Ethiopia yaituhumu Eritrea kwa kujiandaa kwa vita

Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Na:Cantona Joseph|RFA

Ethiopia imeituhumu Eritrea kwa kuungana na kundi moja la upinzani lenye misimamo mikali katika kujiandaa kuanzisha vita.

Haya ni kwa mujibu wa barua kutoka kwa wizara ya mambo ya kigeni ya nchi hiyo iliyoonekana na Shirika la Habari la Ufaransa AFP.

Waziri wa mambo ya kigeni wa Ethiopia amemwandikia Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres, akimueleza kuwa ushirikiano kati ya serikali ya Eritrea na chama cha TPLF ambacho kimepigwa marufuku ya kushiriki siasa kwa miaka 30, umekuwa wazi katika miezi michache iliyopita na kwamba wanapanga kuanzisha vita dhidi ya Ethiopia.

Ethiopia vile vile inaituhumu Eritrea na TPLF kwa kufadhili, kuhamasisha na kuyaelekeza makundi yenye silaha katika eneo la Amhara, ambako jeshi la Ethiopia limekuwa likikabiliana na waasi kwa miaka kadhaa. Kwa miezi kadhaa sasa, mahusiano kati ya majirani hao wawili Ethiopia na Eritrea yamevurugika.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment