Siasa Ghana

Na Cantona Joseph Julai 03, 2026 08:40 (EAT

Ghana na Afrika Kusini zimeingia kwenye mzozo mpya wa kidiplomasia kufuatia mauaji ya mhamiaji nchini Afrika Kusini. Serikali ya Afrika Kusini ilisema kifo hicho hakihusiani na maandamano ya kupinga wahamiaji.

Afrika Kusini imeshuhudia wiki kadhaa za machafuko kuhusu suala la uhamiaji haramuPicha: Oupa Nkosi/REUTERS

Taarifa hiyo imetolewa baada ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Ghana Jumatano kusema kwamba raia wake Bashiru Isak, mwenye umri wa miaka 40, alipigwa risasi na kuuawa wakati wa maandamano hayo.

Ghana ilisema iliwasilisha rasmi malalamiko yake kwa Pretoria. Lakini serikali ya Afrika Kusini ilipuuza madai ya Ghana kuhusu mauaji hayo kama “yasiyo sahihi” na “yasiyotokana na ukweli.” Ilisema “hakuna vifo” vilivyoorodheshwa mnamo siku ya maandamano ambayo yalishuhudia maelfu ya watu wakiandamana  mitaani katika sehemu mbalimbali za nchi.

Maelfu kadha ya watu waliandamana kote Afrika Kusini siku ya Jumanne wakitaka kukomeshwa kwa uhamiaji usio na vibali nchini humo. Waandamanaji waliweka tarehe ya mwisho isiyo rasmi ya Juni 30 kwa wahamiaji wasio na vibali kuondoka nchini humo.Zaidi ya watu 25,000, wakiwemo mamia ya Waghana, tayari wamekimbia nchi hiyo, kulingana na vikosi vya usalama vya Afrika Kusini.

https://www.youtube.com/live/4wQyUNw03cg?si=UmLWPrOlYSQ3845M

Ukraine, Urusi zaapa kuendeleza mashambulizi yao

Migogoro Ukraine

Urusi ilisema mashambulizi hayo yalikuwa ya kulipiza kisasi kwa mashambulizi ya hivi karibuni ya UkrainePicha: Genya Savilov/AFP

Ukraine na Urusi zimeapa kufanya mashambulizi mapya katika vita vyao vya zaidi ya miaka minne baada ya Moscow kufanya mashambulizi makali mjini Kyiv, na kuua watu wasiopungua 27.

Mashambulizi hayo yaliharibu majengo ya ghorofa na kusababisha makumi ya maelfu ya watu kukimbilia kwenye maeneo ya hifadhi. Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky alisema vikosi vyake bila shaka vitalipiza kisasi kwa mashambulizi hayo ya usiku kucha alipokuwa akikagua jengo la ghorofa ambalo lilikuwa limeharibiwa kwa sehemu.

Mwanadiplomasia mkuu wa Umoja wa Ulaya Kaja Kallas alipendekeza vikwazo vipya dhidi ya Moscow, huku Zelensky akiishinikiza Marekani kutoa leseni za kutengeneza makombora ya ulinzi wa anga ya Patriot. 

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres alilaani vikali mashambulizi hayo Urusi na kurudia wito wa kusitishwa mapigano.

Msemaji wake Stephane Dujarric alisema mashambulizi dhidi ya raia na miundombinu ya raia popote yanapotokea ni ukiukwaji wa wazi wa sheria za kimataifa za kibinadamu na lazima yasitishwe mara moja. Lakini Kremlin iliapa kuongeza “shinikizo” zaidi dhidi ya Kyiv. Jeshi la anga la Ukraine lilisema Urusi ilirusha droni 496 na makombora 74, ikiwa ni pamoja na makombora ya balestiki ambayo ni magumu kuyadungua. Lilisema liliyadungua 48 kati ya makombora hayo na droni 476.

https://www.youtube.com/live/4wQyUNw03cg?si=IyNgOPTJB_Z7I3Iq

UN kufunga ofisi yake ya haki za binadamu Burkina Faso

Siasa Burkina Faso

Umoja wa Mataifa umetangaza kwamba utafunga ofisi yake ya haki za binadamu nchini Burkina FasoPicha: DW

Umoja wa Mataifa umetangaza kwamba utafunga ofisi yake ya haki za binadamu nchini Burkina Faso ukisema hatua ya mamlaka kusimamisha kwa muda usiojulikana operesheni zake inamaanisha haiwezi kutekeleza majukumu yake.

Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Volker Turk amesema hatua ya utawala wa kijeshi kusimamisha kwa muda usiojulikana operesheni zake inamaanisha ofisi yake haiwezi kutekeleza majukumu yake. Uamuzi huo unajiri miezi mitatu baada ya Burkina Faso inayotawaliwa na jeshi kusimamisha kazi ya ofisi hiyo kutokana na taarifa kwa vyombo vya habari ambayo ilikuwa imeitaka taifa hilo la Afrika Magharibi kuheshimu haki na nafasi ya kiraia. 

