Jeshi la Sudan lilitumia silaha za kemikali

Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Vocalize Pre-Player Loader

Sudan yakanusha kutumia silaha za kemikali Picha: John Thys/AFP

Na:Cantona Joseph|RFA

Ripoti za vyombo vya habari zilizotolewa leo, zinaonyesha kuwa jeshi la Sudan lilitumia gesi ya klorini katika mashambulizi mawili mwaka 2024, kaskazini mwa mji mkuu, Khartoum.

Mwezi Juni, Marekani iliweka vikwazo kwa serikali ya Sudan inayoshirikiana na jeshi kutokana na matumizi ya silaha za kemikali, lakini haikufafanua wapi na lini walizitumia.

Uchunguzi uliofanywa na Shirika la habari la France24, umeonyesha kuwa jeshi linaonekana kudondosha mapipa mawili yenye klorini Septemba 2024 karibu na kiwanda cha mafuta cha Al-Jaili kaskazini mwa Khartoum.

Shirika la kimataifa la kutetea haki za binaadamu la Human Rights Watch limesema matumizi ya kemikali ya viwandani kama silaha, yanasababisha hali ya wasiwasi.

Sudan imerudia kukanusha madai ya Marekani, ikiyaita ”yasiyo na msingi” na ”kitisho cha kisiasa”.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a Reply