Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

i. Epuka msongo wa mawazo unaoweza kuepukika.
ii. Badilisha vitu au hali zinazokusababisha msongo wa mawazo.
iii. Amua kuendana na mazingira.
iv. Kubaliana na hali halisi.
Katika Makala Hii Tutazungumzia Mbinu Ya Nne
– Kubaliana na hali halisi.
Fikiri kwa mfano umepoteza mtu wako wa karibu uliyekuwa unampenda sana, hawezi kurudi tena hata ungeumia kiasi gani, hata ungelia kwa muda mrefu kiasi gani.
Namna nzuri ya kukabilana na hali hiyo na kukubaliana na ukweli, kumshukuru Mungu kwa muda ambao ulikuwa naye na kisha kufungua ukurasa mpya.
Wewe ulikuwa na mpenzi wako unayempenda halafu unakuja kujua tayari ameshafunga ndoa na mtu mwingine.
Huwezi kubadilisha chochote, cha zaidi ni kukubaliana na hali halisi na kuanza maisha mengine.
Wako wengi wanaosubiri kupendwa, wapo wengi pamoja na kuumizwa bado wana upendo wa dhati usihitimishe kama wote wanakulaghai kama alivyofanya yeye.
Kwa kufanya hivyo utakuwa unajifunga kwenye gereza la msongo wa mawazo.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.