Na Cantona Joseph

Siasa Mashariki ya Kati

Wajumbe wa Marekani na Iran kuendelea na mazungumzo ya kitaalamu DohaPicha: Fabrice Coffrini/AFP

Mtandao wa habari nchini Marekani wa Axious umedai kuwa wajumbe wa Marekani na Iran, wanatarajiwa kukutana kesho Jumanne mjini Doha, kujadili juhudi za kusitisha kikamilifu vita baina yao.

Hata hivyo msimamo wa Iran katika mazungumzo hayo hadi sasa bado haujajulikana.

Mazungumzo hayo hapo awali yalipangwa kufanyika Uswisi na kujikita katika mpango wa nyuklia wa Iran, lakini yalihamishwa kwenda Qatar ili kujadili kwa upana suala la Mlango Bahari wa Hormuz kufuatia mvutano ulioibuka hivi karibuni.

Makubaliano ya muda ya amani kati ya Marekani na Iran, yaliyotiwa saini tarehe 17 Juni, yamekuwa yakikiukwa na pande zote mbili kufuatia mashambulizi ya kijeshi kati ya nchi hizo.

Siku ya Jumapili, Rais wa Marekani  Donald Trump alionya katika mtandao wake wa kijamii wa Truth Social kwamba Jamhuri ya Kiislamu ya Iran itashambuliwa na kuondolewa kabisa duniani ikiwa itafika hatua ambapo Trump ataamua kuwa Marekani haitakuwa tena na uvumilivu na Tehran.

Siasa Amerika Ya Kaskazini

China kutuma dola milioni 14.7 kusaidia Venezuela

Wizara ya mambo ya nje ya China imesema nchi hiyo itatuma dola milioni 14.7, kama msaada wa dharura kwa Venezuela, baada ya matetemeko mawili makubwa ya ardhi yaliyosababisha vifo vya watu zaidi ya 1,450.

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Guo JiakunPicha: Johannes Neudecker/dpa/picture alliance

Maelfu ya watu wengine wamejeruhiwa huku zaidi ya 50,000 wakiwa hawajulikani waliko.

Msemaji wa wizara hiyo Guo Jiakun ameuambia mkutano wa waandishi habari kwamba, China itasaidia pia katika ujenzi mpya wa  Venezuela  baada ya janga hilo pamoja na kusaidia kutoa picha za satelaiti za maeneo yaliyoathirika ili kusaidia katika shughuli za uokoaji.

“China ina wasiwasi mkubwa kuhusu janga la tetemeko la ardhi nchini Venezuela. Rais Xi Jinping ametuma salamu zake za rambirambi kwa Rais wa mpito wa Venezuela Delcy Rodríguez. Serikali ya China imeamua kuipatia Venezuela msaada wa ziada wa dola milioni 14.7 ili kusaidia juhudi za uokoaji na ujenzi mpya baada ya maafa. Vifaa vya msaada vitasafirishwa kwenda Venezuela haraka iwezekanavyo.”

Jiakun ameongeza kuwa China itatoa msaada zaidi kwa Venezuela kadri hali itakavyoendelea kubadilika.

Siku ya Jumatano, Venezuela ilipigwa na matetemeko mawili ya ardhi yenye ukubwa wa 7.2 na 7.5 katika kipimo cha Richter na kusababisha maafa na uharibifu mkubwa wa mali na miundombinu.

Raia nane wa China ni miongoni mwa walioangamia katika janga hilo.

Siasa Ya Afrika

Mkuu wa Jeshi Uganda afungia vyombo vikubwa huru vya habari

Mkuu wa jeshi nchini Uganda Jenerali Muhoozi Kainerugaba amesema amesitisha shughuli za mashirika makubwa huru ya habari nchini humo, kufuatia kile alichokiita kutoamini katika uhuru wa vyombo vya habari.

Kainerugaba ambaye ni mtoto wa rais wa Uganda  Yoweri Museveni  aliyeko madarakani tangu mwaka 1986, amesema alichokifanya ni mwanzo tu wa hatua zake dhidi ya vyombo vya habari akitishia na kuonya kuwakamata waandishi habari zaidi.

Mkuu huyo wa jeshi la Uganda jana Jumapili aliamuru kufungwa kwa televisheni, redio na magazeti ya chombo cha Nation Media Group na gazeti la Daily Monitor.

Ameongeza kuwa ana mamlaka ya kufunga chombo chochote cha habari anachotaka kutokana na mamlaka aliyopewa na babayake tangu mwaka 2017. Amesema vyombo vyote nchini humo vinapaswa kufuata maagizo ya serikali.

Kipenga Cha Michezo

la Dunia

Nagelsmann: Ujerumani lazima ishinde kombe

Kocha wa Ujerumani, Julian Nagelsmann, amesema kwamba kushinda Kombe la Dunia pekee ndio jambo linaloweza kuwanyamazisha wanaotilia shaka uwezo wa timu yake.

Licha ya kusonga mbele kama washindi wa Kundi E baada ya kuwacharaza Curacao 7-1 na ushindi wa dakika za mwisho wa 2 – 1 dhidi ya Ivory Coast,  kushindwa na Ecuador katika mchezo wao wa mwisho kumeibua mashaka zaidi kuhusu nafasi ya  Ujerumani kusonga mbele katika mashindano hayo.

Ujerumani inashuka dimbani leo dhidi ya Paraguay iliyomaliza katika nafasi ya tatu katika kundi lao. Kama watapata ushindi, vijana hao wa Nagelsmann wanaweza kukutana na Ufaransa katika raundi ya 16. Katika mechi nyingine ya leo, Brazil watakabana koo na Japan.

Naglesmann amewaambia waandishi habari kabla ya mechi leo kuwa unapozungumzia timu ya taifa ya Ujerumani, matarajio ni kushinda kila mchezo.

Amesema njia bora ya kukabiliana na matarajio ni kujiamini tu, kuwa na mpango mzuri, kujaribu kuwapa wachezaji mpango mzuri ili waweze kujisikia vizuri uwanjani, wawe na uwezo wa kufanya mambo sahihi uwanjani, kuonyesha wao ni wachezaji wazuri na kushinda mchezo.

afghanistanafricaalbaniaalgeriaAmericaamerican-samoaandorraangolaanguillaantarcticaantigua-and-barbudaargentinaarmeniaarubaarushaaustraliaaustriaazerbaijanbahamasbahrainbangladeshbarbadosbelarusBelgiumbelizebeninbermudabhutanboliviabosnia-and-herzegovinabotswanaBoukinafasobrazilbrunei-darussalambulgariaburkina-fasoburmaburundicaliforniacambodiacamerooncanadacape-verdecayman-islandscentral-african-republicChadchicagochilechinachristmas-islandcocos-keeling-islandscolombiacomoroscongocook-islandscosta-ricacote-divoire-ivory-coastCroatiacubacyprusczech-republicdarsalaamdemocratic-peoples-rep-north-koreademocratic-republic-of-the-congo-kinshasadenmarkdjiboutidodomadominicadominican-republicdr-congodubaieast-timor-timor-lesteecuadoregyptegyptyel-salvadorenglandequatorial-guineaequitorial-guineaeritreaestoniaeswatiniethiopiafalkland-islandsfaroe-islandsfederal-states-of-moldovafijifinlandFloridafrancefrench-guianafrench-polynesiafrench-southern-territoriesgabongazageorgiagermanyghanagibraltargomaGreecegreenlandgrenadaguadeloupeguamguatemalaguineaguinea-bissauguyanahabarihaitiholy-seehondurashong-konghoustonhungaryicelandindiaindonesiaIowairaniran-islamic-republic-ofiraqirelandisraelitaliaitalyivory-coastjamaicajapanjordankaratukazakhstankilimanjarokinshasakiribatikiswahilikoreakosovokuwaitkyrgyzstanlaolatvia-lebanon-lesotho-liberia-libya-liechtenstein-lithuania-luxembourgLebanonliberiamacaumadagascarmalawimalaysia-maldivesMalimaltamarshall-islands-martinique-mauritania-mauritiusmassechutesmayottemazingirambeyamerumexicomiamimicronesiamonaco-mongolia-montenegromontserratmoroccomozambique-myanmarmtwaramwanzanamibianaurunepalnetherlandsnetherlands-antillesnevadanew-caledonianew-zealandnewyorknicaraguanigernigerianiuenorth-macedonianorthern-mariana-islandsnorwayomanpakistanpalaupalestinepalestinian-territoriespanamapapua-new-guineaparaguaypeoples-democratic-republicperuphiladhephiaphilipiansPhilippinespitcairn-islandpolandpoliticsPortugalpuerto-ricoqatarrepublic-ofrepublic-of-brazzavillerepublic-of-south-koreareunion-islandromaniaRussiarussian-federationrwandasahara-occidentalsaint-kitts-and-nevissaint-luciasaint-vincent-and-the-grenadinessamoasan-marinosao-tome-and-principesaudi-arabiasaudiarabiascotlandSenegalserbiaseychellessierra-leoneSingaporesingidaslovakia-slovak-republicsloveniasolomon-islandssomaliasouthafricaspainsri-lankasudansurinameswaziland-eswatiniswedenswitzerlandsyriasyrian-arab-republictaborataiwan-republic-of-chinatajikistantanzaniatexasthailandthe-gambiatibettimor-leste-east-timortogotokelautongatorontotrinidad-and-tobagotunisiaturkeyturkmenistanturks-and-caicos-islandstuvaluugandaunited-arabs-emiratesunited-kingdomunited-statesuruguayuzbekistanvancovervanuatuvatican-city-state-holy-seevenezuelavietnamvirgin-islands-britishvirgin-islands-u-swallis-and-futuna-islandswallis-and-futuna-islandswallis-et-futunawashington-dcwestern-saharayemenzambiazambiezimbabwe

CantonaDigital
CantonaDigital

Listen Live Radio Fortune Africa
Ukweli Na Burudani.

-Be ready to be Impacted, Inspired & Empowered.

-Keep watching our Channels

Cantona Cast Television,

Fortune Television Network (FTN)

Donation
Paypal https://www.paypal.com/donate/?hosted_button_id=6EKXMLNW8W6A2&fbclid=IwY2xjawQxeChleHRuA2FlbQIxMABicmlkETFRdkNBRndpclRDQTB5bXZZc3J0YwZhcHBfaWQQMjIyMDM5MTc4ODIwMDg5MgABHq960uGsyU3ABRIBc2h-iXGhHATvuEqe55gFsQ-rDb0fT-Z7SIQ3TV8LnkpD_aem_ybU2SvBlvyqrVsS9NAczRw

An attitude determines an altitude.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2025

5,550 posts
0 followers

Fediverse Followers


Discover more from Cantona.Digital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a Reply

About us

Welcome to Cantona Group PLC-Where media meets moments.

Cantona Group PLC is a Premier Multi Media Group, where we connect live Broadcasting with world-class Production. We break the latest news in real-time, shape public perception, and produce captivating audio-visual content all under one roof.

Discover more from Cantona.Digital

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading

Discover more from Cantona.Digital

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading