Radio Fortune Africa
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Baadhi ya wachezaji kwenye kikosi cha Sudan Kusini wanaishi katika nchi za Marekani, Australia, Canada, huku wengi wao wakiwa ni watu ambao walianza maisha katika kambi za wakimbizi.
Wanamichezo hawa hawana ufahamu zaidi kuhusu nchi yao kwani, wazazi wao walikimbia wakati wa mzozo wa Sudan wa mwaka 1983-2005, moja ya vita vya kiraia vilivyodumu muda mrefu zaidi kwenye rekodi, ambayo hatimaye ilileta uhuru wa Sudan Kusini mnamo mwaka wa 2011.
Wachezaji hao wanasema wako tayari kuisaidia nchi yao changa kuandikisha historia kaitka mashindano hayo.

Miaka miwili tu baada ya kujipatia uhuru kutoka kwa Sudan, Nchi hiyo iliingia katika vita vya wenyewe kwa wenyewe kuanzia mwaka 2013 hadi 2018, vita ambavyo vilisababisha vifo vya zaidi ya watu 400,000 na kuwasababisha mamilioni ya watu kuhama makaazi yao.
Sudan kusini yenye idadi ya takribani watu milioni 11 inakabiliwa na matatizo ya kisiasa, kikabila, umaskini, ufisadi, pamoja na majanga kama vile mafuriko na ukame.
Kuany Kuany, nahodha wa timu hiyo akizungumza na shirika la habari la AFP huko Kigali, amesisitiza kwamba wanaenda kushiriki mashindano hayo kwa ajili ya nchi yao ilikuleta furaha kwa raia wanaowategemea.

Gabriel, mwenye umri wa miaka 27 na ambaye amecheza pamoja na nyota
Timu hiyo ilijipatia umaarufu wa kimataifa waliposhiriki kwa mara ya kwanza katika Kombe la Dunia la Mpira wa Kikapu mnamo mwezi Agosti mwaka jana, na kusababisha furaha kubwa nyumbani.
Katika mechi ya mazoezi ya mwishoni mwa juma lililopita mjini London, walikaribia kupata ushindi mkubwa dhidi ya timu ya Marekani yenye nguvu hata hivyo, walipoteza kwa pointi moja tu (101-100).
Wahamiaji wa Sudan Kusini wanatarajiwa kujitokeza kwa wingi mjini Paris kuunga mkono timu yao ambayo inatarajiwa kupambana dhidi ya Marekani, Serbia, na Puerto Rico katika kundi lililo na changamoto kubwa.
Na Cantona Joseph
Soma zaidi mada inayofanana:

Olimpiki 2024: Sudan Kusini inalenga kuandikisha matokeo bora jijini Paris

PARIS OLIMPIKI 2024
Daniel Mateiko analenga kumaliza ukame wa dhahabu ya Olimpiki, 10,000m kwa Kenya
Michezo ya Olimpiki inafunguliwa jijini Paris nchini Ufaransa, Ijumaa jioni

Saudi Arabia: Moussa Diaby amejiunga na klabu ya Al-Ittihad

Michezo ya Olimpiki, inaanza siku ya Ijumaa jijini Paris nchini Ufaransa

PARIS OLIMPIKI 2024
Mary Moraa akumbuka maisha magumu aliyopitia akilenga medali ya Olimpiki
Rais Macron kuunga mkono ugombea wa Ufaransa kwa Michezo ya Olimpiki ya Majira ya baridi ya 2030

Muingereza, Andy Murray atangaza kustaafu tenesi baada ya Olimpiki ya Paris
PARIS OLIMPIKI
Ndoto ya Wiseman Were kushiriki Olimpiki yatimia licha ya kuvunjwa moyo na watu
PARIS OLIMPIKI
Omanyala afanyia kazi mita 50 za mwisho akilenga medali ya Olimpiki ya Paris

PARIS OLIMPIKI 2024
“Youtube Man” Julius Yego afurahia kushiriki Olimpiki yake ya nne jijini Paris

All Rights Reserved © Cantona Group Ltd||2024
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.