Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa


Tshisekedi amtaka Kagame kuiamuru M23 kusitisha mapigano Picha: Eduardo Munoz/REUTERS
Na:Cantona Joseph|RFA
Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo Felix Tshisekedi amemtaka Rais wa Rwanda, Paul Kagame kuacha kuwaunga mkono waasi wa M23 nchini Kongo.
Akizungumza Alhamisi mjini Brussels, Ubelgiji, katika Jukwaa la Global Gateway, Tshisekedi amemsihi Kagame washirikiane kwa pamoja katika kuleta amani.
“Ndiyo maana nakuomba kupitia jukwaa hili, na huku ulimwengu mzima ukishuhudia, kukuomba Mheshimiwa Rais, ili tulete amani,” alisisitiza Tshisekedi.
Tshisekedi amesema wito huo unahusisha Kagame kuliamuru Kundi la M23 kusitisha mapigano ambayo tayari yamesababisha vifo vingi.
Kagame hajazungumza wazi
Katika hotuba yake, Rais Kagame hakuuzungumzia moja kwa moja mgogoro huo.
Hata hivyo, alirejelea kwa kifupi kauli ya awali ya Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa aliyesema anahisi “msukumo wa kutaka amani” alipowaona pamoja viongozi wa Rwanda na Kongo.
Hata hivyo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Rwanda, Olivier Nduhungirehe amesema mtu pekee ambaye anaweza kuvimaliza vita vya Kongo ni Rais Tshisekedi.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.