Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Mtoto mwenye umri wa miaka 8 aliyetoweka nyumbani kwao katika kijiji cha Kariba hatimaye alipatikana akiwa salama na askari wa wanyamapori baada ya kuzurura peke yake kwa siku tano katika mbuga ya wanyamapori ya Matusadonha iliyoko Mashonaland Magharibi nchini Zimbabwe, umeripoti wavuti wa mtandaoni ZimLive.com
Tinotenda Pudu alitoweka, akapoteza mwelekeo na bila kujua pa kuelekea katika Mbuga ya wanyama ya Matusadonha, kulingana na Mbunge wa Uwakilishi wa jimbo la Mashonaland Magharibi, Mutsa Murombedzi ambaye alinasa kwa ufupi tukio hilo kwenye mtandao wa kijamii kwenye mtandao wake wa X.
“Muujiza wa kweli katika jamii ya kijijini ya Kasvisva, Nyaminyami katika maeneo ya mashambani ya Kariba, jamii ambapo unaweza unaweza kuingia katika mbuga ya wanyama kwa urahisi kimakosa. Tinotenda Pudu mwenye umri wa miaka 8 alizurura, akapoteza mwelekeo na bila kujua akaelekea katika mbuga ya wanyama ya Matusadonha,” alisema.
“Baada ya siku 5 za kutisha katika msitu uliopo karibu na Mto Hogwe, unaoingia Mto Ume, mvulana huyo amepatikana akiwa hai na walinzi wa ajabu kutoka Mbuga za Matusadona Africa.
“Alikabiliwa na mateso ya kutembea umbali wa kilomita 23 kutoka nyumbani, kulala juu ya miamba ya mawe, kati ya simba wanaonguruma, tembo wanaopita, kula matunda ya mwituni na pori la kutisha ni mateso makubwasana kwa mtoto wa miaka 8.
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.