Jenga misuli ya upambanaji!!!

https://youtu.be/69iBkNmDzus?si=MmFPjY2YTKSpGSrm
Leo tuzungumze kuhusu namna ya kuvuka nyakati ngumu. Kwenye maisha kuna wakati, matatizo unapambana nayo na yanaisha. Ila kuna wakati hayo matatizo hayatoki kwa haraka. Unapitia matatizo kwa muda mrefu.

Kuna wakati ukimuomba Mungu akutoe kwenye moto, atakutoa. Ila kuna wakati utamuomba Mungu akutoe, atakutengenezea kuendelea kuwa kwenye moto, ila hautaungua.
Kuna wakati, mtu anakuwa katika hali ya ugonjwa kwa muda mrefu, au hali ya kukosa fedha kwa muda mrefu, au kukosa kazi muda mrefu.

Wakati huu, kuna watu wanaacha kabisa kutenda mema, au wengine wanamkufuru kabisa Mungu.

Kuna wakati, matatizo yanaondoka kwa haraka, na inakuwaje wakati mwingine changamoto huwa haziondoki mapema. Kuna sababu kwa nini haya yanatokea.

(i) Kuna mambo yanatokea ili kupata ukomavu.

Kuna uvumilivu unatakiwa kuwa nao, ambao huwezi kuupata bila kupitia hali fulani. kuna vitu inabidi ukutane navyo, ili vikujengee misuli, vikujenge uimara.

Kuna mambo ambayo utayakuta huko mbele zaidi, ambavyo ile hali uliyopitia itakuwa base ya wewe kusonga mbele.

Hata mfalme Daudi, alipata ukomavu wakati analinda mifugo ya baba yake, kiasi ambacho ilimpa hari ya kupambana na Daudi na akamshinda.

(ii) Kukufundisha kusimama peke yako.

Nyakati nyingi kwenye maisha, huwa tunapenda watu watukimbilie ili kutupa msaada. Ila kuna wakati Mungu anaacha hiyo hali itokee ili ujifunze kumtegenea yeye. kuna wakati, marafiki zako ullikuwa ukiwa na shida wanakusaidia haraka, ila kwa sasa hawafanyi hivyo.

Siyo kama hawakupendi ila ni hali unayopitia ili ujue kuna wakati inabidi utembee peke yako, ukiwa unamtegemea Mungu. Na haimaanishi kuwa hauna thamani.

Kuna wakati Mungu anazuia watu kukusaidia sababu, wakikusaidia huko mbeleni watakuja kuutumia ule msaada vibaya.

Naendelea kujifunza: Tujifunze Pamoja


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment