Na Cantona Joseph June 26, 2026 06:15 (EAT)

Umoja wa Ulaya (EU), umeweka vikwazo vya muda vinavyowazuia raia wa Somalia kupata viza ya Schengen, baada ya nchi hiyo kushindwa kutoa ushirikiano wa kuwarejesha nyumbani raia wake wanaoishi katika nchi wanachama wa umoja huo kinyume cha sheria.
Chini ya hatua hizo mpya, raia wa Somalia hawatastahiki tena viza ya Schengen, ambayo inawawezesha wamiliki kuzuru eneo la Schengen hadi muda wa viza utakapokamilika.
EU pia imeongeza muda wa kushughulikia maombi ya viza kwa raia wa Somalia kutoka siku 15 hadi siku 45.
Hatua hiyo mpya itawaathiri raia wa Somalia wanaotaka kuenda Ulaya kwa shughuli za kikazi, masomo, ziara za familia au utalii.
Umoja wa Ulaya pia umesitisha taratibu zilizorahisishwa za kuunga mkono hati zinazohitajika kwa ajili ya maombi ya viza, na imerejesha ada za viza kwa wenye hati za kusafiria za kidiplomasia na huduma nchini Somalia.
Marekani yadai meli mafuta ya Singapore ilishambuliwa na Iran

Maafisa wa Marekani ambao majina yao hayakutangazwa hadharani wameviambia vyombo vya habari vya Marekani kwamba shambulio la Alhamisi dhidi meli ya mafuta karibu na Mlango-Bahari wa Hormuz lilitekelezwa na Jeshi la Wanamaji la Walinzi wa Mapinduzi ya Iran IRGC.
Iran haijatoa tamko lolote kuhusiana na madai haya, lakini jeshi la majini la IRGC lilionya Jumatano usiku kwamba meli yoyote itakayopitia Mlango-Bahari wa Hormuz lazima ishirikiane na vikosi vya Irani.
Siku ya Alhamisi Mamlaka mpya ya Usimamizi ya Mlango Bahari wa Hormuz ilionya kwamba “haiwezi kuzihakikishia uslama meli zinazotumia njia ambazo hazijaidhinishwa”.
Mashirika ya habari ya Iran yaliandika siku ya Alhamisi usiku: “Kujibu maswali yanayoulizwa mara kwa mara, Mamlaka ya Njia ya Majini katika Ghuba ya Uajemi (PGSA) imetangaza kwamba meli zozote zinazopita nje ya mfumo uliowekwa na mamlaka hii haitapewa dhamana ya usalama na hazitapewa bima na majukumu yanayohusiana nayo.
Tangazo la shirika hilo pia lilisisitiza kuwa: “Hasara itakayotokana na usafiri kupitia njia zisizo rasmi itasimamiwa na mmiliki, mwendeshaji, na nahodha wa chombo.”
Onyo la IRGC Jumatano usiku lilikuja baada ya Oman kutangaza, wakati wa ziara ya wziri wa mambo ya nje wa Marekani Marco Rubio katika nchi kadhaa za Ghuba, kwamba ilikuwa imeunda njia mpya ya baharini ili kurahisisha meli kupita kwenye Mlango -Bahari wa Hormuz.
Taarifa hizo ziliungwa mkono na Bahrain, lakini huenda Jeshi la majini la IRGC “lilikerwa” na hatua kwa kuundwa kwa njia hiyo.
Hata hivyo Iran bado haijakubali rasmi au kukana kuhusika na shambulio dhidi ya meli hiyo ya Singapore.
Mfalme Charles afichua kodi aliyolipa mwaka 2024-25

Mfalme Charles amekuwa mfalme wa kwanza wa Uingereza kuweka adharani malipo ya kodi yake.
Mfalme Charles alilipa dola milioni 17 kutokana na mapato yake binafsi katika mwaka wa kodi ulioishia Machi, 2025.
Mfalme Charles amelipa takriban dola milioni arobaini kama kodi tangu alipokuwa Mfalme mnamo mwaka wa 2022.
Mwanafalme William, pia ameweka wazi maelezo yake ya kodi, William alilipa dola milioni 10 katika mwaka uliopita wa kodi.
Kando na hayo, imebainika kuwa Mfalme Charles na Malkia Camilla hawaishi tena katika Ikulu ya Buckingham Palace licha ya jengo hilo kufanyiwa ukarabati ambao tayari umegharimu dola za Marekani milioni 430 itakapokamilika mwaka ujao.
Badala yake, watasaliai katika jumba jirani la Clarence.
Wataendelea kutumia Kasri la Buckingham shughuli za kiserikali.
Tetemeko la ardhi Venezuela: Waokoaji mbioni kuwatafuta manusura, idadi ya waliofariki ikifikia 235

Waokoaji wanapekua vifusi watafuta walionusurika matetemeko mawili makubwa ya ardhi yaliyokumba maeneo ya karibu na mji mkuu wa Venezuela na kusababisha vifo vya takribani watu 235 na kuwajeruhi zaidi ya 1,500.
Katika Caracas na mji wa karibu wa pwani wa La Guaira, watu walisikika wakiomba msaada kutoka chini ya vifusi vya majengo yaliyoporomoka.
Tetemeko la kwanza la ukubwa wa 7.2 lilifuatiwa sekunde chache baadaye na lingine lenye nguvu zaidi ya 7.5, kulingana na Utafiti wa Jiolojia wa Marekani (USGS), na kusababisha uharibifu mkubwa zaidi.
Watu wengi zaidi wanahofiwa kufariki, huku wengine wakiwa wameachwa bila makao au kulala barabarani kwa kuogopa kurejea kwenye majengo yaliyoharibiwa baada ya mkasa huo.
Matetemeko ya ardhi yalitokea saa kumi na mbili na dakika ne kwa saa za ndani(22:04 GMT) siku ya Jumatano – sikukuu ya kitaifa nchini Venezuela, kumaanisha kuwa watu walikuwa nyumbani ikilinganishwa na siku ya kawaida ya juma.
Siku ya Alhamisi Rais wa Bunge la Venezuela Jorge Rodríguez, aliripoti kwamba idadi ya waliofariki imeongezeka, baada ya Rais wa mpito wa nchi hiyo Delcy Rodríguez kutangaza hali ya dharura.
Nchi kadhaa zimeahidi kusaidia juhudi za uokoaji, huku Marekani ikiahidi msaada wa dola milioni 150. Jeshi la Marekani linatuma meli za usafiri na ndege kusaidia shughuli ya uokoaji na “operesheni za msaada wadharura”, ilisema katika taarifa.
Jorge Rodríguez alisema majengo 250 yameharibiwa au kupotea, hasa La Guaira, ambapo BBC ilithibitisha picha za hoteli ya ghorofa 10 iliyoharibiwa na kuwa vifusi. Siku ya Alhamisi, watu walikuwa wakitafuta wapendwa huko.
Juan Ortiz ameiambia BBC kwamba mmoja wa marafiki zake wa karibu amethibitishwa kufariki, mwingine anaaminika kuwa chini ya vifusi, na takribani watu 20 anaowafahamu wanaoishi katika eneo la pwani hawajulikani waliko.
“Ninakabiliwa na mshtuko na kuchanganyikiwa, nasikitika kwamba siwezi kusaidia,” mwanafunzi wa matibabu mjini Caracas alisema.
Kombe la Dunia 2026: Ivory Coast yafuzu raundi ya pili baada ya kuilaza Curacao

Ivory Coast imefuzu kwa hatua ya muondoano kwa mara ya kwanza katika historia ya Kombe la Dunia baada ya Nicolas Pepe kufunga mabao mawili na kuwaondoa Curacao.
Wenyeji Ivory Coast walihitaji alama moja tu ili kufika hatua ya 32, baada ya kutoka katika hatua ya makundi katika mechi zao tatu zilizopita za Kombe la Dunia.
Na walionyesha ujasiri wao kwa bao baada ya dakika saba tu mabeki wa Curacao walishikwa wavuni na kuondolewa na Yan Diomande, ambaye alimuandalia mpira safi Pepe.
Katika dakika ya 65, mshambuliaji wa zamani wa Arsenal Pepe – ambaye aliachwa nje ya kikosi cha Ivory Coast kwa ajili ya Kombe la Mataifa ya Afrika mapema mwaka huu – alipata la pili alipopachika wavuni kwa mguu wa kushoto na kumpita kipa wa Curacao, Eloy Room.
Hii inamaanisha kuwa Ivory Coast inamaliza nafasi ya pili katika Kundi E ikiwa na alama sita, ikishinda mechi mbili za Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza.
afghanistan, africa, albania, algeria, America, american-samoa, andorra, angola, anguilla, antarctica, antigua-and-barbuda, argentina, armenia, aruba, arusha, australia, austria, azerbaijan, bahamas, bahrain, bangladesh, barbados, belarus, Belgium, belize, benin, bermuda, bhutan, bolivia, bosnia-and-herzegovina, botswana, Boukinafaso, brazil, brunei-darussalam, bulgaria, burkina-faso, burma, burundi, california, cambodia, cameroon, canada, cape-verde, cayman-islands, central-african-republic, Chad, chicago, chile, china, christmas-island, cocos-keeling-islands, colombia, comoros, congo, cook-islands, costa-rica, cote-divoire-ivory-coast, Croatia, cuba, cyprus, czech-republic, darsalaam, democratic-peoples-rep-north-korea, democratic-republic-of-the-congo-kinshasa, denmark, djibouti, dodoma, dominica, dominican-republic, dr-congo, dubai, east-timor-timor-leste, ecuador, egypt, egypty, el-salvador, england, equatorial-guinea, equitorial-guinea, eritrea, estonia, eswatini, ethiopia, falkland-islands, faroe-islands, federal-states-of-moldova, fiji, finland, Florida, france, french-guiana, french-polynesia, french-southern-territories, gabon, gaza, georgia, germany, ghana, gibraltar, goma, Greece, greenland, grenada, guadeloupe, guam, guatemala, guinea, guinea-bissau, guyana, habari, haiti, holy-see, honduras, hong-kong, houston, hungary, iceland, india, indonesia, Iowa, iran, iran-islamic-republic-of, iraq, ireland, israel, italia, italy, ivory-coast, jamaica, japan, jordan, karatu, kazakhstan, kilimanjaro, kinshasa, kiribati, kiswahili, korea, kosovo, kuwait, kyrgyzstan, lao, latvia-lebanon-lesotho-liberia-libya-liechtenstein-lithuania-luxembourg, Lebanon, liberia, macau, madagascar, malawi, malaysia-maldives, Mali, malta, marshall-islands-martinique-mauritania-mauritius, massechutes, mayotte, mazingira, mbeya, meru, mexico, miami, micronesia, monaco-mongolia-montenegro, montserrat, morocco, mozambique-myanmar, mtwara, mwanza, namibia, nauru, nepal, netherlands, netherlands-antilles, nevada, new-caledonia, new-zealand, newyork, nicaragua, niger, nigeria, niue, north-macedonia, northern-mariana-islands, norway, oman, pakistan, palau, palestine, palestinian-territories, panama, papua-new-guinea, paraguay, peoples-democratic-republic, peru, philadhephia, philipians, Philippines, pitcairn-island, poland, politics, Portugal, puerto-rico, qatar, republic-of, republic-of-brazzaville, republic-of-south-korea, reunion-island, romania, Russia, russian-federation, rwanda, sahara-occidental, saint-kitts-and-nevis, saint-lucia, saint-vincent-and-the-grenadines, samoa, san-marino, sao-tome-and-principe, saudi-arabia, saudiarabia, scotland, Senegal, serbia, seychelles, sierra-leone, Singapore, singida, slovakia-slovak-republic, slovenia, solomon-islands, somalia, southafrica, spain, sri-lanka, sudan, suriname, swaziland-eswatini, sweden, switzerland, syria, syrian-arab-republic, tabora, taiwan-republic-of-china, tajikistan, tanzania, texas, thailand, the-gambia, tibet, timor-leste-east-timor, togo, tokelau, tonga, toronto, trinidad-and-tobago, tunisia, turkey, turkmenistan, turks-and-caicos-islands, tuvalu, uganda, united-arabs-emirates, united-kingdom, united-states, uruguay, uzbekistan, vancover, vanuatu, vatican-city-state-holy-see, venezuela, vietnam, virgin-islands-british, virgin-islands-u-s, wallis-and-futuna-islands, wallis-and-futuna-islands, wallis-et-futuna, washington-dc, western-sahara, yemen, zambia, zambie, zimbabwe
Leave a Reply