Na Cantona Joseph June 24, 2026 09:17 (EAT)

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa
Habari Za Dunia

Azimio hilo kwa kiasi kikubwa ni la kiishara, lakini linaongeza shinikizo kwa Ikulu ya White House kumaliza mzozo huo mara moja.
Bunge la Seneti la Marekani linalodhibitiwa na chama cha Republican limeidhinisha mswada ambao utamlazimu Rais wa Marekani Donald Trump kusitisha vita na Iran au kutafuta kibali cha bunge kabla ya kuendelea na hatua za kijeshi.
Katika kura iliyopigwa Jumanne jioni, maseneta kadhaa wa chama cha Republican walijiunga na wenzao wa Democratic kupitisha mswada huo kwa kura 50 dhidi ya 48, hatua inayoonyesha upinzani wa pande mbili dhidi ya kuendeleza vita.
Mswada huo pia ulipitishwa katika Bunge la Wawakilishi la Marekani mwezi Juni, ambapo wabunge wanne wa Republican walipiga kura ya ndio pamoja na wabunge wate wa Dempcratic wote, na matokeo yakiwa 215 kwa 208.
Hii ni mara ya kwanza tangu kupitishwa kwa Sheria ya Nguvu za Kivita mwaka 1973 ambapo mabunge yote mawili ya Marekani yamepitisha azimio la pamoja la kusitisha hatua ya kijeshi ya rais.
Hata hivyo, azimio hilo kwa kiasi kikubwa ni la kiishara, kwani licha ya kuidhinishwa na mabunge yote mawili, halitatumwa kwa rais kutiwa saini na halilazimishi kisheria.
Umuhimu wa kura hii ni kwamba inaongeza shinikizo kwa Ikulu ya White House kumaliza vita na Iran, haswa wakati huu ambapo bei ya mafuta imepanda na upinzani wa umma dhidi ya vita hivyo umeongezeka.
Hata hivyo, afisa wa Ikulu ya White House aliambia BBC kwamba tangu makubaliano ya kusitisha mapigano yalikubaliwa Aprili 7, kwa sasa hakuna mzozo wowote ambao utahitaji kuondolewa kwa wanajeshi wa Marekani.
Trump alisuta bunge la Marekani kwa kusitisha hatua za kijeshi dhidi ya Iran: Hii ni kumsaidia adui

Rasi wa Marekani Donald Trump amekosoa vikali kura ya Seneti ya Marekani kuhusu azimio la kutaka kusitishwa kwa hatua za kijeshi dhidi ya Iran.
Trump aliandika kwamba maseneta hao walituma ujumbe kwa Iran kwamba “hawajafurahishwa na hatua zangu dhidi yao na ni lazima nisitishe mapigano. Wamemsaidia adui.”
Aliendelea kusema: ”Nilikuwa nimeiweka Iran chini ya shinikizo kali, walikuwa tayari kurudi nyuma, na walikuwa karibu kutupatia chochote. Kwa mara ya kwanza katika miongo kadhaa, Iran iliiheshimu sana Marekani na rais wake, (mimi). Lakini Bunge la Seneti la Marekani liliamua wakati mbaya zaidi, kupiga kura isiyo na maana ya Sheria ya Nguvu za Kivita,
Anasema Warepublican wanne walipiga kura na Democrats, na sasa Iran inawauliza wawakilishi wangu, ‘Kura hii inamaanisha nini?’.
”Maseneta hawa wamefanya kazi yangu kuwa ngumu zaidi, lakini sitarudi nyuma, hata iweje, kwa sababu hivyo ndivyo ninavyofanya kazi kila wakati!”.
Marekani na Israel zina ‘mpango wa kukabidhi’ jeshi la Lebanon eneo la kusini mwa nchi hiyo

Shirika la habari la Reuters linaripoti kuwa Israel na Lebanon zinafanya mradi wa majaribio unaoungwa mkono na Marekani ambapo majeshi ya Israel yatakabidhi udhibiti wa sehemu za kusini mwa Lebanon kwa jeshi la nchi hiyo.
Shirika la habari la Reuters, limewanukuu maafisa watatu waandamizi wa Israel, na kuripoti kwamba vikosi vya Lebanon vilivyohusika katika mpango huo vitapitia mafunzo ya Marekani na ukaguzi wa usalama ili kuhakikisha kuwa havina uhusiano na Hezbollah.
Kwa mujibu wa vyanzo hivyo, Israel itasalia katika eneo hilo hadi usalama wa maeneo ya kusini mwa Lebanon utakapokabidhiwa kwa wanajeshi wa Lebanon.
Marekani na Israel bado hazijathibitisha rasmi taarifa hiyo.
Mazungumzo kati ya Israel na Lebanon yanaendelea leo mjini Washington.
Suala la kujiondoa majeshi na kusitisha vita kwa pande zote, ikiwemo Lebanon, ni kipengee cha kwanza cha mkataba wa maelewano kati ya Marekani na Iran.
Marekani inachunguza madai ya makampuni ya mafuta ‘kuwapunja’ wateja – Trump

