Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa


Picha: Ahmed Gomaa/Xinhua/IMAGO
Na:Cantona Joseph|RFA
Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Misaada ya Kiutu, OCHA imesema takribani tani 170,000 za misaada zimeandaliwa na zinasubiri kupelekwa katika Ukanda wa Gaza.
Msemaji wa OCHA, ameyasema hayo Alhamisi baada ya Israel na Hamas kufikia makubaliano ya kusitisha mapigano katika awamu ya kwanza ya mpango wa amani wa Gaza.
Amesema mara tu maafisa wa Israel watakapotoa idhini, misaada hiyo inaweza kupelekwa kwa watu wenye uhitaji.
Amesema misaada hiyo ni pamoja na chakula, dawa, mahema na misaada mingine inayohitajika haraka.
Asilimia 45 ya magari ya misaada imezuiwa
Mapema wiki hii, OCHA ilisema maafisa wa Israel ama hawajaidhinisha au wamezuia asilimia 45 ya magari yake ya misaada yaliyoorodheshwa tangu vita vilipoanza Oktoba, 2023.
Amesema ili kutoa msaada kwa raia, OCHA inahitaji maeneo ya kuvukia ya mipakani yawe wazi, usalama kwa wafanyakazi wa mashirika ya misaada uhakikishwe, na wale wenye uhitahaji waweze kuhama kwa usalama.
Wakati huo huo, Israel imesema usitishaji mapigano utaanza kutekelezwa ndani ya saa 24 baada ya mkutano wa baraza la mawaziri la usalama.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.