Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Na : Cantona Joseph|RFA

Rais Donald Trump wa Marekani.Picha: Jonathan Ernst/REUTERS
Maseneta nchini Marekani wamefikia makubaliano ya kurejesha ufadhili kwa serikali kuu na kukomesha hatua ya ufungwaji wa shughuli ulioingia siku yake ya 40 na kulazimisha operesheni nyingi za serikali kusimamishwa.
Vyombo vya habari nchini Marekani, vikiwemo vituo vya CNN na Fox News, viliripoti kwamba watunga sheria hao wameafikiana kuruhusu ufadhili kwa serikali kuu hadi mwezi Januari baada ya kubishana sana juu ya ruzuku kwenye huduma za afya, mafao ya chakula na hatua ya Rais Donald Trump kuwafuta kazi wafanyakazi kadhaa wa serikali kuu.
Makubaliano hayo yalitazamiwa kupigiwa kura na Bazara la Seneti usiku wa Jumapili.
Hata hivyo, makubaliano hayo yamefikiwa baada ya hasara kubwa sana, hasa kwenye sekta ya usafirishaji, ambapo zaidi ya safari 7,000 zilicheleweshwa siku ya Jumapili (Novemba 9), huku zaidi ya 1,000 zikifutwa siku ya Ijumaa, na zaidi ya 1,500 siku ya Jumamosi.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.