Marekani na Iran zatishia kushambulia miundombinu muhimu

Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Na  Cantona Joseph  Imechapishwa: March 23, 2026 9:19 (EAT)

Vocalize Pre-Player Loader

Televisheni ya Iran ilisema shambulizi la Dimona, ambako kuna kinu cha nyuklia, lilikuwa la kulipiza shambulizi la awali kwenye kinu chake cha nyuklia cha Natanz.Picha: John Wessels/AFP

Marekani na Iran zimetishia kushambulia miundombinu muhimu wakati vita katika Mashariki ya Kati, ambavyo vipo katika wiki yake ya nne, vikiyaweka maisha ya watu hatarini kote katika kanda hiyo.

Iran imesema Mlango-Bahari wa Hormuz, ambao ni muhimu kwa usafirishaji wa mafuta na bidhaa nyingine, utafungwa kabisa ikiwa Marekani itatekeleza kitisho cha Rais Donald Trump cha kushambulia mitambo yake ya umeme. Trump alitangaza Jumamosi usiku muda wa mwisho wa saa 48 kwa mlango huo kufunguliwa.

Hayo yalijiri wakati viongozi wa Israel walitembelea moja ya jamii mbili za kusini karibu na eneo la siri la utafiti wa nyuklia lililopigwa na makombora ya IranJumamosi jioni, huku watu wengi wakijeruhiwa. Akizungumza na waandishi wa habari katika eneo lililoshambuliwa la Arad, Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu alisema ni “muujiza” kwamba hakuna mtu aliyeuawa. Amesema Israel na Marekani wanaendelea kumuangamiza adui. “Tumeweka wazi malengo mawili. Moja ni kuvunja kabisa mpango wao wa nyuklia, kuvunja kabisa mpango wao wa makombora, kuvunja kabisa uwezo wao wa kufanikisha miradi hii miwili. Tunakaribia kufanikisha hilo. Pia tumeweka lengo la kutengeneza mazingira kwa watu wa Iran kuupindua udhalimu huu ambao umewatesa na kufanya maisha kuwa magumu, na unafanya maisha kuwa magumu kwa ulimwengu mzima. Na natumai tutafanikisha hilo pia.”

Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu alisema ni “muujiza” kwamba hakuna mtu aliyeuawa katika shambulizi la Iran katika mji wa AradPicha: Avi Ohayon/GPO/Handout/Anadolu/picture alliance

Jeshi la Israel lilisema Jumatatu asubuhi kwamba lilianzisha “wimbi kubwa la mashambulizi yanayolenga miundombinu ya kile lilichoita utawala wa kigaidi wa Iran huko Tehran.”

Milipuko ilisikika kote Tehran mapema leo huku Shirika la habari la Fars lilisema mashambulizi ya anga yalilenga maeneo matano ya mji mkuu wa Iran.

Wakati huohuo, Kuwait, Umoja wa Falme za Kiarabu na Saudi Arabia, zimesema mapema leo kuwa mitambo yao ya ulinzi wa makombora iliyashughulikia mashambulizi ya makombora na droni huku ving’ora vya kutahadharisha kuhusu mashambulizi ya angani vikilia Bahrain.

Uchumi wa dunia uko katika “tishio kubwa” – IEA

Mkuu wa Shirika la Nishati la Kimataifa – IEA Fatih Birol amesema uchumi wa dunia uko chini ya “tishio kubwa” kutokana na mgogoro wa nishati unaosababishwa na vita vya Mashariki ya Kati. Ameonya kwamba “hakuna nchi itakayokwepa” athari zake.

Mkuu wa Shirika la Nishati la Kimataifa – IEA Fatih Birol amesema uchumi wa dunia uko chini ya “tishio kubwa” kutokana na mgogoro wa nishatiPicha: Ludovic Marin/AFP/Getty Images

Akizungumza katika hafla ya Waandishi wa Habari katika mji mkuu wa Australia, Birol aliulinganisha mgogoro wa sasa wa nishati na ule wa miaka ya 1970 na athari za uvamizi wa Urusi dhidi ya Ukraine mwaka wa 2022. Mkuu huyo wa IEA amesema kiasi ya vituo arobaini vya nishati vimeharibiwa kwa kiasi kikubwa katika Mashariki ya Kati kutokana na vita katika eneo hilo. Amesema mambo yalivyo sasa ni kuwa kuna migogoro miwili ya mafuta na mmoja wa gesi, ambayo imeunganishwa pamoja. Birol amesema anatumai kuwa hali hiyo itatuliwa haraka iwezekanavyo akiongeza kuwa IEA inashauriana na serikali za Asia na Ulaya kuhusu kutolewa kwa hifadhi zaidi ya mafuta kama itahitajika. Mataifa wanachama wa IEA walikubaliana Machi 11 kutoa mapipa milioni 400 ya mafuta kutoka kwenye hifadhi za kimkakati ili kupambana na kupanda kwa bei za mafuta ghafi duniani.

Kwingineko mapigano yamepamba moto kusini mwa Lebanon. Kundi la Hezbollah linaloungwa mkono na Iran lilidai kuhusika na shambulio la anga lililomuua mtu mmoja kaskazini mwa Israel.

Siku ya Jumapili, Israel ilipanua orodha yake ya maeneo inayolenga ili kujumuisha madaraja ya Mto Litani ambayo Waziri wa Ulinzi Israel Katz alisema Hezbollah inayatumia kuhamisha wapiganaji na silaha kuelekea kusini. Baadaye Israel iliripua daraja la Qasmiyeh karibu na Tiro, baada ya kutoa onyo la saa moja.

Rais wa Lebanon Joseph Aoun amesema hatua ya Israel kuyalenga madaraja kusini nchi hiyo ni maandalizi ya jeshi kuanzisha uvamizi wa ardhini.

Vyanzo: AFP, AP, Reuters, DPA

afghanistanafricaalbaniaalgeriaAmericaamerican-samoaandorraangolaanguillaantarcticaantigua-and-barbudaargentinaarmeniaarubaarushaaustraliaaustriaazerbaijanbahamasbahrainbangladeshbarbadosbelarusBelgiumbelizebeninbermudabhutanboliviabosnia-and-herzegovinabotswanaBoukinafasobrazilbrunei-darussalambulgariaburkina-fasoburmaburundicaliforniacambodiacamerooncanadacape-verdecayman-islandscentral-african-republicChadchicagochilechinachristmas-islandcocos-keeling-islandscolombiacomoroscongocook-islandscosta-ricacote-divoire-ivory-coastCroatiacubacyprusczech-republicdarsalaamdemocratic-peoples-rep-north-koreademocratic-republic-of-the-congo-kinshasadenmarkdjiboutidodomadominicadominican-republicdr-congodubaieast-timor-timor-lesteecuadoregyptegyptyel-salvadorenglandequatorial-guineaequitorial-guineaeritreaestoniaeswatiniethiopiafalkland-islandsfaroe-islandsfederal-states-of-moldovafijifinlandFloridafrancefrench-guianafrench-polynesiafrench-southern-territoriesgabongazageorgiagermanyghanagibraltargomaGreecegreenlandgrenadaguadeloupeguamguatemalaguineaguinea-bissauguyanahabarihaitiholy-seehondurashong-konghoustonhungaryicelandindiaindonesiaIowairaniran-islamic-republic-ofiraqirelandisraelitaliaitalyivory-coastjamaicajapanjordankaratukazakhstankilimanjarokinshasakiribatikiswahilikoreakosovokuwaitkyrgyzstanlaolatvia-lebanon-lesotho-liberia-libya-liechtenstein-lithuania-luxembourgLebanonliberiamacaumadagascarmalawimalaysia-maldivesMalimaltamarshall-islands-martinique-mauritania-mauritiusmassechutesmayottemazingirambeyamerumexicomiamimicronesiamonaco-mongolia-montenegromontserratmoroccomozambique-myanmarmtwaramwanzanamibianaurunepalnetherlandsnetherlands-antillesnevadanew-caledonianew-zealandnewyorknicaraguanigernigerianiuenorth-macedonianorthern-mariana-islandsnorwayomanpakistanpalaupalestinepalestinian-territoriespanamapapua-new-guineaparaguaypeoples-democratic-republicperuphiladhephiaphilipiansPhilippinespitcairn-islandpolandpoliticsPortugalpuerto-ricoqatar Norrbottens lanrepublic-of-brazzavillerepublic-of-south-koreareunion-islandromaniaRussiarussian-federationrwandasahara-occidentalsaint-kitts-and-nevissaint-luciasaint-vincent-and-the-grenadinessamoasan-marinosao-tome-and-principesaudi-arabiasaudiarabiascotlandSenegalserbiaseychellessierra-leoneSingaporesingidaslovakia-slovak-republicsloveniasolomon-islandssomaliasouthafricaspainsri-lankasudansurinameswaziland-eswatiniswedenswitzerlandsyriasyrian-arab-republictaborataiwan-republic-of-chinatajikistantanzaniatexasthailandthe-gambiatibettimor-leste-east-timortogotokelautongatorontotrinidad-and-tobagotunisiaturkeyturkmenistanturks-and-caicos-islandstuvaluugandaunited-arabs-emiratesunited-kingdomunited-statesuruguayuzbekistanvancovervanuatuvatican-city-state-holy-seevenezuelavietnamvirgin-islands-britishvirgin-islands-u-swallis-and-futuna-islands

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2026

Follow this blog on Mastodon or the Fediverse to receive updates directly in your feed.

CantonaDigital
CantonaDigital

Listen Live Radio Fortune Africa
Ukweli Na Burudani.

-Be ready to be Impacted, Inspired & Empowered.

-Keep watching our Channels

Cantona Cast Television,

Fortune Television Network (FTN)

Donation
Paypal https://www.paypal.com/donate/?hosted_button_id=6EKXMLNW8W6A2&fbclid=IwY2xjawQxeChleHRuA2FlbQIxMABicmlkETFRdkNBRndpclRDQTB5bXZZc3J0YwZhcHBfaWQQMjIyMDM5MTc4ODIwMDg5MgABHq960uGsyU3ABRIBc2h-iXGhHATvuEqe55gFsQ-rDb0fT-Z7SIQ3TV8LnkpD_aem_ybU2SvBlvyqrVsS9NAczRw

An attitude determines an altitude.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025

5,344 posts
0 followers

Fediverse Followers


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a Reply