Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa


Na:Cantona Joseph|RFA
Usichanganye katı ya changamoto unazozipitia kwa sababu UMEKOSEA na zile unazozipotia kwa sababu UNAANDALIWA.
Zile ambazo zimetokana na makosa yako, utahitaji kulipa gharama ya kuzirekebisha au kutafuta mbinu za kuepuka.
Lakini kwa upande mwingine, changamoto ambazo Mungu ameziruhusu ili kukuandaa na kukutengeneza huwa hazikimbiwi.
Yaani, hakutoi kwenye moto Ila atahakikisha moto haukuunguzi. Ndio, gharika itakupata Ila haitakuangamiza.
Uzuri ni kuwa, wengi ambao watakuwa chanzo cha hiyo changamoto wataamini kuwa wanakusababishia mabaya, Ila hawatajua kuwa Mungu anatumia hayohayo wanayokufanyia kukusogeza mbele zaidi.
Kikubwa, Usikate tamaa kuendelea kupambania maono yako. Usiache kukiri Ukuu wako.
Siku Yako Inakuja, watashangaa Kuwa walinia mabaya Ila yametumika kukuinua.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.