Zaidi ya wanajihadi wa kiislamu 100 waachiwa huru nchini Mali

Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Na  Cantona Joseph  Imechapishwa: March 23, 2026 9:19 (EAT)

Vocalize Pre-Player Loader

Zaidi ya wanajihadi wa kiislamu 100 wameachiwa huru hivi karibuni na mamlaka za Mali, ikiwa ni sehemu ya makubaliano ya wao kusitisha mashambulio dhidi ya misafara ya malori ya mafuta, mashambulizi ambayo yametatiza upatikanaji wa nishati hiyo kwenye taifa hilo la Afrika Magharibi.

Luteni Kanali Assimi Goita - Rais wa Mali.
Luteni Kanali Assimi Goita – Rais wa Mali. AP

Tangu mwezi Septemba, kundi moja la wanajihadi wa kiislamu wenye uhusiano na mtandao wa kigaidi duniani, Al Qaeda, limekuwa likishambulia misafara ya malori ya mafuta, hali ambayo imefanya shughuli kwenye jiji la Bamako kusimama kutokana na uhaba wa mafuta.

Kwa mujibu wa vyanzo vya ndani vilivyozungumza na shirika la habari la AFP, vilithibitisha kuachiwa kwa wanajihadi zaidi ya 100 kwa kubadilishana na kufunguliwa kwa njia kuu za kibiashara ambazo zimekuwa zikitumiwa na malori kupitisha mafuta kwenda Bamako.

Kwa mujibu wa viongozi wa Bamako, makubaliano haya yatasalia hadi pale sherehe za Eid al Adha maarufu kama Tabaski kwenye ukanda huo, zitakapomalizika mwishoni mwa mwezi Mei.

RDC: Mjadala kuhusu marekebisho ya katiba waendelea kuibua hisia

Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, mjadala wa mabadiliko ya katiba unaendelea, miaka miwili kabla ya uchaguzi mkuu, suala linaloonekana kuwagawa wanasiasa na wananchi wa taifa hilo.

Imechapishwa: 23/03/2026 – 04:38Imehaririwa: 23/03/2026 – 05:22

Dakika 1Wakati wa kusomaCheza – 00:44

Félix Tshisekedi - Rais wa DRC.
Félix Tshisekedi – Rais wa DRC. Getty Images via AFP – ALEX WONG

Hata hivyo, wachambuzi wa siasa wanaona kuwa, mjadala huu sasa unaanza kusababisha kusahaulika kwa masuala muhimu na makubwa yanayoikumba nchi hiyo.

Kwa mujibu wa kituo cha utafiti wa siasa na uongozi cha Ebuteli nchini DRC kwa sababu za kisiasa, kati ya mwaka 2021 hadi 2025, kumekuwa na miswada 458 iliyowasilisha bungeni ni 22 ndio iliyojadiliwa tu.

Aidha, utafiti unaonesha kuwa, chama tawala bungeni kinatumia wingi wake kutanguliza maswala ya kisiasa kama kuendeleza mijadala ya mabadiliko ya katiba, baada ya kujadili masuala muhimu kama ya kiuchumi na changamoto za kiusalama, zinazowatatiza raia wa kawaida nchini DRC.

Hata hivyo, baadhi ya wanasiasa mashuhuri kama Delly Sassanga wanapinga mapendezo ya katiba kufanyiwa marekebisho kutoka kwa wanasiasa wanaomuungano mkono rais Felix Thshisekedi.

Wiki hii pia, Makamu Rais wa Pili wa Seneti Bahati Lukwebo, alijiuzulu kwenye nafasi yake, baada ya kuhusishwa na upinzani wa mabadiliko ya katiba, na kuwepo harakati za kumwondoa kwenye nafasi hiyo na wabunge.

AFCON2025: Kiungo wa Senegal Idrissa Gueye, yuko tayari kurejesha medali yake

Mwishoni mwa juma kiungo wa timuj ya taifa ya Senegal na klabu ya Everton ya Uingereza, Idrissa Gueye, amesema nchi yake ilistahili kutawazwa mabingwa wa kombe la mataifa ya Afrika nchini Morocco, na kwamba yuko tayari kurejesha medali yake ikiwa itasaidia kutuliza joto baina ya mataifa hayo mawili.

Imechapishwa: 23/03/2026 – 05:35

Dakika 1Wakati wa kusoma

Kiungo wa Senegal, Idrissa Gueye, akishangilia katika fainali ya januari 18. tarahe 18 Januari 2026
Kiungo wa Senegal, Idrissa Gueye, akishangilia katika fainali ya januari 18. tarahe 18 Januari 2026 AP – Themba Hadebe

Senegal iliifunga wenyeji Morocco kwa gili 1 kwa 0 katika fainali ya mwezi Januari iliyochezwa mjini Rabat, hatahivyo shirikisho la soka barani Afrika CAF, wiki iliyopita liliiadhibu Senegal kwa kitendo chao cha kutoka uwanjani kwa karibuj dakika 15, shirikisho hilo liiipa Morocco ushindi wa mabao 3 – 0.

Akinukuliwa baada ya mechi ya klabu yake ya Everton dhidi ya Chelsea ambapo ilipata ushindi wa mabao 3 kwa 0, Gueye alisema “binafsi nimejitolea kuzikusanya medali zote nap engine nizikabidhi kwa Morocco kama hii itasaidia kutuliza sintofahamu iliyojitokeza”, alisema Gueye katika mahojiano na kituo cha televisheni cha Canal+

“Inashangaza sana, mechi ya mpira inashindwa uwanjani, hiki ndicho tulikifanya Morocco, tulifanya kile tulipaswa kufanya uwanjani, na tukashinda mechi”. Alisema Gueye.

“Tunastahili kuwa mabingwa wa Afrika. Na sisi ni machampioni hadi sasa. Mataji yanashindwa uwanjani na sio ofisini”. Aliongeza Gueye.

Gueye ambaye aliiongoza nchi yake katika fainali baada ya nahodha aliyezoeleka Kalidou Koulibaly kuwa anatumikia adhabu ya kadi, ameshangazwa na uamuzi wa chama cha soka cha nchi yake kuamua kwenda kukata rufaa kupinga maamuzi ya CAF katika mahakama ya kimataifa ya usuluhishi wa michezo CAS.

“Ingelikuwa ni mimi, ningeliambia shirikisho langu lisikate rufaa”. Alisema Gueye.

Fainali ya CAN ya mwezi Januari ilishuhudia sintofahamu baada ya wachezaji wa Senegal kuamua kutoka uwanjani kupinga wenyeji kupewa penalty yenye utata katika kipindi cha pili cha dakika za lala salama, penalty ambayo kiungo mchambuliajik wa Morocco Brahim Diaz aliikosa, Senegal wakishinda katika mud awa nyongeza kupitia bao la Pape Gueye.

afghanistanafricaalbaniaalgeriaAmericaamerican-samoaandorraangolaanguillaantarcticaantigua-and-barbudaargentinaarmeniaarubaarushaaustraliaaustriaazerbaijanbahamasbahrainbangladeshbarbadosbelarusBelgiumbelizebeninbermudabhutanboliviabosnia-and-herzegovinabotswanaBoukinafasobrazilbrunei-darussalambulgariaburkina-fasoburmaburundicaliforniacambodiacamerooncanadacape-verdecayman-islandscentral-african-republicChadchicagochilechinachristmas-islandcocos-keeling-islandscolombiacomoroscongocook-islandscosta-ricacote-divoire-ivory-coastCroatiacubacyprusczech-republicdarsalaamdemocratic-peoples-rep-north-koreademocratic-republic-of-the-congo-kinshasadenmarkdjiboutidodomadominicadominican-republicdr-congodubaieast-timor-timor-lesteecuadoregyptegyptyel-salvadorenglandequatorial-guineaequitorial-guineaeritreaestoniaeswatiniethiopiafalkland-islandsfaroe-islandsfederal-states-of-moldovafijifinlandFloridafrancefrench-guianafrench-polynesiafrench-southern-territoriesgabongazageorgiagermanyghanagibraltargomaGreecegreenlandgrenadaguadeloupeguamguatemalaguineaguinea-bissauguyanahabarihaitiholy-seehondurashong-konghoustonhungaryicelandindiaindonesiaIowairaniran-islamic-republic-ofiraqirelandisraelitaliaitalyivory-coastjamaicajapanjordankaratukazakhstankilimanjarokinshasakiribatikiswahilikoreakosovokuwaitkyrgyzstanlaolatvia-lebanon-lesotho-liberia-libya-liechtenstein-lithuania-luxembourgLebanonliberiamacaumadagascarmalawimalaysia-maldivesMalimaltamarshall-islands-martinique-mauritania-mauritiusmassechutesmayottemazingirambeyamerumexicomiamimicronesiamonaco-mongolia-montenegromontserratmoroccomozambique-myanmarmtwaramwanzanamibianaurunepalnetherlandsnetherlands-antillesnevadanew-caledonianew-zealandnewyorknicaraguanigernigerianiuenorth-macedonianorthern-mariana-islandsnorwayomanpakistanpalaupalestinepalestinian-territoriespanamapapua-new-guineaparaguaypeoples-democratic-republicperuphiladhephiaphilipiansPhilippinespitcairn-islandpolandpoliticsPortugalpuerto-ricoqatar Norrbottens lanrepublic-of-brazzavillerepublic-of-south-koreareunion-islandromaniaRussiarussian-federationrwandasahara-occidentalsaint-kitts-and-nevissaint-luciasaint-vincent-and-the-grenadinessamoasan-marinosao-tome-and-principesaudi-arabiasaudiarabiascotlandSenegalserbiaseychellessierra-leoneSingaporesingidaslovakia-slovak-republicsloveniasolomon-islandssomaliasouthafricaspainsri-lankasudansurinameswaziland-eswatiniswedenswitzerlandsyriasyrian-arab-republictaborataiwan-republic-of-chinatajikistantanzaniatexasthailandthe-gambiatibettimor-leste-east-timortogotokelautongatorontotrinidad-and-tobagotunisiaturkeyturkmenistanturks-and-caicos-islandstuvaluugandaunited-arabs-emiratesunited-kingdomunited-statesuruguayuzbekistanvancovervanuatuvatican-city-state-holy-seevenezuelavietnamvirgin-islands-britishvirgin-islands-u-swallis-and-futuna-islands

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2026

Follow this blog on Mastodon or the Fediverse to receive updates directly in your feed.

CantonaDigital
CantonaDigital

Listen Live Radio Fortune Africa
Ukweli Na Burudani.

-Be ready to be Impacted, Inspired & Empowered.

-Keep watching our Channels

Cantona Cast Television,

Fortune Television Network (FTN)

Donation
Paypal https://www.paypal.com/donate/?hosted_button_id=6EKXMLNW8W6A2&fbclid=IwY2xjawQxeChleHRuA2FlbQIxMABicmlkETFRdkNBRndpclRDQTB5bXZZc3J0YwZhcHBfaWQQMjIyMDM5MTc4ODIwMDg5MgABHq960uGsyU3ABRIBc2h-iXGhHATvuEqe55gFsQ-rDb0fT-Z7SIQ3TV8LnkpD_aem_ybU2SvBlvyqrVsS9NAczRw

An attitude determines an altitude.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025

5,344 posts
0 followers

Fediverse Followers


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a Reply