Afrika Leo Jioni -Oktoba 9,2024

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Karibu katika Matangazo yetu ya jioni moja kwa moja kutoka Communication Center. Tumekuandalia mengi ikiwa ni pamoja

Muhtasari

  • Maseneta Kenya waaswa kutokuwa na upendeleo katika kuamua suala la Gachagua
  • Wanne mbaroni Tanzania kwa kumuua mume wa mdaiwa mkopo
  • Erdogan aiita Israel “shirika la kigaidi la Kiyahudi”
  • Mapigano yaendelea Gaza, idadi ya waliouawa yafikia 42,000
  • Israel yasema imeshambulia maeneo 185 ya Hezbollah katika saa 24 zilizopita
  • Bunge la Seneti Kenya kusikiliza mashtaka dhidi ya Naibu wa rais Gachagua leo
  • Hezbollah inasema iliwarudisha nyuma wanajeshi wa Israel kwenye mpaka
  • Msumbiji yafanya uchaguzi huku chama tawala kikitarajiwa kudumisha uongozi
  • Brazil yaondoa marufuku dhidi ya X baada ya kampuni hiyo kulipa faini ya dollar milioni 5
  • Raia wa Afghanistan akamatwa kwa madai ya njama ya shambulizi siku ya uchaguzi wa Marekani
  • Urusi inadhamiria kusababisha ghasia katika maeneo ya Uingereza, inaonya MI5
  • Jimbo la Florida Marekani lajitayarisha kukabiliana na kimbunga Milton

Naam,Natumai U buheri wa afya popote pale ulipo duniani kwa mwoyo mkunjufu na mikono miwili Hujambo na karibu katika matangazo yetu Afrika Leo Jioni moja kwa moja ikiwa ni tarehe 09/10/2024  Jina langu ni Cantona Joseph,karibu.

Jinsi ya kuchaji simu yako ikiwa hakuna umeme

.

5 Julai 2024

Wakati wa majanga kama vile dhoruba, mafuriko na matetemeko ya ardhi, matatizo mengi hutokea kutokana na kukatika kwa umeme.

Katika hali kama hiyo, ikiwa simu haina chaji, ni kama kukata uhusiano na ulimwengu.

Hata tunapokwenda maeneo ya mbali ya milimani, ambako umeme haupatikani, mara nyingi tunakabiliwa na tatizo la kukosa kuchaji simu zetu.

Lakini hata kama huna kifaa cha kuhifadhia chaji (power bank), unaweza kuchaji simu yako ya mkononi kwa urahisi katika hali ya dharura kama hiyo.

Nini kinahitajika?

Mambo machache yanahitajika ili kuchaji simu ya mkononi wakati hakuna umeme:

  • Waya wa kuchaji simu (USB) na soketi ya gari ya kuchaji
  • Kebo inayotumika kuchaji simu
  • Betri ya volteji 9
  • Kalamu au ufunguo.

Tunachopaswa kufanya ni kupeleka umeme kutoka kwenye betri hadi kwenye simu ya mkononi.

Umeme hutumwa kutoka katika betri hadi kwenye kwa kutumia kiunganishi cha umeme. Hapa ufunguo ndio utakuwa kiunganishi chetu.

Molekyuli za umeme zilizochajiwa hutumwa kutoka kwenye betri hadi kwa simu ya rununu kupitia kifaa kinachowezesha umeme kupitia kati yake.

Hapa klipu ya chuma hutumika kama kifaa hicho kinachowezesha umeme kupitia katikati yake.

Angalau nishati ya kutosha inapatikana ili kupiga simu za dharura na kutuma ujumbe.

Hata hivyo, tujifunze kufanya hivyo katika hatua tatu.

Wanne mbaroni Tanzania kwa kumuua mume wa mdaiwa mkopo

oya

Jeshi la polisi nchini Tanzania linawashikilia wafanyakazi wanne wa kampuni ya kutoa ya mikopo ya kifedha ya OYA kwa tuhuma za mauaji ya Juma Mfaume kwa kumshambulia sehemu mbalimbali za mwili mume wa mdaiwa wa mkopo.

Taarifa ya Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Pwani, Muhudhwari Msuya inasema tukio hilo limetokea Jumatatu katika wilaya ya kipolisi Mlandizi ambapo wafanyakazi hao walifika nyumbani hapo kwa lengo la kudai fedha za marejesho ya mkopo kwa mke wa Mfaume.

