
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa
Na Cantona Joseph Juni 11, 2026 06:00 (EAT)


Israel ikibomoa nyumba ya Wapalestina Ukingo wa Magharibi katika eneo la HebronPicha: Mussa Qawasma/REUTERS
Mamlaka za Israel zadaiwa kuwafurusha wakaazi wakipalestina kutoka maeneo yao,kwa lengo la kuipora ardhi
Shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International limeishutumu Israel kwa kile ilichokiita kuendesha kampeni ya “Takasataka ya kikabila” dhidi ya jamii za Wabedui na wafugaji wa Kipalestina katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu.
Katika ripoti mpya, shirika hilo limesema mamlaka za Israel zinaharakisha hatua za kuunganisha eneo hilo kwa kuwafurusha wakazi wa Kipalestina kutoka maeneo yao.
Shirika hilo linasema jamii 27 za Wabedui na wafugaji, zinazojumuisha mamia ya watu, zilifurushwa kati ya mwaka 2023 na 2025 au zilikuwa hatarini kufurushwa katika eneo ambalo liko chini ya udhibiti kamili wa Israel,lililopewa jina la herufi C.
Amnesty pia imeishutumu serikali ya Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, kwa kuunga mkono ajenda ya walowezi wa Kiyahudi. Israel haikutoa tamko lake kuhusu madai hayo.
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.