Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Na : Cantona Joseph|RFA

Mkuu wa Sera za Nje wa Umoja wa Ulaya, Kaja Kallas.Picha: Nicolas Landemard/Le Pictorium Agency/ZUMA/picture alliance
Viongozi wa Amerika ya Kusini na Ulaya wanatarajiwa kufikia makubaliano ya kuanzisha ushirikiano wa kupambana na ulanguzi wa madawa ya kulevya, uhalifu wa kupangwa na ufisadi.
Mkutano huo uliofanyika kwenye mji wa pwani ya Kolombia, Santa Maria, kati ya Umoja wa Ulaya na Jumuiya ya Mataifa ya Amerika Kusini na Karibi, ulidhamiria kuanzisha uratibu wa pamoja kati ya mamlaka za polisi, mahakama, na forodha za pande hizo.
Mkuu wa sera za nje wa Umoja wa Ulaya, Kaja Kallas, alisema ushirikiano wao utafanya mengi zaidi ya kuwalinda raia, ambapo mpango wa Umoja wa Ulaya kulinda njia za baharini utatanuliwa kuwezesha upashanaji habari na uchukuwaji hatua za pamoja dhidi ya uhalifu baharini.
Miongoni mwa waliohudhuria mkutano huo ni Rais Lula da Silva wa Brazil, Rais wa Baraza la Ulasa, Antonio Costa na Waziri Mkuu wa Uhispania, Pedro Sanchez.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.