Kwa mujibu wa polisi, baada ya kufika nyumbani kwa Mfaume aliwaelekeza kuwa mkewe hakuwepo lakini watuhumiwa hao walilazimisha kuingia ndani kwa nguvu huku wakimshambulia kwa kumchapa na fimbo sehemu mbalimbali za mwili wake na kupelekea kuanguka chini na kupoteza fahamu.

Kamanda Msuya alisema kutokana na hali hiyo watuhumiwa walimbeba Mfaume kwenye gari lao kwaajili ya kumpeleka hospitali lakini alifariki akiwa anapewa matibabu.

Alisema, “Mwili wa marehemu umefanyiwa uchunguzi na daktari kisha kukabidhiwa ndugu kwa taratibu za mazishi.”

Hata hivyo, Jeshi la Polisi linatoa wito kwa makampuni na taasisi za kifedha kufuata taratibu za kisheria katika kudai fedha kutoka kwa wateja wao ili kuepusha usumbufu na madhara yanayoweza kutoka ikiwemo uharibifu wa Mali, kujeruhi na vifo.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Kampuni ya OYA ya nchini Tanzania, Alpha Peter ameiambia BBC kuwa waliodaiwa kusababisha kifo ni watumishi wa taasisi yao na kwamba kitendo hicho hakikuwa maelekezo ya kampuni hiyo.

Peter alisema, “Kilichofanyika, si maelekezo wala utaratibu wa taasisi yetu pale tunapoenda kudai marejesho kwa wateja wetu. Kwasasa tuko karibu na familia kuifariji lakini pia tunaendelea kutoa ushirikiano kwa jeshi la Polisi wakati huu wakiendelea na uchunguzi wa tukio hilo.”

Kampuni ya OYA ya nchini Tanzania ilisajiliwa mwaka 2020 na kwasasa inatoa huduma kwenye mikoa nane

Erdogan aiita Israel “shirika la kigaidi la Kiyahudi”

Erdogan

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdoğan katika ukosoaji wake wa mashambulizi ya Israel dhidi ya Lebanon na Gaza ameitaja nchi hii kuwa ni “shirika la kigaidi la Kiyahudi”.

Bwana Erdoğan ambaye alikuwa akizungumza mbele ya wabunge wa chama tawala cha Justice and Development, kwa mara nyingine tena alikosoa madola ya Magharibi hasa Marekani kwa kuiunga mkono Israel.

Rais wa Uturuki pia alionya kwamba mzozo kati ya Iran na Israel umeongeza hatari ya vita vya kikanda.

Bwana Erdogan, ambaye ana historia ndefu ya ukosoaji mkali wa Israel, hapo awali alimwita Benjamin Netanyahu “mchinjaji wa Gaza” na kumlinganisha yeye na serikali yake na Hitler na serikali ya Ujerumani ya Nazi.

Mapigano yaendelea Gaza, idadi ya waliouawa yafikia 42,000

Waombolezaji wakimfariji mvulana huko Deir al-Balah, katikati mwa Gaza

Tumekuwa tukiangazia Lebanon asubuhi ya leo, lakini mapigano yanaendelea huko Gaza, ikiwa ni pamoja na Jabalia kaskazini, ambapo vifaru vya Israel na wanajeshi wanafanya operesheni ya ardhini.

Katika taarifa yake asubuhi ya leo, jeshi la Israel limesema lilishambulia maeneo 45 ya Hamas huko Gaza katika muda wa saa 24 zilizopita, ikiwa ni pamoja na kambi za Hamas, kurusha roketi na maeneo ya kuhifadhi silaha.

Wizara ya afya inayosimamiwa na Hamas huko Gaza imesema zaidi ya Wapalestina 42,010 wameuawa katika mashambulizi ya kijeshi ya Israel tangu yalipoanza mwaka mmoja uliopita.

Hilo ni ongezeko la 45 kwa jumla ya siku iliyotangulia. Wizara haitofautishi kati ya vifo vya wapiganaji kutoka Hamas na raia, inapochapisha takwimu hizo.

Israel imetoa amri ya kuhama kwa watu kaskazini mwa Gaza, lakini Philippe Lazzarini kutoka shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi wa Kipalestina (UNRWA) anasema watu 400,000 wamenaswa katika mapigano.

Israel yasema imeshambulia maeneo 185 ya Hezbollah katika saa 24 zilizopita

Vifusi kutokana na jengo lililoharibiwa katika vitongoji vya kusini mwa Beirut, kama ilivyoonekana Jumanne

Jeshi la Israel leo asubuhi lilitoa taarifa kuhusu mapigano katika muda wa saa 24 zilizopita, likisema yalipiga takribani maeneo 185 ya Hezbollah nchini Lebanon.

Katika taarifa, Vikosi vya Ulinzi vya Israel vinasema wanajeshi wake walijihusisha katika “makabiliano ya karibu” na wapiganaji wa Hezbollah waliokuwa ardhini kusini mwa Lebanon, pamoja na kufanya mashambulizi zaidi ya anga.

Wakati wa mapigano ya ardhini, kamanda wa Israel aliuawa kwa kurushiana risasi, IDF inasema.

Hezbollah hapo awali ilidai kuwa imezuia uvamizi wa Israel katika maeneo ya mashariki na magharibi mwa mpaka wa Lebanon.

IDF pia inasema ililenga maeneo 45 ya Hamas katika Ukanda wa Gaza katika muda wa saa 24 zilizopita.

Kitabu kinadai Trump alituma kwa siri mashine za kupima Covid kwa Putin

.

Kitabu kipya cha mwandishi mkongwe wa Watergate Bob Woodward kinasema Donald Trump alituma kwa siri mashine za kupima Covid-19 kwa Vladimir Putin kwa matumizi ya kibinafsi wakati zilikuwa na uhaba, madai ambayo yalikataliwa kwa hasira na kambi ya kampeni ya Trump.

Kitabu hicho kwa jina ‘War’- pia kinajumuisha madai kwamba Trump amekuwa akiwasiliana kwa siri na Putin tangu alipoondoka madarakani, kwa mujibu wa nukuu zilizotajwa na vyombo vya habari vya Marekani.

Kambi ya Trump ilisema hakuna hata moja ya “madai hayo ya kubuni” ambayo ni ya kweli.

“Rais Trump hakumpa idhini kabisa ya kufikia kitabu hiki kisicho na thamani kabisa ambacho ama kiko kwenye kasha la vitabu vyenye kuuzwa kwa bei ya chini au kinachotumika kama karatasi ya shashi,” alisema msemaji wa kambi ya Trump Steven Cheung katika taarifa yake kwa BBC.

Kitabu hicho kipya, kitakachotolewa wiki ijayo, kinahusisha kuendelea kwa mawasiliano kati ya rais huyo wa zamani na Putin na msaidizi mmoja wa Trump ambaye hajatajwa kwenye kitabu hicho.

Kesi ya kumuondoa Gachagua madarakani yatua rasmi Bunge la Seneti

th

Bunge la Seneti nchini Kenya litaanza kujadili hoja ya kumuondoa afisini Naibu wa rais Rigathi Gachagua siku za Jumatano na Alhamisi wiki ijayo.

Seneti leo imefanya kikao kupokea hoja hiyo kutoka kwa Kiongozi wa walio wengi Aaron Cheruyot baada ya bunge la kitaifa kupifa kura ya kumuondoa afisini Gachagua siku ya Jumanne.

Bunge zima la Seneti litachunguza mashtaka dhidi ya Gachagua na kusikiliza ushahidi kutoka pande zote .

Gachagua alitimuliwa Jumanne baada ya wabunge 281 kupiga kura ya kuunga mkono kuondolewa kwake afisini.

Kiwango kilichowekwa na katiba ni angalau wabunge 233.

Hezbollah inasema iliwarudisha nyuma wanajeshi wa Israel kwenye mpaka

.
Maelezo ya picha,Nyumba iliyoko Kiryat Yam, karibu na Haifa, iliyoharibiwa na roketi ya Hezbollah siku ya Jumanne

Hezbollah inasema iliwavizia wanajeshi wa Israel kwa kifaa cha kulipua usiku kucha, wakati wakijaribu kuelekea mji wa Blida, karibu na mpaka wa Israel-Lebanon upande wa mashariki.

Vile vile, Hezbollah inasema ilirudisha nyuma kikosi cha Israel kilichojaribu kuingia katika eneo la Labouneh, karibu na pwani ya magharibi mwa Lebanon.

Hezbollah ilirusha makombora kaskazini mwa Israel

.
Maelezo ya picha,Moshi ukipaa kusini mwa Beirut

Wakati huo huo, Jeshi la Israel linasema limenasa makombora mawili yaliyorushwa kutoka Lebanon asubuhi ya leo kuelekea maeneo ya Carmel na Menashe, kusini mwa mji wa bandari wa Haifa.

Ving’ora vya mashambulizi ya anga pia vilisikika katika mji wa Kaisaria, ulioko kwenye pwani kati ya Haifa na Tel Aviv.

Siku ya Jumanne, Israel ilisema iligundua roketi 180 zilizorushwa kutoka Lebanon.

Baadhi ya maeneo 100 yalilengwa katika eneo la Haifa – mengi yalinaswa, lakini mengine yalifika kwenye vitongoji vya Kiryat Yam na Kiryat Motzkin.Wakati huo huo, Jeshi la Israel linasema limenasa makombora mawili yaliyorushwa kutoka Lebanon asubuhi ya leo kuelekea maeneo ya Carmel na Menashe, kusini mwa mji wa bandari wa Haifa.

Ving’ora vya mashambulizi ya anga pia vilisikika katika mji wa Kaisaria, ulioko kwenye pwani kati ya Haifa na Tel Aviv.

Siku ya Jumanne, Israel ilisema iligundua roketi 180 zilizorushwa kutoka Lebanon.

Baadhi ya maeneo 100 yalilengwa katika eneo la Haifa – mengi yalinaswa, lakini mengine yalifika kwenye vitongoji vya Kiryat Yam na Kiryat Motzkin.

Msumbiji yafanya uchaguzi huku chama tawala kikitarajiwa kudumisha uongozi

.

Vituo vya kupiga kura vimefunguliwa nchini Msumbiji huku watu milioni 17 wakitarajiwa kupiga kura katika uchaguzi wa rais, pamoja na uchaguzi wa wabunge na majimbo.

Katika uchaguzi huo chama tawala cha Frelimo kinatarajiwa kudumisha utawala wake.

Rais Filipe Nyusi anajiuzulu baada ya mihula miwili na mgombea wa chama hicho Daniel Chapo anatarajiwa kuchukua nafasi yake.

Frelimo imetawala Msumbiji tangu uhuru kutoka kwa Ureno mwaka 1975.

Daniel Chapo atakuwa kinyang’anyironi na Venancio Mondlane, mgombea binafsi mwenye haiba ambaye amevutia umati mkubwa wa watu, kamanda wa zamani wa waasi Ossufo Momade, na kiongozi mdogo wa chama cha upinzani, Lutero Simango.

Matokeo ya uchaguzi huo yanatarajiwa kutangazwa kabla ya Oktoba 24.

Msumbiji imekuwa ikikabiliana na uasi wa Kiislamu katika eneo la kaskazini ambao umesababisha kusitishwa kwa miradi ya mabilioni ya dola ya gesi huku maelfu ya wakaazi wakihama makwao.

Umaskini pia ni tatizo kwa idadi kubwa ya watu waliojiandikisha kupiga kura.

Brazil yaondoa marufuku dhidi ya X baada ya kampuni hiyo kulipa faini ya dollar milioni 5

.

Mahakama ya Juu Zaidi ya Brazil imesema kuwa inaondoa marufuku ya mtandao wa kijamii wa X, ambao zamani ulijulikana kama Twitter.

Katika uamuzi wake, Jaji Alexandre de Moraes alisema kwamba aliidhinisha “kurudishwa mara moja” kwa shughuli za mtandao wa X nchini humo baada ya kulipa faini kubwa na kuzuia akaunti zinazotuhumiwa kueneza habari potofu.

Kulingana na taarifa, jukwaa hilo limelipa faini ya jumla ya reais milioni 28 ($5.1m; £3.8m) na kukubali kuteua mwakilishi wa eneo hilo, kama inavyotakiwa na sheria ya Brazil.

Moraes alikuwa amezuia ufikiaji wa jukwaa hilo linalomilikiwa na Elon Musk, baada ya kukataa kupiga marufuku wasifu kadhaa uliochukuliwa na serikali kueneza habari potofu kuhusu uchaguzi wa Rais wa Brazil wa 2022.

Shirika la mawasiliano nchini Brazil, Anatel, limeagizwa kuhakikisha huduma imeanza tena kwa watumiaji zaidi ya milioni 20 nchini humo ndani ya saa 24.

Baada ya miezi kadhaa ya kukaidi maagizo ya mahakama, Musk aliwafuta kazi wafanyakazi wa kampuni hiyo wa Brazil mwishoni mwa Agosti na kufunga ofisi ya X nchini Brazil.

“Uamuzi wa kufunga ofisi za X nchini Brazil ulikuwa mgumu,” Musk, ambaye pia ni mkuu wa kampuni ya kutengeneza magari ya umeme ya Tesla na kampuni ya roketi ya SpaceX, aliandika wakati huo.

Aliyejitangaza kama “mtiifu wa uhuru wa kuzungumza”, mfanyabiashara huyo bilionea alielezea hatua ya Jaji Moraes ya kupiga marufuku akaunti kadhaa kama matumizi mabaya ya mamlaka na ukiukaji wa uhuru wa kujieleza.

Siku kadhaa baadaye, Jaji Moraes aliamuru jukwaa zima kuzuiwa kote nchini humo.

Watumiaji wengi walihamia kwenye majukwaa mbadala kama vile Bluesky, na mahitaji ya VPN (Virtual Proxy Networks) nchini Brazili yaliongezeka.

Raia wa Afghanistan akamatwa kwa madai ya njama ya shambulizi siku ya uchaguzi wa Marekani

.

Wizara ya Sheria ya Marekani imemkamata mtu anayedaiwa kupanga shambulizi siku ya Uchaguzi na anahusishwa na kundi la Islamic State.

Mshukiwa, Nasir Ahmad Tawhedi, 27, ni raia wa Afghanistan anayeishi katika mji wa Oklahoma, kulingana na waendesha mashtaka.

Mkurugenzi wa FBI Christopher Wray alisema katika taarifa ya Jumanne kwamba: “Mshtakiwa huyu, akichochewa na ISIS, alikula njama ya kufanya shambulio la kikatili, Siku ya Uchaguzi, hapa nchini kwetu.”

FBI ilisema alikuwa akijaribu kuhifadhi silaha, na alikuwa amechukua hatua kuuza mali za familia yake na kuwahamisha wanafamilia wake nje ya nchi.

Bw Tawhedi anashtakiwa kwa kutoa, kujaribu kutoa, na kula njama ya kusaidia au kutoa rasilimali kwa shirika la kigeni la kigaidi; na kwa kujaribu kununua bunduki na risasi za kutumia kufanya uhalifu au kitendo cha kigaidi.

FBI ilisema Bw Tawhedi alifanya kazi na mwenzake ambaye jina lake halikutajwa, jamaa wake mwenye umri mdogo na pia ni raia wa Afghanistan.

Inamtuhumu kwa kutumia propaganda za Islamic State kupitia mtandao, kulingana na rekodi za Google zilizopatikana na vyombo vya sheria, na kutoa michango kwa shirika la kutoa msaada linalotumika na IS.

“Tutaendelea kupambana na tishio linaloendelea ambalo ISIS na wafuasi wake wanaleta kwa usalama wa taifa wa Marekani, na tutawatambua, kuwachunguza na kuwafungulia mashtaka watu wanaotaka kuwatisha watu wa Marekani,” alisema Mwanasheria Mkuu Merrick Garland.

Bw Tawhedi alitafuta bunduki aina ya AK-47 ili kutumia katika shambulio hilo, mamlaka zinadai.

Mnamo tarehe 7 Oktoba, yeye na mwanzilishi mwenza walikutana na watu ambao kwa kweli walifanya kazi kwa siri kwa FBI kununua silaha na risasi.

Baada ya ununuzi huo, Bw Tawhedi na mshiriki mwenzake walikamatwa.

Bw Tawhedi aliwasili Marekani mnamo Septemba 2021 kwa visa maalum ya wahamiaji pamoja na mkewe na mtoto wake mdogo.

Alikuwa anaishi katika mji wa Oklahoma wakati wa kukamatwa kwake.

Haijabainika mara moja ikiwa ana uwakilishi wa kisheria.

Urusi inadhamiria kusababisha ghasia katika mitaa ya Uingereza, inaonya MI5

.

Shirika la kijasusi la Urusi limekuwa likifanyia kazi suala la kuhakikisha kuna “ghasia endelevu katika mitaa ya Uingereza na Ulaya”, mkuu wa MI5 amesema.

Akitoa taarifa yake ya kila mwaka kuhusu vitisho vya usalama vinavyoikabili Uingereza, Ken McCallum alisema maafisa wa ujasusi wa GRU waliendeleza vitendo vya “uchomaji moto, hujuma na vingine vya hatari zaidi pamoja na kuongezeka kwa uzembe” nchini Uingereza baada ya nchi hiyo kuunga mkono Ukraine katika vita vyake na Urusi.

MI5 pia imejibu njama 20 zilizoungwa mkono na Iran tangu 2022, alisema, ingawa aliongeza kuwa kazi zake nyingi bado zinahusisha itikadi kali za Kiislamu na kufuatiwa na ugaidi uliokithiri wa mrengo wa kulia.

Mchanganyiko wa vitisho vinavyohusiana na ugaidi kutoka kwa mataifa ulimaanisha MI5 ilikuwa na “kazi moja walioyoipa kipaumbele”, alionya.

Katika hotuba yake ya wigo mpana, alisema:

  • Vijana walikuwa wakivutiwa zaidi na itikadi kali mtandaoni, huku 13% ya wale waliochunguzwa kwa kuhusika na ugaidi walikuwa na umri wa chini ya miaka 18.
  • Jumla ya njama 43 zilizofanywa dakika za mwisho zilihusisha bunduki na vilipuzi kwa nia ya kutekeleza “mauaji ya watu wengi” nchini Uingereza zilizuiliwa tangu 2017
  • Uchunguzi wa vitisho dhidi ya serikali uliofanywa na MI5 uliongezeka kwa 48%
  • Kazi ya kukabiliana na ugaidi imesalia katika pande mbili kati ya “asilimia 75 ya Waislamu wenye msimamo mkali, na 25% ni ugaidi uliokithiri wa mrengo wa kulia”

Pia kulikuwa na “imani na itikadi mchanganyiko” na ilibidi MI5 kukabiliana nazo, aliambia mkutano huo katika kituo cha oparesheni za kukabiliana na ugaidi cha MI5 huko London.

Jimbo la Florida Marekani lajitayarisha kukabiliana na kimbunga Milton

.

Wakazi wa eneo la Florida wanaharakisha kumaliza maandalizi ya dharura – au waondoke tu – huku Kimbunga Milton kikielekea kwa haraka kwenye Ghuba ya Tampa iliyo na watu wengi.

Milton kwa sasa ni dhoruba ya aina ya tano, yenye upepo mkali wa hadi 165mph (270km/h).

Kinatarajiwa kupiga kwa nguvu zote Jumatano usiku, chini ya wiki mbili baada ya jimbo hilo kukumbwa na kimbunga cha Helene.

Rais Joe Biden alionya watu huko Florida Jumanne kuondoka makwao na kulichukulia suala hilo kwa uzito mkubwa kama lenye kuhusisha “maisha au kifo” wakati jimbo hilo likijitahidi zaidi kwenye uhamishaji.

Kimbunga hicho kikiwa kimewekwa “kitengo cha tano, ni kama kimbunga kikubwa,” mkazi mmoja wa jiji la Ghuba la Bradenton aliambia BBC kutoka hoteli ambayo amehamia Kissimmee.

“Nisingependa kuwa huko,” alisema Gerald Lemus. “Hii itakuwa dhoruba isiyokifani haijalishi itakumba wapi.”

Bw Lemus, ambaye ameishi Bradenton maisha yake yote, alisema hajawahi kuhama kutokana na dhoruba zilizotangulia. Lakini aliamua kufanya hivyo kwa ajili ya usalama wa binti yake wa miaka minane.

“Nilimtazama tu na sikuweza kumtia mashaka kwa kitu kama hiki,” alisema Jumanne usiku.

“Ni hatua ya hatari ambayo hatukutaka kuichukua.”

ML Ferguson amekuwa akihangaika kujenga upya nyumba yake huko Anna Maria, Florida, baada ya kuharibiwa vibaya mwezi uliopita na kimbunga Helene, ambacho kilikuwa kikali kilichowekwa kwenye kitengo cha nne.

“Hiki kitakuwa kibaya zaidi kuliko Helene,” alisema kwenye simu akiwa katika barabara kuu nje ya jiji.

“Gari langu limeharibika kiasi cha kutoweza kutengenezeka tena, sote tulifutwa kazi, na mali [zangu] ziliharibiwa. Baada ya dhoruba hii kupiga, itakuwa rasmi sasa sina makazi.”

Kwanini Marekani imeshindwa kupata makubaliano ya amani Mashariki ya Kati?

d

Saa 2 zilizopita

Mwaka mmoja uliopita, baada ya mashambulizi ya Oktoba 7 na kuanza kwa mashambulizi ya Israel huko Gaza, Joe Biden alikua rais wa kwanza wa Marekani kuizuru Israel wakati wa vita.

Alikutana na waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu na baraza la mawaziri la vita huko Tel Aviv, na kuwaambia: “Hamuko pekee yenu.” Lakini pia aliuhimiza uongozi wa Netanyahu, kutorudia makosa ambayo Marekani iliyafanya baada ya 9/11.

Mwezi Septemba mwaka huu katika Umoja wa Mataifa mjini New York, Rais Biden aliongoza wito wa kimataifa akitaka Israel na Hezbollah zijizuie kushambuliana.

Netanyahu alitoa majibu kwa kusema Israel ina mkono mrefu, na unaweza kufika popote katika eneo la Mashariki ya Kati.

Dakika tisini baadaye, marubani wa Israel walirusha makombora yaliyotolewa na Marekani kwenye majengo ya kusini mwa Beirut.

Shambulio hilo lilimuua kiongozi wa Hezbollah Hassan Nasrallah.

Diplomasia ya Biden ilikuwa ikizikwa katika magofu ya shambulio la anga la Israel kwa kutumia mabomu yaliyotolewa na Marekani.

Lengo kuu la diplomasia kama inavyoelezwa na utawala wa Biden ni kupata usitishaji wa mapigano kwa makubaliano ya kuwaachilia huru mateka wa huko Gaza.

Mwaka mmoja baada ya Hamas kuvunja uzio wa kijeshi kuelekea kusini mwa Israel – na kuua zaidi ya watu 1,200 na kuwateka nyara 250 – ikiwa ni pamoja na raia saba wa Marekani – mateka wengi wamesalia kifungoni, huku idadi kubwa ikiaminika kuwa wamekufa.

Huko Gaza, mashambulizi makubwa ya kulipiza kisasi ya Israel yamesababisha vifo vya takribani Wapalestina 42,000, kwa mujibu wa takwimu za wizara ya afya inayoendeshwa na Hamas, eneo hilo limeharibiwa, watu wanakimbia na limekumbwa na njaa.

Umoja wa Mataifa unasema idadi kubwa ya wafanyakazi wa misaada wameuawa katika mashambulizi ya Israel, huku makundi ya kibinadamu yakiishutumu mara kwa mara Israel kwa kuzuia upelekwaji wa misaada – jambo ambalo serikali ya Israel imekuwa ikilikanusha.

Wakati huo huo, vita vimeenea hadi Ukingo wa Magharibi na Lebanon. Wiki iliyopita Iran ilirusha makombora 180 kwenda Israel kulipiza kisasi mauaji ya Nasrallah, kiongozi wa kundi la Hezbollah linaloungwa mkono na Iran.

Mafanikio na hasara

Maafisa wa Biden wanadai shinikizo la Marekani lilibadilisha “sura ya operesheni za kijeshi za Israel,” wakirejelea operesheni za Israel huko Rafah, wanaamini ilikuwa na mipaka, hata kama sehemu kubwa ya mji huo ni kifusi na magofu.

Kabla ya uvamizi wa Rafah, Biden alisimamisha shehena moja ya silaha alipokuwa akijaribu kuizuia Israel kufanya mashambulizi makubwa. Lakini rais huyo alikabiliwa na upinzani kutoka Republicans huko Washington na kutoka kwa Netanyahu mwenyewe na tangu wakati huo ameondoa usitishwaji huo na hajarudia tena kusitisha.

Wizara ya Mambo ya Nje inadai shinikizo lake kwa Israel lilifanikisha kupelekwa msaada zaidi Gaza, licha ya Umoja wa Mataifa kuripoti uwepo wa njaa huko Gaza mapema mwaka huu.

Kazi nyingi za Biden zimefanywa na mwanadiplomasia wake mkuu, Anthony Blinken. Amefanya safari kumi Mashariki ya Kati tangu Oktoba katika duru za kidiplomasia na kazi ya siri ya CIA ya kujaribu kupata makubaliano ya kusitisha mapigano Gaza kati ya Israel na Hamas.

Lakini safari hizo zilionekana kutofua dafu hasa baada ya Netanyahu kudai kuwa “amemshawishi” Blinken juu ya hitaji la kuweka wanajeshi wa Israel kwenye mpaka wa Gaza na Misri kama sehemu ya makubaliano.

Hilo lilivunja makubaliano na Hamas na Misri. Afisa mmoja wa Marekani alimshutumu Netanyahu kwa kujaribu kuhujumu makubaliano hayo. Mpango huo haukuenda popote.

Katika safari yake ya kumi katika eneo hilo mwezi uliopita, Blinken hakuitembelea Israel.

Diplomasia imefikia wapi?

Wakati Marekani inatoa wito wa kusitishwa vita huku ikiipa Israel silaha za thamani ya dola za kimarekani bilioni 3.8 kwa mwaka, na imekubali ombi la nyongeza ya silaha tarehe 7 Oktoba, inaonekana imeshindwa kutumia nguvu zake au inafanya undumilakuwili.

Wakosoaji wa Biden wakiwemo maafisa wa Marekani, wanasema upanuzi wa sasa wa vita kwa kweli unathibitisha undumilakuwili, kuliko kushindwa kwa sera ya kidiplomasia ya Marekani.

“Ni kweli Marekani imefanya diplomasia na mikutano mingi. Lakini haijafanya juhudi yoyote ya maana kubadili tabia ya mmoja wa wahusika wakuu – Israel,” anasema afisa wa zamani wa ujasusi Harrison J. Mann, Meja wa Jeshi la Marekani ambaye alikuwa akifanya kazi katika kitengo cha kijasusi cha Mashariki ya Kati na Afrika wakati wa shambulio la Oktoba 7.

Mann alijiuzulu mapema mwaka huu akipinga uungaji mkono wa Marekani kwa mashambulizi ya Israel huko Gaza na idadi ya raia wanaouawa kwa kutumia silaha za Marekani.

Washirika wa Biden wanakataa ukosoaji huo. Wanatoa mfano upatanishi uliosababisha wa mwezi Novemba mwaka jana ambao ulishuhudia mateka zaidi ya 100 wakiachiliwa huru huko Gaza na karibu wafungwa 300 wa Kipalestina wanaoshikiliwa na Israel wakiachiwa.

Maafisa wa Marekani pia wanasema utawala huo uliizuia Israel kuivamia Lebanon mapema zaidi wakati mzozo wa Gaza unaanza, licha ya kurushwa kwa roketi za Hezbollah kwenda Israel.

Seneta Chris Coons, muungaji mkono wa Biden ambaye hushiriki katika Kamati ya Seneti ya Mahusiano ya Kigeni na amesafiri kwenda Israel, Misri na Saudi Arabia mwishoni mwa mwaka jana, anasema ni muhimu kuipima diplomasia ya Biden na hali ya mwaka jana.

“Nadhani pande zote mbili zinahusika kwa kutopatikana kwa makubaliano, lakini hatuwezi kupuuza au kusahau kwamba Hamas ndio ilianzisha mashambulizi haya,” anasema.

“Amefanikiwa kuzuia chokochoko za kichokozi za mara kwa mara kutoka kwa Wahouthi, na Hezbollah, na wanamgambo wa Shia nchini Iraq – na amewaleta pamoja washirika wetu wa kikanda,” anasema.

Waziri mkuu wa zamani wa Israel, Ehud Olmert anasema uungaji mkono wa Biden umekwenda katika kiwango ambacho hakijawahi kushuhudiwa, akiashiria kupelekwa kwa jeshi kubwa la Marekani, ikiwa ni pamoja na meli za kivita zinazobeba ndege na nyambizi ya nyuklia.

Lakini anaamini Biden ameshindwa kuushinda upinzani wa Netanyahu.

“Kila mara alipokaribia kufanikiwa, Netanyahu kwa namna fulani alipata sababu ya kutotii, hivyo sababu kuu ya kushindwa kwa diplomasia hii ni upinzani wa mara kwa mara wa Netanyahu,” anasema Olmert.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment