
Kiongozi wa upinzani nchini Uganda, Kizza Besigye, anatarajiwa kufikishwa mahakamani leo mjini Kampala kuanza kusikilizwa kwa kesi ya uhaini inayomkabili.
Besigye na msaidizi wake, Obeid Lutale, wanakabiliwa na mashtaka ya kupanga njama za kuipindua serikali ya Uganda.
Besigye alikamatwa mjini Nairobi mnamo Novemba 2024 na kurejeshwa kwa nguvu nchini Uganda, ambako amekuwa akizuiliwa tangu wakati huo.
Kesi hiyo inaanza kusikilizwa leo baada ya kuahirishwa mara kadhaa hapo awali.
Besigye, aliyekuwa daktari wa binafsi wa Rais Yoweri Museveni, mwaka jana hali ya afya yake ilidhoofika na kukimbizwa hospitalini kabla ya kurejeshwa gerezani.
Katika uamuzi wa kihistoria mwaka jana, Mahakama ya Juu ya Uganda ilitangaza kuwa ni kinyume cha katiba kwa mahakama za kijeshi kuwahukumu raia, na kuamuru kesi zote hizo kuhamishiwa katika mahakama za kiraia.
Uamuzi huo ulimkasirisha Rais Museveni, ambaye alipuuzilia mbali na kuutaja kuwa “uamuzi usio sahihi” na kuapa kuupinga.
Raia wengi wa Uganda ikiwemo mpinzani mwenza Bobi Wine aliandika kwa mtandao wa kijamii kushurutisha Besigye aachiliwe huru na aruhusiwe kupata huduma za matibabu.
Hofu ya ghasia huku Afrika Kusini ikiimarisha ulinzi kabla ya maandamano dhidi ya wahamiaji

Vyombo vya usalama vimeimarishwa kote nchini Afrika Kusini kutokana na hofu kwamba maandamano dhidi ya wahamiaji yanaweza kugeuka na kuwa ya vurugu, huku Rais Cyril Ramaphosa akiwataka watakaoshiriki kufanya hivyo bila “vitisho au kutoa masharti.”
Maandamano hayo yanafanyika baada ya wanaharakati kuweka tarehe ya mwisho isiyo rasmi ya kuwataka wageni wote wasio na nyaraka halali kuondoka nchini.
Wengi wao tayari wameondoka ili kuepuka vitisho na ghasia. Polisi wa Afrika Kusini wanasema watu 25,000 wamekwisharejeshwa katika nchi zao, wengi wao wakitoka mataifa mengine ya Afrika.
Mhamiaji mmoja kutoka Malawi asiye na nyaraka halali ameiambia BBC kuwa ana furaha kurejea nyumbani, lakini amevunjika moyo kwa kuacha nyuma watoto wake wanne wadogo.
Johannesburg, ambako moja ya maandamano hayo yanatarajiwa kufanyika, imeonekana kuwa tulivu isivyo kawaida, huku maduka yote karibu na eneo la mkusanyiko wa waandamanaji yakiwa yamefungwa.
Rais Ramaphosa amesisitiza mara kadhaa kuwa maandamano yafanyike kwa amani na uwajibikaji, huku pia akitambua haja ya kufanya mageuzi ya sera za uhamiaji.
Aliwakumbusha wananchi kuwa baadhi ya raia wa kigeni wanaishi Afrika Kusini kihalali.
“Wanafanya kazi, wanasoma, wanalea familia, wanawekeza katika uchumi wetu na wanachangia kwa njia chanya katika jamii yetu. Nao pia wana haki ya kulindwa na sheria na Katiba yetu.”
Aliongeza kuwa:
“Haki ya kuandamana na uhuru wa kujieleza havitoi ruhusa ya kutishia au kuwahofisha wengine, wala kushiriki vitendo vya uharibifu au vurugu.”
Kwa mujibu wa takwimu rasmi, kuna zaidi ya wahamiaji milioni tatu wenye nyaraka halali nchini Afrika Kusini.
Kabla ya kufika kwa muda huo wa mwisho, maelfu ya wahamiaji wamekuwa wakisubiri kushughulikiwa katika kambi za muda kwa wiki kadhaa kutokana na hofu ya usalama wao.
Huko Durban, ambako baadhi ya maandamano makubwa zaidi yamefanyika, mahema meupe yanayowahifadhi zaidi raia wa Malawi yameanza kubomolewa huku mamlaka zikikimbizana kuondoa kambi hiyo ya mpito.
Mwanamume mmoja kutoka Malawi, Hassan Phiri, alitoa ujumbe kwa waandamanaji:
“Ninachotaka kuwaambia Waafrika Kusini ni kwamba sisi sote ni kitu kimoja. Afrika haiwezi kuwa Afrika bila Afrika Kusini, bila Malawi na bila mataifa mengine. Lazima tupendane na tushikamane kama Waafrika.”
JangaJamhuri ya Kidemokrasia ya Congo
Mgonjwa wa kwanza wa Ebola apona mjini Beni

Mwili unapelekwa katika chumba cha kuhifadhi maiti katika kituo cha matibabu cha NyankundePicha: Anadolu Agency/IMAGO
Mji wa Beni, ulioko mashariki mwa Kongo, umepiga hatua hatua muhimu katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa Ebola baada ya Charline Kavira Mukelu kuwa mgonjwa wa kwanza kuthibitishwa kupona ugonjwa huo.
Kupona kwa mgonjwa huyo kunatajwa kuwa ishara ya matumaini kwa wakaazi wa eneo hilo, ambao kwa miaka mingi wameathiriwa na milipuko ya mara kwa mara ya Ebola pamoja na changamoto za kiusalama zinazoathiri utoaji wa huduma za afya.
Serikali ya Kongo, kwa ushirikiano na wadau wa kimataifa, inatarajia kufungua kituo kipya cha matibabu ya Ebola katika mji wa Beni.
Kituo hicho kinatarajiwa kuongeza uwezo wa kupokea wagonjwa, kuboresha huduma za matibabu, na kuimarisha ufuatiliaji wa maambukizi katika mikoa iliyo hatarini.
Mji wa Beni umewahi kuwa kitovu cha mlipuko mkubwa wa Ebola kati ya mwaka 2018 hadi 2020, mlipuko uliosababisha maelfu ya maambukizi na kuacha athari kubwa za kiafya, kijamii na kiuchumi. Changamoto za kiusalama, uhamaji wa watu, na udhaifu wa miundombinu ya afya zilichangia kuongezeka kwa kasi ya maambukizi katika kipindi hicho.
Mlipuko wa sasa unatofautiana na ile ya miaka ya nyuma kwa sababu unasababishwa na kirusi cha Bundibugyo, ambacho ni nadra ikilinganishwa na kirusi cha Zaire kinachojitokeza mara nyingi zaidi.
Tofauti hii imeleta changamoto katika utambuzi wa ugonjwa huo, kwani kwa wiki kadhaa maambukizi yalikuwa hayagunduliki kwa usahihi kutokana na vipimo vilivyoelekezwa zaidi kwenye kirusi cha Zaire.
Migogoro Iran
Iran yapinga uwepo wa vikosi vya kimataifa Hormuz

Meli ya mizigo ikipita katika mlango bahari wa HormuzPicha: Anadolu/picture alliance
Iran imepinga vikali pendekezo la Macron la kuhusisha vikosi vya kimataifa katika operesheni ya kuondoa mabomu ya baharini katika Mlango Bahari wa Hormuz, eneo muhimu linalounganisha Ghuba ya Uajemi na Bahari ya Oman.
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Kazem Gharibabadi amesisitiza kuwa ushiriki wa vikosi vya kimataifa katika operesheni hiyo ungekiuka makubaliano yaliyopo, ambayo yanaeleza wazi kuwa jukumu la kuondoa mabomu baharini ni la Iran pekee.
Mwanadiplomasia huyo pia ameishtumu Ufaransa kwa kuchochea taharuki zaidi katika mlango Bahari wa Hormuz wenye umuhimu mkubwa kimkakati katika eneo la Ghuba ya Uajemi.
Gharibabadi ameonya kuwa kuingilia majukumu ya Iran kutavuruga utaratibu wa usalama uliokubalika na kuongeza hatari ya mivutano ya kijeshi.
Rais Macron alizungumzia suala hilo wakati wa ziara ya Sultan Haitham bin Tarik wa Oman mjini Paris, ambako mazungumzo yao yalijikita katika hali ya usalama wa baharini na umuhimu wa kulinda uhuru wa meli kupita katika njia za kimataifa.
Ikulu ya Élysée pia ilitoa taarifa ya pamoja ikisema viongozi wa Ufaransa na Oman walisisitiza umuhimu wa kufunguliwa tena ujia huo muhimu na kuthibitisha dhamira yao ya kuhakikisha uhuru wa usafiri wa majini bila masharti wala vikwazo, ikiwemo haki ya meli kupita kwa mujibu wa sheria za kimataifa za bahari.
Uhalifu Ulaya
Watu watano wauawa kwa kupigwa risasi mjini Stade, Ujerumani

Picha: Ulrich Perrey/dpa/picture alliance
Watu watano wameuawa kwa kupigwa risasi katika kituo cha vijana nchini Ujerumani.
Polisi imesema washukiwa wa tukio hilo tayari wamekamatwa huku ikilielezea tukio hilo kama moja ya mashambulizi mabaya zaidi ya risasi kuwahi kutokea katika miaka ya hivi karibuni.
Polisi waliovalia vesti za kuzuwia risasi walionekana katika eneo la tukio lililofungwa Kaskazini mwa mji wa Stade Magharibi mwa mji wa Hamburg. Magari ya kubebea wagonjwa pia yalionekana huko.
Polisi imesema mauaji hayo yametokea katika eneo ambalo ni makaazi ya makundi ya kina mama na watoto.
Kulingana na gazeti la Der Spigel la Ujerumani Washukiwa wote wawili waliokamatwa wana zaidi ya miaka 21.
Michezo
Merz aitia moyo Ujerumani licha ya kutolewa Kombe la Dunia

Wachezaji wa Ujerumani wakionekana kuvunjika moyo baada ya timu hiyo kutolewa na Paraguay kwa njia ya penaltiPicha: Peter Cziborra/REUTERS
Kansela wa Ujerumani Friedrich Merz ametuma ujumbe wa kutia moyo kwa wachezaji wa timu ya taifa ya Ujerumani baada ya kuondolewa mapema kwa mara ya tatu mfululizo katika michuano ya Kombe la Dunia.
Kupitia ujumbe aliouandika kwenye mtandao wa kijamii wa X, Merz amesisitiza kuwa ingawa matokeo hayo yanaumiza, mechi dhidi ya Paraguay ilikuwa ya kuvutia na taifa bado linajivunia juhudi za timu.
Die Mannschaft iliondolewa kwenye mashindano hayo baada ya kufungwa 4–3 kwa mikwaju ya penalti kufuatia sare ya 1–1 katika muda wa kawaida.
Licha ya kuondolewa, Ujerumani ilifanikiwa kufika hatua ya mtoano kwa mara ya kwanza tangu ilipotwaa ubingwa wa Kombe la Dunia mwaka 2014.
Katika mashindano ya mwaka 2018 na 2022, timu hiyo ilishindwa kuvuka hatua ya makundi, jambo lililoibua mjadala mpana kuhusu mustakabali wa soka la taifa hilo.
Paraguay ilitangulia kupata bao kunako dakika ya 42 kupitia Julio Enciso. Hata hivyo baada ya mapumziko, Ujerumani Die Mannschaft ilisawazisha kupitia Kai Havertz dakika ya 54 ya mchezo baada ya kupokea krosi safi kutoka kwa Florian Wirtz.
Pamoja na mashambulizi mengi ya Ujerumani katika kipindi cha pili na muda wa nyongeza, walishindwa kupata bao la ushindi kutokana na uimara wa Paraguay na ubora wa kipa Orlando Gill.
Dakika za nyongeza zilikuwa na patashika baada ya Jonathan Tah kufunga bao ambalo lingeipa Ujerumani ushindi, lakini mwamuzi alilifuta kufuatia mapitio ya VAR yaliyobaini kulikuwepo na madhambi kabla ya Jonathan Zah kuutia mpira kambani.
Katika mikwaju ya penalti, Ujerumani ilikumbwa na presha kubwa huku Kai Havertz, Nick Woltemade na Jonathan Tah wakishindwa kufunga mikwaju yao. Kipa wa Paraguay, Orlando Gill, aliibuka shujaa kwa kuokoa penalti muhimu, kabla ya José Canale kufunga mkwaju wa ushindi na kuipeleka Paraguay hatua inayofuata ya mashindano.
afghanistan, africa, albania, algeria, America, american-samoa, andorra, angola, anguilla, antarctica, antigua-and-barbuda, argentina, armenia, aruba, arusha, australia, austria, azerbaijan, bahamas, bahrain, bangladesh, barbados, belarus, Belgium, belize, benin, bermuda, bhutan, bolivia, bosnia-and-herzegovina, botswana, Boukinafaso, brazil, brunei-darussalam, bulgaria, burkina-faso, burma, burundi, california, cambodia, cameroon, canada, cape-verde, cayman-islands, central-african-republic, Chad, chicago, chile, china, christmas-island, cocos-keeling-islands, colombia, comoros, congo, cook-islands, costa-rica, cote-divoire-ivory-coast, Croatia, cuba, cyprus, czech-republic, darsalaam, democratic-peoples-rep-north-korea, democratic-republic-of-the-congo-kinshasa, denmark, djibouti, dodoma, dominica, dominican-republic, dr-congo, dubai, east-timor-timor-leste, ecuador, egypt, egypty, el-salvador, england, equatorial-guinea, equitorial-guinea, eritrea, estonia, eswatini, ethiopia, falkland-islands, faroe-islands, federal-states-of-moldova, fiji, finland, Florida, france, french-guiana, french-polynesia, french-southern-territories, gabon, gaza, georgia, germany, ghana, gibraltar, goma, Greece, greenland, grenada, guadeloupe, guam, guatemala, guinea, guinea-bissau, guyana, habari, haiti, holy-see, honduras, hong-kong, houston, hungary, iceland, india, indonesia, Iowa, iran, iran-islamic-republic-of, iraq, ireland, israel, italia, italy, ivory-coast, jamaica, japan, jordan, karatu, kazakhstan, kilimanjaro, kinshasa, kiribati, kiswahili, korea, kosovo, kuwait, kyrgyzstan, lao, latvia-lebanon-lesotho-liberia-libya-liechtenstein-lithuania-luxembourg, Lebanon, liberia, macau, madagascar, malawi, malaysia-maldives, Mali, malta, marshall-islands-martinique-mauritania-mauritius, massechutes, mayotte, mazingira, mbeya, meru, mexico, miami, micronesia, monaco-mongolia-montenegro, montserrat, morocco, mozambique-myanmar, mtwara, mwanza, namibia, nauru, nepal, netherlands, netherlands-antilles, nevada, new-caledonia, new-zealand, newyork, nicaragua, niger, nigeria, niue, north-macedonia, northern-mariana-islands, norway, oman, pakistan, palau, palestine, palestinian-territories, panama, papua-new-guinea, paraguay, peoples-democratic-republic, peru, philadhephia, philipians, Philippines, pitcairn-island, poland, politics, Portugal, puerto-rico, qatar, republic-of, republic-of-brazzaville, republic-of-south-korea, reunion-island, romania, Russia, russian-federation, rwanda, sahara-occidental, saint-kitts-and-nevis, saint-lucia, saint-vincent-and-the-grenadines, samoa, san-marino, sao-tome-and-principe, saudi-arabia, saudiarabia, scotland, Senegal, serbia, seychelles, sierra-leone, Singapore, singida, slovakia-slovak-republic, slovenia, solomon-islands, somalia, southafrica, spain, sri-lanka, sudan, suriname, swaziland-eswatini, sweden, switzerland, syria, syrian-arab-republic, tabora, taiwan-republic-of-china, tajikistan, tanzania, texas, thailand, the-gambia, tibet, timor-leste-east-timor, togo, tokelau, tonga, toronto, trinidad-and-tobago, tunisia, turkey, turkmenistan, turks-and-caicos-islands, tuvalu, uganda, united-arabs-emirates, united-kingdom, united-states, uruguay, uzbekistan, vancover, vanuatu, vatican-city-state-holy-see, venezuela, vietnam, virgin-islands-british, virgin-islands-u-s, wallis-and-futuna-islands, wallis-and-futuna-islands, wallis-et-futuna, washington-dc, western-sahara, yemen, zambia, zambie, zimbabwe

Leave a Reply