Waziri mkuu wa India ajiandaa kuongoza kwa muhula wa tatu.

Na Cantona Joseph-Juni 06,2024

Modi wa India ajiandaa kuongoza muhula wa tatu
Wachambuzi wanasema, utegemezi wa Modi kwa washirika wa kisiasa inamaanisha anakabiliwa na hali ngumu zaidi katika muhula wake wa tatu.

Waziri Mkuu wa India Narendra Modi anajiandaa kuapishwa kwa ajili ya muhula wa tatu baada ya uchaguzi uliokuwa na ushindani mkali ambao matokeo yake yamekifanya chama chake kuunda serikali ya muungano.

Chama cha Modi cha Bharatiya Janata Party (BJP), ambacho kimekuwa madarakani kwa muongo mmoja kwa kupata ushindi mkubwa, kilikuwa kinatarajia ushindi ma kishindo.

Lakini matokeo ya uchaguzi wa wiki sita yaliyotolewa Jumanne yameonyesha chama cha BJP kikipoteza ushawishi wake na kukifanya kutafuta mshirika wa kuunda nae serikali.

Kundi la muungano lenye wajumbe 15 kutoka National Democratic Alliance (NDA) limetangaza siku ya Jumatano kwamba limekubali kuunda serikali.

“Sote kwa pamoja tumemchangua kiongozi anayeheshimika wa NDA Narendra Modi kuwa kiongozi wetu,” kwa mujibu wa taarifa ya pamoja iliyotolewa na BJP.

Muungano huo una viti 293 bungeni, na kuufanya kuwa na ushawishi mkubwa katika bunge hilo lenye viti 543.

Taarifa ya vyombo vya habari nchini Indian inasema Modi ataapishwa kama waziri mkuu Jumamosi.

Wachambuzi wanasema Modi kutegemea muungano inamaanisha atakabiliwa na muhula wa tatu wenye changamoto.

“Itamlazimu Modi kuchukua maoni ya wengine — tutaona demokrasia zaidi na bunge lenye afya,” amesema Nilanjan Mukhopadhyay, ambae ameandiika kitabu kuhusu maisha ya Modi.

“Atahitajika kuwa kiongozi ambae hakuwahi kuwa nae, tutamuona Modi mpya.”

Afrika Leo Jioni:Radio Fortune Africa


Modi India
Uchaguzi India
Waziri Mkuu India
Modi Kuunda Serikali Ya Muungano
Kazi Ngumu Ya Narendra Modi
Habari zinazohusia Vijana waliochoshwa na vita DRC wapata faraja mchezo wa kuteleza Vijana waliochoshwa na vita DRC wapata faraja mchezo wa kuteleza
Huku kukiwa na operesheni za kijeshi zinazoendelea nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo za kung’oa makundi ya waasi, kijana mmoja anatoa suluhu la kipekee ili kupunguza msongo wa mawazo na kukabiliana na uhalifu mijini
Ukame wapelekea changamoto ya kiafya nchini Somalia
Ukame wapelekea changamoto ya kiafya nchini Somalia
Ukame Afrika Mashariki
Kenya yatangaza ubinafsishaji wa makampuni yake ya serikali

All Rights Reserved|©Cantona Group Ltd


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a Reply