoko ya fedha na mafuta.”

Israel imepanua operesheni yake dhidi ya wanamgambo wa Hezbollah wanaoungwa mkono na Iran nchini LebanonPicha: Ibrahim Amro/AFP
Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Iran, Esmaeil Baqaei, alisema kuna ujumbe ulipokelewa kutoka “baadhi ya nchi rafiki ulioashiria ombi la Marekani la kutaka mazungumzo yenye lengo la kukomesha vita”, lakini akakanusha kuwa mazungumzo yoyote kama hayo yalifanyika. Lilisema shirika rasmi la Iran IRNA.
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu alisema amezungumza na Trump na kukiri kwamba Marekani inatumai makubaliano yanawezekana, lakini akaapa kuendelea kuishambulia Iran na Lebanon ili kuilinda Israel.
Nchini Lebanon, Israel imepanua operesheni yake ya ardhini dhidi ya wanamgambo wa Hezbollah wanaoungwa mkono na Iran, ikionya kuhusu “wiki kadhaa za mapigano.” Imeshambulia tena kusini mwa BeirutJumatatu na mapema Jumanne na kudai kuwakamata wapiganaji wawili wa Hezbollah.
Lebanon iliingizwa katika vita vya Mashariki ya Kati wakati Hezbollah ilipoanza kurusha makombora dhidi ya Israel mnamo Machi 2 ili kulipiza kisasi mauaji ya kiongozi mkuu wa Iran Ayatollah Ali Khamenei katika shambulio la Israel na Marekani.
AP, AFP, DPA, Reuters
afghanistan, africa, albania, algeria, America, american-samoa, andorra, angola, anguilla, antarctica, antigua-and-barbuda, argentina, armenia, aruba, arusha, australia, austria, azerbaijan, bahamas, bahrain, bangladesh, barbados, belarus, Belgium, belize, benin, bermuda, bhutan, bolivia, bosnia-and-herzegovina, botswana, Boukinafaso, brazil, brunei-darussalam, bulgaria, burkina-faso, burma, burundi, california, cambodia, cameroon, canada, cape-verde, cayman-islands, central-african-republic, Chad, chicago, chile, china, christmas-island, cocos-keeling-islands, colombia, comoros, congo, cook-islands, costa-rica, cote-divoire-ivory-coast, Croatia, cuba, cyprus, czech-republic, darsalaam, democratic-peoples-rep-north-korea, democratic-republic-of-the-congo-kinshasa, denmark, djibouti, dodoma, dominica, dominican-republic, dr-congo, dubai, east-timor-timor-leste, ecuador, egypt, egypty, el-salvador, england, equatorial-guinea, equitorial-guinea, eritrea, estonia, eswatini, ethiopia, falkland-islands, faroe-islands, federal-states-of-moldova, fiji, finland, Florida, france, french-guiana, french-polynesia, french-southern-territories, gabon, gaza, georgia, germany, ghana, gibraltar, goma, Greece, greenland, grenada, guadeloupe, guam, guatemala, guinea, guinea-bissau, guyana, habari, haiti, holy-see, honduras, hong-kong, houston, hungary, iceland, india, indonesia, Iowa, iran, iran-islamic-republic-of, iraq, ireland, israel, italia, italy, ivory-coast, jamaica, japan, jordan, karatu, kazakhstan, kilimanjaro, kinshasa, kiribati, kiswahili, korea, kosovo, kuwait, kyrgyzstan, lao, latvia-lebanon-lesotho-liberia-libya-liechtenstein-lithuania-luxembourg, Lebanon, liberia, macau, madagascar, malawi, malaysia-maldives, Mali, malta, marshall-islands-martinique-mauritania-mauritius, massechutes, mayotte, mazingira, mbeya, meru, mexico, miami, micronesia, monaco-mongolia-montenegro, montserrat, morocco, mozambique-myanmar, mtwara, mwanza, namibia, nauru, nepal, netherlands, netherlands-antilles, nevada, new-caledonia, new-zealand, newyork, nicaragua, niger, nigeria, niue, north-macedonia, northern-mariana-islands, norway, oman, pakistan, palau, palestine, palestinian-territories, panama, papua-new-guinea, paraguay, peoples-democratic-republic, peru, philadhephia, philipians, Philippines, pitcairn-island, poland, politics, Portugal, puerto-rico, qatar, Norrbottens lan, republic-of-brazzaville, republic-of-south-korea, reunion-island, romania, Russia, russian-federation, rwanda, sahara-occidental, saint-kitts-and-nevis, saint-lucia, saint-vincent-and-the-grenadines, samoa, san-marino, sao-tome-and-principe, saudi-arabia, saudiarabia, scotland, Senegal, serbia, seychelles, sierra-leone, Singapore, singida, slovakia-slovak-republic, slovenia, solomon-islands, somalia, southafrica, spain, sri-lanka, sudan, suriname, swaziland-eswatini, sweden, switzerland, syria, syrian-arab-republic, tabora, taiwan-republic-of-china, tajikistan, tanzania, texas, thailand, the-gambia, tibet, timor-leste-east-timor, togo, tokelau, tonga, toronto, trinidad-and-tobago, tunisia, turkey, turkmenistan, turks-and-caicos-islands, tuvalu, uganda, united-arabs-emirates, united-kingdom, united-states, uruguay, uzbekistan, vancover, vanuatu, vatican-city-state-holy-see, venezuela, vietnam, virgin-islands-british, virgin-islands-u-s, wallis-and-futuna-islands
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2026
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.