Tawi la Ofisi ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa nchini humo linatarajiwa kufungwa ifikapo Novemba 30. Mkuu wa utawala wa kijeshi Kapteni Ibrahim Traore, mwenye umri wa miaka 38, amefuata sera za kupinga nchi za Magharibi tangu alipochukua madaraka katika mapinduzi mnamo Septemba 2022, huku sauti za wakosoaji zikikabiliwa na ukandamizaji.

Ofisi hiyo ilianzishwa Oktoba 2021 na ilikuwa imefanya ufuatiliaji na utafiti wa haki za binadamu na kutetea kuheshimiwa kwa haki za binadamu. Pia ilikuwa imewafunza karibu maafisa 4,000 wa vikosi vya ulinzi na usalama kuhusu sheria ya kimataifa ya haki za binaadamu na sheria ya ubinaadamu.

Serikali ya Muungano Ujerumani yazindua mageuzi makubwa

Uchumi Ujerumani

Baada ya mazungumzo ya usiku mrefu, viongozi wa muungano walirudi kwenye ofisi ya Kansela kuwasilisha mageuzi yao yaliyopendekezwaPicha: Michael Kappeler/dpa/picture alliance

Kansela wa Ujerumani Friedrich Merz na washirika wake wa serikali ya muungano wameidhinisha mpango mahsusi wa mageuzi kwa lengo la kuuimarisha uchumi wa nchi hiyo unaoyumba.

Kansela wa Ujerumani Fredrick Merz na washirika wake wa serikali ya muungano wameidhinisha mpango mahsusi wa mageuzi kwa lengo la kuuimarisha uchumi wa nchi hiyo unaoyumba. Tangazo hilo lilitolewa katika mkutano na waandishi wa habari siku ya Alhamisi, na Merz akiwa pamoja na viongozi wa SPD Bärbel Bas na Lars Klingbeil, na kiongozi wa Chama cha Kihafidhina cha Bavaria, Christian Social Union Markus Soder.

Vipengele hivyo 34 ni pamoja na kupunguzwa kwa kodi ya mapato kwa familia zenye kipato cha chini na cha kati,marekebisho ya mfumo wa pensehni unaozidi kuporomoka, sheria kali za likizo ya kuugua wafanyakazi na kupunguza urasimu unaokandamiza nchi. Merz amesema lengo kuu la mageuzi hayo ni kuboresha uchumi na kurejesha ushindani.

Muungano wa Merz wa vyama vya siasa za wastani za mrengo wa kulia na za wastani za mrengo wa kushoto uliingia madarakani zaidi ya mwaka mmoja uliopita kwa ahadi za mageuzi na kuufufua uchumi unaoyumba wa Ujerumani, ambao ni mkubwa zaidi barani Ulaya.

Urusi yaituhumu Ulaya kwa kuchochea mzozo wake na Ukraine

Migogoro Ulaya

Msemaji wa Ikulu ya Kremlin Dmitry Peskov akiwa mjini MoscowPicha: Alexander Kazakov/TASS/ZUMA/picture alliance

Kamanda Mkuu wa Jeshi la Urusi amempa taarifa Rais Vladimir Putin kuhusu mashambulizi makubwa waliyoyafanya kwenye miji kadhaa ya Ukraine ikiwemo Kyiv.

Ikulu ya Kremlin imesema itaongeza shinikizo kwa Ukraine ili kufikia malengo yake. Katika shambulio hilo,  watu wasiopungua 17 wameuwawa   na wengine zaidi ya 40 wamejeruhiwa.

Msemaji wa Ikulu ya Kremlin Dmitry Peskov ameilaumu Ulaya kwa kuuchochea mzozo huo akiapa kuwa Urusi haiwezi kufumbia macho mwenendo huo:

“Hakuna shaka kwamba Ulaya ndio inayochochea mzozo huu huku ikiimarisha nguvu zake za kijeshi ikijiandaa kukabiliana na Shirikisho la Urusi, hili halina shaka kabisa. Jambo hili linazidisha mvutano ambao tayari umeongezeka barani Ulaya. Jambo hili linatufanya tuchukue hatua za ziada ili kuhakikisha usalama wetu wenyewe,” alisisitiza Peskov.

Wakati huo huo, Mkuu wa Sera za Nje wa Umoja wa Ulaya, Kaja Kallas, amesema atapendekeza vikwazo vipya kwa viwanda vya kijeshi vya Urusi, ili kuongeza shinikizo kwa Moscow hadi pale itakapoelewa kuwa haiwezi kuvishinda vita hivyo.

afghanistanafricaalbaniaalgeriaAmericaamerican-samoaandorraangolaanguillaantarcticaantigua-and-barbudaargentinaarmeniaarubaarushaaustraliaaustriaazerbaijanbahamasbahrainbangladeshbarbadosbelarusBelgiumbelizebeninbermudabhutanboliviabosnia-and-herzegovinabotswanaBoukinafasobrazilbrunei-darussalambulgariaburkina-fasoburmaburundicaliforniacambodiacamerooncanadacape-verdecayman-islandscentral-african-republicChadchicagochilechinachristmas-islandcocos-keeling-islandscolombiacomoroscongocook-islandscosta-ricacote-divoire-ivory-coastCroatiacubacyprusczech-republicdarsalaamdemocratic-peoples-rep-north-koreademocratic-republic-of-the-congo-kinshasadenmarkdjiboutidodomadominicadominican-republicdr-congodubaieast-timor-timor-lesteecuadoregyptegyptyel-salvadorenglandequatorial-guineaequitorial-guineaeritreaestoniaeswatiniethiopiafalkland-islandsfaroe-islandsfederal-states-of-moldovafijifinlandFloridafrancefrench-guianafrench-polynesiafrench-southern-territoriesgabongazageorgiagermanyghanagibraltargomaGreecegreenlandgrenadaguadeloupeguamguatemalaguineaguinea-bissauguyanahabarihaitiholy-seehondurashong-konghoustonhungaryicelandindiaindonesiaIowairaniran-islamic-republic-ofiraqirelandisraelitaliaitalyivory-coastjamaicajapanjordankaratukazakhstankilimanjarokinshasakiribatikiswahilikoreakosovokuwaitkyrgyzstanlaolatvia-lebanon-lesotho-liberia-libya-liechtenstein-lithuania-luxembourgLebanonliberiamacaumadagascarmalawimalaysia-maldivesMalimaltamarshall-islands-martinique-mauritania-mauritiusmassechutesmayottemazingirambeyamerumexicomiamimicronesiamonaco-mongolia-montenegromontserratmoroccomozambique-myanmarmtwaramwanzanamibianaurunepalnetherlandsnetherlands-antillesnevadanew-caledonianew-zealandnewyorknicaraguanigernigerianiuenorth-macedonianorthern-mariana-islandsnorwayomanpakistanpalaupalestinepalestinian-territoriespanamapapua-new-guineaparaguaypeoples-democratic-republicperuphiladhephiaphilipiansPhilippinespitcairn-islandpolandpoliticsPortugalpuerto-ricoqatarrepublic-ofrepublic-of-brazzavillerepublic-of-south-koreareunion-islandromaniaRussiarussian-federationrwandasahara-occidentalsaint-kitts-and-nevissaint-luciasaint-vincent-and-the-grenadinessamoasan-marinosao-tome-and-principesaudi-arabiasaudiarabiascotlandSenegalserbiaseychellessierra-leoneSingaporesingidaslovakia-slovak-republicsloveniasolomon-islandssomaliasouthafricaspainsri-lankasudansurinameswaziland-eswatiniswedenswitzerlandsyriasyrian-arab-republictaborataiwan-republic-of-chinatajikistantanzaniatexasthailandthe-gambiatibettimor-leste-east-timortogotokelautongatorontotrinidad-and-tobagotunisiaturkeyturkmenistanturks-and-caicos-islandstuvaluugandaunited-arabs-emiratesunited-kingdomunited-statesuruguayuzbekistanvancovervanuatuvatican-city-state-holy-seevenezuelavietnamvirgin-islands-britishvirgin-islands-u-swallis-and-futuna-islandswallis-and-futuna-islandswallis-et-futunawashington-dcwestern-saharayemenzambiazambiezimbabwe

CantonaDigital
CantonaDigital

Listen Live Radio Fortune Africa
Ukweli Na Burudani.

-Be ready to be Impacted, Inspired & Empowered.

-Keep watching our Channels

Cantona Cast Television,

Fortune Television Network (FTN)

Donation
Paypal https://www.paypal.com/donate/?hosted_button_id=6EKXMLNW8W6A2&fbclid=IwY2xjawQxeChleHRuA2FlbQIxMABicmlkETFRdkNBRndpclRDQTB5bXZZc3J0YwZhcHBfaWQQMjIyMDM5MTc4ODIwMDg5MgABHq960uGsyU3ABRIBc2h-iXGhHATvuEqe55gFsQ-rDb0fT-Z7SIQ3TV8LnkpD_aem_ybU2SvBlvyqrVsS9NAczRw

An attitude determines an altitude.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2025

5,565 posts
0 followers

Fediverse Followers


Discover more from Cantona. Digital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a Reply

About us

Welcome to Cantona Group PLC-Where media meets moments.

Cantona Group PLC is a Premier Multi Media Group, where we connect live Broadcasting with world-class Production. We break the latest news in real-time, shape public perception, and produce captivating audio-visual content all under one roof.

Discover more from Cantona. Digital

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading

Discover more from Cantona. Digital

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading