Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

“Cantona, huwezi kufikia kiwango cha kufanya kwa UBORA unaoutaka kama unaogopa KUKOSEA, KUCHEKWA na KUKOSOLEWA”
Huu ni moja ya ushauri bora sana niliowahi kupewa na mentor wangu hapo zamani.
Changamoto mojawapo iliyokuwa inanikabili ni kutaka kuwa MKAMILIFU kwa mara ya kwanza ninapoanza kitu.
Hii sio shauku mbaya, ni nzuri sana ila ukweli ni kuwa unapoanza lazima kuna makosa utayafanya, uwe tayari kwa hilo.
Hivyo usiweke jicho lako katika KUEPUKA kukosea utakapoamua kufanya, weka jicho lako katika kuwa bora kila UTAKAPOPATA nafasi ya kufanya.
Kuna watu wengi sana wamekata tamaa kwa sababu walipofanya mara ya kwanza haikuwa vizuri kama WALIVYOTARAJIA.
Kuna watu watakucheka unapoanza, kuna watu watakosoa sana unapoanza, kuna watu watakunyooshea vidole, utakose ana kufeli mara kadhaa n.k
Kikubwa ni kujua kuwa, uko darasani unajifunza.
Badala ya KUSUSA na KUACHA, dhamiria kuwa bora kwa kila fursa MPYA unayopata.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.