Rais wa Marekani Donald Trump ameagiza makampuni makubwa ya nishati kuchunguzwa baada ya madai kuibuja kwamba ”wanawapunja” wateja kwa kutopunguza bei ya petroli licha ya gharama ya mafuta ghafi kushuka katika masoko ya kimataifa.
Trump aliandika kwenye mtandao wa kijamii kwamba ameamuru Idara ya Haki (DOJ) “kuanza mara moja kuchunguza hili”, akiongeza kuwa anatarajia kuona bei ya petroli ikishuka “haraka zaidi kuliko ninavyoona.”
Hakutaja kampuni zozote za mafuta kwenye chapisho hilo.
Matamshi yake yanakuja baada ya bei ya mafuta kushuka baada ya kupanda zaidi wakati wa wa vita vya Iran lakini badobei ya bidhaa hiyo iko juu kuliko kabla ya mzozo kuanza.
BBC imewasiliana na DOJ na Ikulu ya White House kupata ufafanuzi zaidi.
Marekani na Israel ziliposhambulia Iran tarehe 28 Februari. Tehran ilijibu mashambulizi ya Marekani na Israel kwa kufunga Mlango wa Bahari wa Hormuz Strait hatua ambayo ilivuruga sana usafirishaji wa mafuta na gesi na kusababisha bei ya nishati duniani kupanda.
Kenya kuwashtaki wanafunzi kwa mauaji kufuatia moto uliosababisha vifo shuleni

Waendesha mashtaka wa Kenya wanasema wanajiandaa kuwashtaki wanafunzi kadhaa kwa mauaji ya wanafunzi wenzao kufuatia shambulio la kuchoma moto shule mwezi uliopita.
Wanafunzi kumi na sita, wenye umri wa kati ya miaka 15 na 18, walifariki na wengine kadhaa walijeruhiwa wakati moto ulipozuka katika bweni la Shule ya Wasichana ya Utumishi huko Gilgil, yapata kilomita 120 (maili 77) kaskazini-magharibi mwa mji mkuu, Nairobi.
Wanafunzi wanane walikamatwa baada ya polisi kusema huenda walihusika katika kuchoma moto kwa kuwasha magodoro karibu na njia ya kutokea.
“Baada ya kutathmini kwa makini ushahidi, Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (DPP) ameidhinisha mashtaka dhidi ya wanafunzi wanaotuhumiwa,” ofisi ya mwendesha mashtaka wa serikali ilisema katika taarifa.
Moto wa Mei 28 uliharibu ghorofa ya juu ya bweni lenye vitanda 135 vya kulala na malazi ya wanafunzi 202, na kuwalazimisha kukimbia kupitia mlango mmoja baada ya njia ya dharura kushindwa kufunguliwa.
Baada ya mahojiano na wanafunzi na wafanyakazi na uchunguzi wa picha za CCTV, wanafunzi wanane shuleni walishikiliwa kuhusiana na mipango na utekelezaji” wa moto huo,” polisi walisema.
Washukiwa hao, ambao wanazuiliwa, wanatarajiwa kushtakiwa rasmi mahakamani, kufuatia mapitio ya ushahidi uliokusanywa na wachunguzi.
“Washukiwa watakabiliwa na mashtaka kumi na sita (16) ya mauaji yanayotokana na tukio hilo,” ilisema Ofisi ya DPP.
Waendesha mashtaka hawakusema ni washukiwa wangapi watakaoshtakiwa au ni lini mashtaka hayo yatafikishwa mahakamani. Wanafunzi hao wanatarajiwa kufika mahakamani mjini Naivasha siku ya Jumatano.
Kenya ina historia ndefu ya moto shuleni – miaka miwili tu iliyopita watu 21 walikufa katika moto wa bweni katikati mwa Kenya.
Msongamano mkubwa katika mabweni na kushindwa kufuata miongozo ya usalama, kama vile kuweka njia za kutokea wazi na madirisha yakiwa wazi, mara nyingi husababisha idadi kubwa ya majeruhi.
Mwanamke anayesema alishikiliwa mateka na mumewe kwa miaka 12 ameokolewa Pakistan

Polisi nchini Pakistani wamemkamata mwanaume mmoja ambaye inadaiwa alimshikilia mke wake na watoto wake mateka nyumbani na kuwatendea vibaya kwa zaidi ya muongo mmoja.
Mkewe, raia wa Ufaransa anayeitwa Sylvie Yasmina, anadai kwamba mwanaume huyo alishambulia familia yake kimwili na kiakili “kila siku” na kumtaja kama “mkali sana”, polisi wa eneo hilo waliambia BBC Urdu.
Mmoja wa wana wao alifanikiwa kutoka kisiri ili kutoa ripoti polisi, jambo lililosababisha uvamizi wa nyumba yao huko Bara, mji wa mbali katika jimbo la milimani la Khyber Pakhtunkhwa.
Polisi waliwapata Yasmina na watoto wake watano katika chumba chenye msongamano na “chakavu sana”, wakiwa na michubuko miilini mwao.
Yasmina na watoto wake wamepelekwa kwenye makazi ya wanawake huko Peshawar. Polisi wanasema wanapanga kurejea Ufaransa.
Kulingana na Yasmina, mwenye umri wa miaka 54, mumewe “alikuwa amewafunga gerezani” familia hiyo tangu walipohamia Pakistan kutoka Australia mwaka 2014.
“Kulingana na mwanamke huyo… Hakuruhusiwa kukutana na mtu yeyote, watoto wao wawili wakubwa walikuwa wamekosa masomo yao, huku watoto watatu wadogo wakizaliwa Pakistani na hawakuwahi kujiandikisha shuleni,” afisa mkuu wa polisi aliambia BBC Urdu.
Mamlaka hazijamtambua mume wa Yasmina, raia wa Pakistani ambaye wanasema alikuwa “akiishi kinyume cha sheria” nchini Australia wakati wanandoa hao walipokutana.
Walioana mwaka 2003 na kuishi Australia hadi mwaka wa 2014, walipohamia Pakistani na watoto wao wawili wakubwa. Yasmina anadai kuwa hajawasiliana na ulimwengu wa nje tangu wakati huo.
“Tulinyimwa uhuru [wetu], mume wangu hakututunza jinsi anavyopaswa kama mume na baba wa watoto wangu. Anatupiga na kuweka shinikizo katika maisha yetu kila siku,” Yasmina aliandika katika taarifa yake kwa polisi, ambayo sehemu zake zimechapishwa na vyombo vya habari vya ndani.
“Nilihisi kwamba mustakabali wangu ulikuwa tayari umeharibika, mustakabali wa watoto pia ungeharibika.”
Ufaransa yathibitisha kisa cha kwanza cha Ebola

Ufaransa imethibitisha kisa cha kwanza cha Ebola – kuhusu daktari ambaye alikuwa amerejea kutoka misheni ya kibinadamu katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Daktari huyo “alilazwa mara moja katika kituo maalum” na yuko katika hali nzuri, wizara ya afya ya Ufaransa imesema Jumatano.
DR Congo ilitangaza mlipuko wa Ebola mwezi uliopita, lakini wataalamu wanaamini virusi hivyo vilianza kusambaa kwa wiki kadhaa zilizopita.
Zaidi ya watu 260 wamethibitishwa kufariki kutokana na virusi hivyo katika nchi hiyo ya Afrika ya Kati, huku watu 1,000 wakiambukizwa.
Katika taarifa yake siku ya Jumatano, wizara ya afya ya Ufaransa ilisisitiza kwamba hatari kwa watu iko “chini sana”.
Iliongeza kuwa mamlaka inafanya kazi kuwatafuta watu ambao huenda wamekutana na daktari.
Wafanyakazi wa afya wako katika hatari kubwa ya kupata Ebola, ambayo husambazwa kupitia majimaji ya mwili.
Mlipuko wa sasa wa Ebola unasababishwa na aina ya virusi vya Bundibugyo, ambavyo kwa sasa hakuna chanjo yake.
Wizara ya afya ilisema Ufaransa imeanzisha “mfumo maalum wa ufuatiliaji” kwa wafanyakazi wa misaada wanaorejea kutoka DR Congo.
Zaidi ya shule 1,000 zimefungwa huku joto kali likiongezeka Uingereza
Zaidi ya shule 1,000 nchini Uingereza na Wales zimefungwa mapema huku halijoto ikipanda kote Uingereza.
Kusini mwa Uingereza kunatabiriwa kuona viwango vya juu vya joto vya takriban 37C leo – lakini Utabiri wa hali ya hewa inaeleza halijoto “inaonekana” inaweza kuwa kubwa zaidi.
Ni kiwango kikubwa zaidi cha tahadhari kwa mujibu wa Ofisi ya Met na inamaanisha kuwa kunaweza kuwa na hatari kwa maisha pamoja na kutatiza usafiri.
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2026
afghanistan, africa, albania, algeria, America, american-samoa, andorra, angola, anguilla, antarctica, antigua-and-barbuda, argentina, armenia, aruba, arusha, australia, austria, azerbaijan, bahamas, bahrain, bangladesh, barbados, belarus, Belgium, belize, benin, bermuda, bhutan, bolivia, bosnia-and-herzegovina, botswana, Boukinafaso, brazil, brunei-darussalam, bulgaria, burkina-faso, burma, burundi, california, cambodia, cameroon, canada, cape-verde, cayman-islands, central-african-republic, Chad, chicago, chile, china, christmas-island, cocos-keeling-islands, colombia, comoros, congo, cook-islands, costa-rica, cote-divoire-ivory-coast, Croatia, cuba, cyprus, czech-republic, darsalaam, democratic-peoples-rep-north-korea, democratic-republic-of-the-congo-kinshasa, denmark, djibouti, dodoma, dominica, dominican-republic, dr-congo, dubai, east-timor-timor-leste, ecuador, egypt, egypty, el-salvador, england, equatorial-guinea, equitorial-guinea, eritrea, estonia, eswatini, ethiopia, falkland-islands, faroe-islands, federal-states-of-moldova, fiji, finland, Florida, france, french-guiana, french-polynesia, french-southern-territories, gabon, gaza, georgia, germany, ghana, gibraltar, goma, Greece, greenland, grenada, guadeloupe, guam, guatemala, guinea, guinea-bissau, guyana, habari, haiti, holy-see, honduras, hong-kong, houston, hungary, iceland, india, indonesia, Iowa, iran, iran-islamic-republic-of, iraq, ireland, israel, italia, italy, ivory-coast, jamaica, japan, jordan, karatu, kazakhstan, kilimanjaro, kinshasa, kiribati, kiswahili, korea, kosovo, kuwait, kyrgyzstan, lao, latvia-lebanon-lesotho-liberia-libya-liechtenstein-lithuania-luxembourg, Lebanon, liberia, macau, madagascar, malawi, malaysia-maldives, Mali, malta, marshall-islands-martinique-mauritania-mauritius, massechutes, mayotte, mazingira, mbeya, meru, mexico, miami, micronesia, monaco-mongolia-montenegro, montserrat, morocco, mozambique-myanmar, mtwara, mwanza, namibia, nauru, nepal, netherlands, netherlands-antilles, nevada, new-caledonia, new-zealand, newyork, nicaragua, niger, nigeria, niue, north-macedonia, northern-mariana-islands, norway, oman, pakistan, palau, palestine, palestinian-territories, panama, papua-new-guinea, paraguay, peoples-democratic-republic, peru, philadhephia, philipians, Philippines, pitcairn-island, poland, politics, Portugal, puerto-rico, qatar, republic-of, republic-of-brazzaville, republic-of-south-korea, reunion-island, romania, Russia, russian-federation, rwanda, sahara-occidental, saint-kitts-and-nevis, saint-lucia, saint-vincent-and-the-grenadines, samoa, san-marino, sao-tome-and-principe, saudi-arabia, saudiarabia, scotland, Senegal, serbia, seychelles, sierra-leone, Singapore, singida, slovakia-slovak-republic, slovenia, solomon-islands, somalia, southafrica, spain, sri-lanka, sudan, suriname, swaziland-eswatini, sweden, switzerland, syria, syrian-arab-republic, tabora, taiwan-republic-of-china, tajikistan, tanzania, texas, thailand, the-gambia, tibet, timor-leste-east-timor, togo, tokelau, tonga, toronto, trinidad-and-tobago, tunisia, turkey, turkmenistan, turks-and-caicos-islands, tuvalu, uganda, united-arabs-emirates, united-kingdom, united-states, uruguay, uzbekistan, vancover, vanuatu, vatican-city-state-holy-see, venezuela, vietnam, virgin-islands-british, virgin-islands-u-s, wallis-and-futuna-islands, wallis-and-futuna-islands, wallis-et-futuna, washington-dc, western-sahara, yemen, zambia, zambie, zimbabwe
Leave a Reply