Chad yasema tarehe ya mwisho ya kuondoka wanajeshi wa Ufaransa ‘haiwezi kujadiliwa’

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

f
Maelezo ya picha,Waziri Mkuu wa Chad, Allamaye Halina

Waziri Mkuu wa Chad, Allamaye Halina, amesema Ufaransa lazima ikamilishe kuwaondoa wanajeshi wake kutoka nchi hiyo ya Afrika ya Kati ifikapo Januari 31 kufuatia matamshi ya kutatanisha yaliyotolewa na Rais wa Ufaransa, imeripoti tovuti binafsi ya Alwihda.

Halina amesema tarehe ya mwisho ya kuondoka kwa vikosi vya Ufaransa “haiwezi kujadiliwa na lazima iheshimiwe bila masharti.”

Halina aliwataka wajumbe wa kamati inayosimamia uondokaji huo kumpatia taarifa ya kina kuhusu mpango huo na kuhakikisha uondokaji wao unaharakishwa kwa mujibu wa ratiba iliyokubaliwa.

Ufaransa ilianza kuliondoa jeshi lake kutoka Chad tarehe 10 Disemba, kufuatia kusitishwa kwa makubaliano ya ushirikiano wa kiulinzi tarehe 28 Novemba.

Matamshi ya Halina yamekuja baada ya Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron kusema tarehe 6 Januari kwamba Paris bado inasubiri maneno ya shukrani kutoka kwa nchi za Kiafrika, ilizozisaidia kupambana na makundi ya wanamgambo.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment