Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Na : Cantona Joseph|RFA

Katibu wa Baraza la Usalama la Urusi, Sergei Shoigu, ameongoza ujumbe mkubwa wa nchi yake kuelekea Misri kwa majadiliano muhimu ya ulinzi, usalama na ujasusi.Picha: Mikhail Klimentyev/Russian President Press Office/dpa/picture alliance
Katibu wa Baraza la Usalama la Urusi, Sergei Shoigu, amewasili nchini Misri akiongoza ujumbe mkubwa wa maafisa wa kijeshi na wataalamu wa silaha za nyuklia kwa ajili ya mazungumzo na serikali mjini Cairo.
Shoigu aliyewasili siku ya Jumapili (Novemba 10) alitarajiwa kukutana na Rais Abdel Fattal al-Sisi, mshauri mkuu wa usalama wa Misri, mawaziri wa nje na ulinzi, na pia maafisa wengine wa ngazi za juu wa ulinzi na ujasusi.
Shirika la habari la Urusi, RIA, liliinukuu taarifa kutoka Baraza la Usalama la nchi hiyo ikisema kwamba pande hizo mbili zingelijadiliana utekelezaji wa makubaliano yaliyokwishafikiwa katika ngazi za juu, ukiwemo ushirikiano wa kiufundi kwenye masuala ya kijeshi.
Shoigu, mshirika wa muda mrefu wa Rais Vladimir Putin wa Urusi na waziri wake wa zamani wa ulinzi, anaendelea kuwa mtu mwenye nguvu sana kwenye mfumo wa kijeshi wa Kremlin.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.