Rais wa zamani asiye na mamlaka Korea Kaskazini afariki.

Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Vocalize Pre-Player Loader

Na: Cantona Joseph|RFA

Picha: KCNA/AFP

Mtu wa pekee nje ya familia ya Kim kuhudumu kama rais asiye na mamlaka nchini Korea Kaskazini, Kim Yong Nam, amefariki dunia.

Haya ni kulingana na shirika la habari la kitaifa la Korea Kaskazini, KCNA, lililotoa tangazo hilo leo.

Kim Yong Nam ambaye alihudumu chini ya viongozi wote watatu wa nchi hiyo, amefariki dunia jana akiwa na umri wa miaka 97.

Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un ametoa heshima zake kwa kiongozi huyo mapema leo.

Nam alihudumu katika wadhfa huo kuanzia mwaka 1998 na akastaafu mwaka 2019 na ndiye aliyekuwa kama sura ya diplomasia ya Korea Kaskazini.

Nam alizaliwa 1928 na alihudumu katika wizara muhimu ya mambo ya kigeni na alikuwa na mchango mkubwa katika diplomasia ya nchi hiyo chini ya mwanzilishi wa taifa Kim II Sung.

Chini ya Kim Jong Un aliendelea kuwa sura ya diplomasia ya nchi hiyo akiwa na jukumu la kuwakaribisha viongozi wa ngazi ya juu nchini humo.

Mwaka 2018 aliongoza ujumbe wa wanamichezo wa Korea Kaskazini kuelekea Korea Kusini kwa michezo wa Olimpiki ya majira ya baridi ambapo alifanya mazungumzo na Rais wa wakati huo wa Korea Kusini, Moon Jae-in.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment