Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Mwandishi wa habari wa Italia aliyezuiliwa nchini Iran mwezi uliopita ameachiliwa na yuko kwenye ndege kurejea Roma, serikali ya Italia imesema.
Cecilia Sala, 29, alikamatwa tarehe 19 Disemba, siku tatu baada ya mhandisi wa Iran kuzuiliwa na Italia mjini Milan kwa tuhuma za kusambaza teknolojia ya ndege zisizo na rubani ambazo zilisababisha vifo vya wanajeshi wa Marekani.
Ripoti zinasema Sala alikuwa amezuiliwa katika gereza maarufu la Evin la Tehran.
Haijulikani ni nini kimesababisha kuachiliwa kwa Sala, hata hivyo habari kutoka kwa maafisa wa Waziri Mkuu Giorgia Meloni zinasema “kazi kubwa kupitia njia za kidiplomasia na kijasusi ilifanyika.”
Meloni amewashukuru “wote waliochangia kufanikisha kurudi kwa Cecilia.” Yeye binafsi aliwapa habari wazazi wa Sala kuhusu kuachiliwa kwake.
Iran ilisema hapo awali kuwa ilimzuilia Sala kwa “kukiuka sheria za Jamhuri ya Kiislamu,” hata hivyo maafisa wa idara ya mambo ya nje ya Marekani wanaamini alizuiwa baada ya kukamatwa kwa raia wa Iran Mohammad Abedini katika uwanja wa ndege wa Malpensa mjini Milan tarehe 16 Disemba.
Alikamatwa kwa waranti ya Marekani na afisa mmoja aliviambia vyombo vya habari vya Italia kwamba Sala alikuwa akitumiwa kama “mtaji wa kisiasa”.
Mohammad Abedini anatazamiwa kufikishwa mbele ya mahakama ya Milan tarehe 15 Januari.
Mkuu wa idara ya ujasusi ya Italia, Giovanni Caravelli, inasemekana alisafiri hadi Tehran yeye mwenyewe ili kumrejesha Sala nchini Italia.
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.