
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa
Na Cantona Joseph Juni 11, 2026 06:00 (EAT)


Rais wa FIFA Gianni Infantino akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari katika uwanja wa Mexico City, Jumatano, Juni 10, 2026, siku moja kabla ya mechi ya ufunguzi ya Kombe la Dunia kati ya Mexico na Afrika Kusini.Picha: Eduardo Verdugo/AP Photo/picture alliance
Michuano ya kombe la dunia la kandanda inaanza leo kwa pambano kati ya wenyeji Mexico na Afrika Kusini. Rais wa shirikisho la soka ulimwenguni FIFA Gianni Infantino ametetea bei ya tiketi.
Michuano ya kombe la dunia la kandanda inaanza leo kwa pambano kati ya wenyeji Mexico na Afrika Kusini. Mechi hiyo ya ufunguzi itachezwa katika uwanja wa Estadio Azteca jijini Mexico.
Jumatano rais wa shirikisho la soka ulimwenguni FIFA Gianni Infantino alitetea bei za tiketi za kombe la dunia, akisema ikiwa wanafanya kitu kibaya, basi labda kila mtu anayeuza tiketi Amerika Kaskazini anafanya kitu kibaya.
Infantino alizungumza na waandishi wa habari wakati wa kipindi cha maswali na majibu cha nadra usiku wa kuamkia mechi ya ufunguzi. Alitetea bei za tiketi na kusema FIFA haikuwa na nguvu ya kuishawishi serikali ya Marekani kumruhusu mwamuzi wa Somalia, Omar Artan na akasifu uwezo wake wa kuiwezesha timu ya taifa ya soka ya Iran kuingia Marekani kushiriki michuano hiyo.
Mamia ya polisi wametumwa kupiga doria katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mexico City kabla ya ufunguzi wa michuano huku mamlaka wakiimarisha ulinzi wakati kukiwa na kitisho cha maandamano ya walimu.
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.