“MUONE, KIKO WAPI SASA” Nikakumbuka kuwa Cheo, nafasi, umaarufu, Pesa n.k ni vitu unavyoweza kuvipoteza muda wowote ila UTU ndio UTAKULINDA.

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

“MUONE, KIKO WAPI SASA” Hivi karibuni nilikuwa nahudhuria tukio kubwa sana la kiserikali kwenye maadhimisho fulani.

Nilipoketi nyuma yangu kulikuwa na watu wawili walikuwa wanazungumza wakati tukio linaendelea.

Nikasikia wakisema, “Mwangalie yule anapita pale (huku wanacheka)”, Kisha mwenzake akasema “Muone, kiko wapi sasa”.

Kadiri walivyoendelea kuongea nikagundua wanamzungumzia mtu mmoja ambaye aliwahi kuwa kiongozi mkubwa.

Kwa mujibu wa mazungumzo yao, kiongozi huyo alikuwa anajidai sana na aliumiza watu wengi mno.

Sasa, hii siku ya hili tukio alikuwepo Ila hakuna mtu alikuwa ana mjali na hakuwa anapewa heshima na mtu yeyote.

Ilinitafakarisha sana.

Nikakumbuka kuwa Cheo, nafasi, umaarufu, Pesa n.k ni vitu unavyoweza kuvipoteza muda wowote ila UTU ndio UTAKULINDA.

Yaani, hutakiwi Kujisahau kwa kitu kinachokupa nguvu ambacho UMEAZIMWA.

Siku ukinyan’ganywa unageuka kuwa STORI.

Mungu atusaidie tusipoteze UTU na TUSIDHARAU WATU ili tusigeuzwe STORI MAJUKWAANI.

Kama umeipenda makala hii…

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment