Mungu ana mipango mikubwa na mwanadamu.

Shetani alimkosanisha mwanadamu na Mungu alijua Mungu yuko tayari kufanya mambo makubwa juu ya mtu ampendaye,yuko tayari kumpa chochote atakacho omba.shetani alimwambia Eva utawala wa Mungu sio mzuri kuna mambo amewaficha msijue na ni mazuri hapo mlipo bustanini ni kama mpo kifungoni amewazuia kujua na kuona mambo mazuri zaidi,Eva na Adamu walikubaliana na shetani na kuamua kujaribu maisha mbali na utawala wa Mungu.Sio kwamba Mungu alishindwa kupinga na sio kwamba Mungu alishindwa kumuadhibu shetani kwa kitendo alicho fanya kwa ufupi tu ni kwamba Mungu alimuumba mwanadamu aliyempenda na kumuamini kwenye bustani ya Edeni na alimuumba kwa mfano wake aliamini mwanandamu huyo anaweza kushinda kila vishawishi.Kuanzia leo anza kujiamini maana Mungu anakuamini unaweza shindana na adui yako,unaweza kumiliki chochote unaweza kufanya haki mbele za watu wengine,unaweza kudumisha upendo kama Mungu mwenyewe alivyo.Yehova anakuamini simama na ujitie nguvu.
Iposiku #Getinspired #CantonaJosephMotivates All rights reserved©2019


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment