
Kiongozi wa kundi la Hezbollah, Naim Qassem, amesema Israel haina njia nyingine isipokuwa kuondoka kikamilifu katika kila sehemu ya ardhi ya Lebanon, akisisitiza kuwa hakuna masharti yanayopaswa kuambatanishwa na hatua hiyo.
Katika hotuba yake ya televisheni wakati wa maadhimisho ya Ashura, Qassem alisema Lebanon haitakubali uhusiano wa kawaida na Israel wala hatua zozote ambazo zinaweza kuhalalisha uwepo wake katika ardhi ya Lebanon.
“Israel haina chaguo jingine isipokuwa kuondoka kabisa kutoka kwa kila ardhi ya Lebanon,” alisema.
Aliongeza kuwa kundi lake halitakubali “kurekebishwa kwa uhusiano, kusitishwa kwa uhasama, faida yoyote kwa Israel, wala uwepo wa sehemu yoyote ya Israel katika ardhi ya Lebanon.”
Kauli hiyo inakuja wakati maafisa wa Lebanon na Israel wakiendelea na mazungumzo ya moja kwa moja Washington, hatua ambayo imezua mjadala mpana kuhusu mustakabali wa mahusiano ya mataifa hayo mawili.
Lebanon na Israel bado zipo katika mvutano wa muda mrefu, huku Hezbollah ikiwa na uhusiano wa karibu na Iran ambayo imekuwa ikisema inazingatia maslahi ya kundi hilo katika mazungumzo yake na Marekani.
Hasira Kenya baada ya video kuonesha polisi wakimkamata kwa nguvu mwanamume mwenye ulemavu

Wakenya wameeleza kutoridhishwa na kukasirishwa baada ya video kusambaa ikionyesha maafisa wa polisi wakimkamata kwa nguvu mwanamume mwenye ulemavu wakati wa maandamano ya kupinga serikali mjini Nakuru, yaliyofanyika jana Alhamisi.
Huduma ya Kitaifa ya Polisi ya Kenya imekosolewa vikali baada ya tukio hilo linalomhusisha James Thuku, ambaye hutumia magongo kutembea, kuonekana akivutwa na kuangushwa chini kabla ya kuingizwa kwenye gari la polisi.
Kwa mujibu wa taarifa ya Seneta Crystal Asige, Thuku alikamatwa na anashikiliwa katika Kituo Kikuu cha Polisi Nakuru kwa tuhuma za kuchochea vurugu.
“Nimeweza kuthibitisha kwamba alikamatwa na anashikiliwa katika Kituo Kikuu cha Polisi Nakuru. Jina lake ni James Thuku. Mashtaka: kuchochea vurugu,” Seneta Crystal Asige aliandika kwenye mtandao wa X.
Seneta huyo ameitaka mamlaka ya polisi kutoa maelezo kuhusu mazingira ya kukamatwa kwake.
Video hiyo iliyosambaa mitandaoni inaonyesha Thuku akijaribu kuvuka barabara akiwa ameandamana na mtu mwingine wakati wa maandamano. Gari la polisi aina ya Land Cruiser kisha linafika eneo hilo likiwa na maafisa zaidi ya kumi waliokuwa na silaha na vifaa vya kudhibiti vurugu.
Baada ya maafisa hao kushuka, mtu aliyekuwa akimsaidia Thuku anakimbia, na kumwacha akiwa peke yake. Thuku anaanguka chini wakati akijaribu kukwepa kukamatwa kabla ya kuburutwa na maafisa hao na kisha kuwekwa ndani ya gari la polisi.
Tukio hilo limeibua ukosoaji mkali kutoka kwa wananchi na watumiaji wa mitandao ya kijamii, wengi wakilaani matumizi ya nguvu dhidi ya mtu mwenye ulemavu.
Wadau wa haki za binadamu wametoa wito wa uchunguzi huru kubaini iwapo taratibu za polisi zilizingatiwa na kama nguvu iliyotumika ilikuwa ya lazima katika tukio hilo.

India yataka masharti bora ya ushuru kabla ya mkataba wa biashara na Marekani

Kwa mujibu wa BBC Monitoring, Waziri wa Biashara wa India, Piyush Goyal, amesema New Delhi haitasaini mkataba wa biashara wa pande mbili na Washington hadi kuwe na mfumo utakaohakikisha bidhaa za India zinapata ushindani wa juu zaidi katika ushuru wa forodha.
Akizungumza katika hafla moja jijini London, Goyal alisema, “Lengo kuu la mkataba wa biashara huria ni kukupa faida dhidi ya washindani wako.”
Akirejelea makubaliano ya muda ya biashara yaliyotangazwa kati ya India na Marekani mwezi Februari, alisema: “Bila shaka tunahitaji sababu thabiti ya kutekeleza makubaliano ambayo tayari yamefikiwa.”
Goyal alisema chini ya makubaliano hayo yanayopendekezwa, Marekani italazimika kuipa India masharti ya kibiashara yaliyo bora zaidi kuliko yale yanayotolewa kwa nchi kama Vietnam, Thailand, Philippines, Indonesia, Malaysia, China, Bangladesh na Sri Lanka.
Kauli zake zinakuja wakati India na Marekani zikifanya tathmini ya maendeleo ya makubaliano ya muda ya biashara yanayojumuisha masuala ya upatikanaji wa masoko, biashara ya kidijitali na minyororo ya ugavi.
Nchi hizo mbili zinafanya jitihada za kukamilisha makubaliano hayo kabla ya Julai 24, tarehe ambayo ushuru wa muda wa asilimia 10 uliowekwa na Washington unatarajiwa kuondolewa.
Makubaliano ya mpito kati ya Marekani na Iran yataruhusu ukaguzi wa vituo vya nyuklia vya Iran – IAEA

Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA), Rafael Grossi, amesema mfumo “madhubuti” wa uhakiki unahitajika ili kuhakikisha Iran haiwezi kumiliki silaha za nyuklia baada ya vita vya Mashariki ya Kati.
Akizungumza na wanahabari nchini Japan, Grossi amesema anaamini lengo la makubaliano kati ya Marekani na Iran ni kuhakikisha Tehran haielekei katika kutengeneza silaha za nyuklia.
“Serikali ya Iran tayari imeweka wazi kuwa haina nia hiyo,” alisema.
Hata hivyo, alisisitiza kuwa kauli pekee haitoshi.
“Tunahitaji kuanzisha mfumo imara sana wa uhakiki haraka iwezekanavyo,” alisema.
Grossi pia amesema makubaliano ya mpito ya amani kati ya Marekani na Iran yataruhusu wakaguzi wa IAEA kurejea katika vituo vya nyuklia vya Iran.
Kauli hiyo imekuja baada ya Tehran kutangaza kwamba baadhi ya vituo muhimu vya nyuklia vitaendelea kufungwa na wakaguzi hawataruhusiwa hadi pale makubaliano ya mwisho na Marekani yatakapofikiwa na vikwazo vya kiuchumi kuondolewa.
“Kuna makubaliano, na ili yatekelezwe, Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki utahitaji kupata fursa ya kufanya ukaguzi na kufikia vituo husika. Tunatumaini tutaweza kufanya hivyo hivi karibuni,” Grossi alisema katika mkutano na waandishi wa habari nchini Japan.
Hakukuwa na majibu ya haraka kutoka Iran. Hata hivyo, Tehran tayari imesema kurejea kwa wakaguzi wa nyuklia wa IAEA kutakuwa sehemu ya mazungumzo yanayoendelea kati yake na Marekani na pia sehemu ya makubaliano ya mwisho yanayoweza kufikiwa.
Kwa mujibu wa makubaliano ya awali yaliyofikiwa kati ya Iran na Marekani ili kumaliza vita, inatarajiwa kuwa nchi hizo mbili zitafikia makubaliano ya mwisho baada ya miezi miwili ya mazungumzo.
Unyanyasaji wa kingono wageuka sehemu ya maisha ya kila siku katika baadhi ya maeneo ya Sudan

Tahadhari: Makala haya yana maelezo kuhusu unyanyasaji wa kijinsia ambayo baadhi ya wasomaji wanaweza kuyapata kuwa ya kusikitisha au ya kushtua.
Ubakaji na aina nyingine za unyanyasaji wa kijinsia bado vimeshamiri nchini Sudan, hata katika maeneo ambayo hayajaathiriwa moja kwa moja na vita vya wenyewe kwa wenyewe vinavyoendelea nchini humo, kulingana na ripoti mpya ya shirika la kimatibabu la Médecins Sans Frontières (MSF).
Ingawa ubakaji umeelezwa kuwa “alama rasmi” ya mzozo huo, ripoti hiyo inasema vitendo vingi vya unyanyasaji wa kijinsia vinafanywa na wanaume wenye silaha, mara nyingi vikisindikizwa na ukatili, udhalilishaji na vitendo vya kuwavunjia heshima waathiriwa.
Hata hivyo, MSF imesema ubakaji umeendelea kuwa sehemu “iliyofichika” ya maisha ya kila siku kwa jamii nyingi katika eneo la Darfur Magharibi, hata katika maeneo ambayo kwa sasa hayako mstari wa mbele wa mapigano.
Ripoti hii ndiyo pana zaidi kuwahi kutolewa kuhusu unyanyasaji wa kijinsia katika vita vya Sudan ambavyo sasa vinakaribia kutimiza miaka mitatu.
Ripoti hiyo inategemea ushuhuda wa waathiriwa 3,396 waliotafuta matibabu katika vituo vinavyoungwa mkono na MSF katika maeneo ya Darfur Kaskazini na Darfur Kusini kati ya Januari 2024 na Novemba 2025.
Pande zote mbili zinazohusika katika mzozo huo, yaani jeshi la Sudan na wanamgambo wa Kikosi cha Msaada wa Haraka (RSF), zimekabiliwa na tuhuma za kufanya unyanyasaji wa kijinsia.
Hata hivyo, Darfur inachukuliwa kuwa ngome kuu ya RSF, na waathiriwa wengi waliobainisha waliowadhulumu walisema wahusika walikuwa wapiganaji wa kundi hilo.
Mashambulizi hayo mara nyingi yalihusisha wabakaji zaidi ya mmoja na yaliambatana na aina nyingine za ukatili mkubwa na vitisho, ikiwemo kupigwa na kushuhudia ndugu zao wakitishiwa kuuawa au kuuawa.
“Mara walitupeleka katika eneo la wazi,” anasimulia mwanamke mmoja aliyenukuliwa katika ripoti hiyo. “Mwanaume wa kwanza alinibaka mara mbili, wa pili mara moja, wa tatu mara nne na wa nne mara moja.”
Anaongeza: “Mbali na ubakaji, walitupiga kwa fimbo na kutuelekezea bunduki vichwani. Msichana mwingine mwenye umri wa miaka 15 pia alibakwa na wanaume watatu. Tulibakwa usiku kucha.”
Jiji la Paris ladhibiti unywaji pombe kukabiliana na wimbi la joto Ulaya

Mamlaka ya Ufaransa imepiga marufuku ya unywaji pombe hadharani na mauzo yake mjini Paris, katika jitihada za kupunguza shinikizo kwa hospitali za mji mkuu kipindi hiki cha joto kali.
Wakaazi wa Parisi wamezuiawa kunywa pombe hadharani kuanzia saa sita mchana Ijumaa hadi saa moja siku ya Jumamosi.
Agizo hilo litazingatiwa kuanzia Jumamosi hadi Jumapili.
Hali ya joto kali ambayo imesababisha Uhispania, Uingereza na Ufaransa kudorora kwa siku kadhaa inatarajiwa kuelekea upande wa mashariki, huku watabiri wa hali ya hewa nchini Ujerumani na Jamhuri ya Czech wakionya juu ya hali mbaya zaidi.
Halijoto nchini Ujerumani inaweza kufikia nyuzi joto 40 kote nchini siku ya leo Ijumaa.
Tahadhari ya hali mbaya ya hewa umetolewa katika sehemu kadhaa za Jamhuri ya Czech.
afghanistan, africa, albania, algeria, America, american-samoa, andorra, angola, anguilla, antarctica, antigua-and-barbuda, argentina, armenia, aruba, arusha, australia, austria, azerbaijan, bahamas, bahrain, bangladesh, barbados, belarus, Belgium, belize, benin, bermuda, bhutan, bolivia, bosnia-and-herzegovina, botswana, Boukinafaso, brazil, brunei-darussalam, bulgaria, burkina-faso, burma, burundi, california, cambodia, cameroon, canada, cape-verde, cayman-islands, central-african-republic, Chad, chicago, chile, china, christmas-island, cocos-keeling-islands, colombia, comoros, congo, cook-islands, costa-rica, cote-divoire-ivory-coast, Croatia, cuba, cyprus, czech-republic, darsalaam, democratic-peoples-rep-north-korea, democratic-republic-of-the-congo-kinshasa, denmark, djibouti, dodoma, dominica, dominican-republic, dr-congo, dubai, east-timor-timor-leste, ecuador, egypt, egypty, el-salvador, england, equatorial-guinea, equitorial-guinea, eritrea, estonia, eswatini, ethiopia, falkland-islands, faroe-islands, federal-states-of-moldova, fiji, finland, Florida, france, french-guiana, french-polynesia, french-southern-territories, gabon, gaza, georgia, germany, ghana, gibraltar, goma, Greece, greenland, grenada, guadeloupe, guam, guatemala, guinea, guinea-bissau, guyana, habari, haiti, holy-see, honduras, hong-kong, houston, hungary, iceland, india, indonesia, Iowa, iran, iran-islamic-republic-of, iraq, ireland, israel, italia, italy, ivory-coast, jamaica, japan, jordan, karatu, kazakhstan, kilimanjaro, kinshasa, kiribati, kiswahili, korea, kosovo, kuwait, kyrgyzstan, lao, latvia-lebanon-lesotho-liberia-libya-liechtenstein-lithuania-luxembourg, Lebanon, liberia, macau, madagascar, malawi, malaysia-maldives, Mali, malta, marshall-islands-martinique-mauritania-mauritius, massechutes, mayotte, mazingira, mbeya, meru, mexico, miami, micronesia, monaco-mongolia-montenegro, montserrat, morocco, mozambique-myanmar, mtwara, mwanza, namibia, nauru, nepal, netherlands, netherlands-antilles, nevada, new-caledonia, new-zealand, newyork, nicaragua, niger, nigeria, niue, north-macedonia, northern-mariana-islands, norway, oman, pakistan, palau, palestine, palestinian-territories, panama, papua-new-guinea, paraguay, peoples-democratic-republic, peru, philadhephia, philipians, Philippines, pitcairn-island, poland, politics, Portugal, puerto-rico, qatar, republic-of, republic-of-brazzaville, republic-of-south-korea, reunion-island, romania, Russia, russian-federation, rwanda, sahara-occidental, saint-kitts-and-nevis, saint-lucia, saint-vincent-and-the-grenadines, samoa, san-marino, sao-tome-and-principe, saudi-arabia, saudiarabia, scotland, Senegal, serbia, seychelles, sierra-leone, Singapore, singida, slovakia-slovak-republic, slovenia, solomon-islands, somalia, southafrica, spain, sri-lanka, sudan, suriname, swaziland-eswatini, sweden, switzerland, syria, syrian-arab-republic, tabora, taiwan-republic-of-china, tajikistan, tanzania, texas, thailand, the-gambia, tibet, timor-leste-east-timor, togo, tokelau, tonga, toronto, trinidad-and-tobago, tunisia, turkey, turkmenistan, turks-and-caicos-islands, tuvalu, uganda, united-arabs-emirates, united-kingdom, united-states, uruguay, uzbekistan, vancover, vanuatu, vatican-city-state-holy-see, venezuela, vietnam, virgin-islands-british, virgin-islands-u-s, wallis-and-futuna-islands, wallis-and-futuna-islands, wallis-et-futuna, washington-dc, western-sahara, yemen, zambia, zambie, zimbabwe
Leave a Reply