Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Liverpool haina nia ya kumuuza Federico Chiesa licha ya kumuacha nje ya kikosi chake cha Ligi ya Mabingwa. Klabu ya Besiktas ya Uturuki ilikuwa imeonyesha nia ya kutaka kumsajili mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 27. (Liverpool Echo)
Kipa wa Ujerumani Stefan Ortega, 32, sasa anaweza kusalia Manchester City angalau hadi Januari baada ya Trabzonspor, klabu ya Uturuki ambayo alikuwa ikimfuatilia, kuamua kumsajili mchezaji wa kimataifa wa Cameroon Andre Onana mwenye umri wa miaka 29 wa Manchester United badala yake. (Manchester, Evening News)
Arsenal wako mstari wa mbele kumsajili kiungo wa Stuttgart Angelo Stiller baada ya ofa ya dakika za mwisho kutoka kwa Manchester United kukataliwa katika msimu wa kiangazi, lakini Bayern Munich na Real Madrid pia wanavutiwa na mchezaji huyo wa kimataifa wa Ujerumani, 24. (Express)
Tottenham walifanya uamuzi wa dakika za mwisho wa kumsajili Senny Mayulu wa Paris St-Germain, 19, kabla ya dirisha la uhamisho kufungwa huku Chelsea na Manchester City pia wakimtaka kiungo huyo wa kati. (Team talk)
Real Madrid inajiandaa kumsajili mlinzi wa Ufaransa Dayot Upamecano, 26, ambaye yuko katika mwaka wa mwisho wa mkataba wake na klabu ya Bayern Munich ya Ujerumani. (Bild – kwa Kijerumani)
Wolverhampton Wanderers inaamini hakuna masualayoyote yatakayoibuka katika mazungumzo ya kandarasi mpya na Jorgen Strand Larsen, 25, lakini itajumuisha kipengele cha chini cha kuachiliwa kwa mshambuliaji huyo wa Norway baada ya kukataa ofa mbili za zaidi ya pauni milioni 50 kutoka Newcastle msimu wa kiangazi. (Telegraph – usajili unahitajika)
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.