Ufaransa kumshitaki mwanajeshi wa zamani wa Rwanda

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Na Cantona Joseph April 09, 2026 06:40 (EAT)

Vocalize Pre-Player Loader

Ufaransa itamfungulia mashitaka mwanajeshi wa zamani wa Rwanda kwa kuhusika katika mauaji ya halaiki ya mwaka 1994.Picha: SIMON MAINA/AFP

Mahakama ya Ufaransa itamshtaki luteni kanali wa zamani wa jeshi la Rwanda Cyprien Kayumba kwa mashtaka ya kushiriki katika mauaji ya kimbari ya 1994.

Mahakama ya Ufaransa itamshtaki luteni kanali wa zamani wa jeshi la Rwanda Cyprien Kayumba kwa mashtaka ya kushiriki katika mauaji ya kimbari kwa madai ya kuwasilisha silaha zilizotumika wakati wa mauaji ya mwaka 1994.

Hayo ni kwa mujibu wa chanzo cha mahakama katika kauli yake ya jana Jumatano.

Kayumba mwenye umri wa miaka 71 kutoka kwa jamii ya Wahutu, aliongoza idara ya wizara ya ulinzi iliyohusika na kuagiza na kuwasilisha silaha wakati wa mauaji ya kimbari.

Kayumba, ambaye ameishi Ufaransa tangu 1998, amekuwa akidai kila mara kwamba hakujua silaha alizoagiza zingetumika kuwaua Watutsi.

Majaji waliamuru kwamba Kayumba ashtakiwe katika tarehe ambayo haijapangwa kwa mashtaka ya kushiriki katika mauaji ya kimbari na kushiriki katika uhalifu dhidi ya binadamu. Walimwamuru akabidhi pasipoti yake na kumkataza kuondoka Ufaransa.

Trump: Lebanon si sehemu ya makubalino ya kusitisha vita

Israel imefanya wimbi la mashambulizi nchini Lebanon licha ya usitishwaji vita mashariki ya kati.Picha: Bilal Hussein/AP Photo/picture alliance

Rais wa Marekani Donald Trump amesema Lebanon si sehemu ya makubaliano ya kusitisha mapigano kwa wiki mbili yaliyoafikiwa, akiliita suala la Lebanon kuwa mzozo tofauti.

Kauli ya Trumo imekuja huku Israel ikifanya wimbi kubwa la mashambulizi dhidi ya Lebanon baada ya makubaliano hayo kutangazwa. Iran kwa upande wake imesema itakomesha usitishaji mapigano kwa upande mmoja ikiwa mashambulizi ya Israel yataendelea dhidi ya Lebanon.

Wizara ya afya ya Lebanon imetangaza idadi ya vifo kutokana na mashambulizi makubwa ya Israeli jana Jumatano kuwa watu 182.

Kamati ya kimataifa ya Msalaba Mwekundu (ICRC) ilisema imekasirishwa na vifo na uharibifu huo mbaya. Kundi la Hezbollah limesema hivi leo limevurumisha maroketi kuelekea kaszini mwa Israel kujibu mashambulizi hayo.

Wakati haya yakiarifiwa, waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema Israel iko tayari kurudi vitani  baada ya kutangazwa kwa makubaliano ya kusitisha mapigano na Iran.

Zaidi ya wafanyakazi 3,000 wa misaada wauwawa katika miaka 3

Tom Fletcher amesema vifo vimeongezeka kutokana na kusambaratika ulinzi.Picha: Manuel Elias/Xinhua/IMAGO

Umoja wa Mataifa umesema zaidi ya wafanyakazi 1,000 wa kutoa misaada ya kibinadamu wameuawa kote ulimwenguni katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita, karibu mara tatu ya idadi ya vifo katika miaka mitatu iliyopita.

Mkuu wa kuratibu misaada ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa Tom Fletcher aliliambia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa Jumatano kwamba ongezeko hilo halikutokea kwa bahati mbaya bali ni kutokana na kusambaratika kwa ulinzi.

Fletcher alisema kati ya wafanyakazi zaidi ya 1,010 wa kibinadamu waliouawa kuanzia 2023 hadi 2025, zaidi ya 560 waliuwawa Gaza na Ukingo wa Magharibi, 130 nchini Sudan, 60 nchini Sudan Kusini, 25 nchini Ukraine na 25 nchini Kongo.

Baraza la Usalama lilikuwa likikutana kuhusu azimio lililopitishwa Mei 2024 ambalo lililaani vikali mashambulizi dhidi ya wafanyakazi wa kutoa misaada ya kibinadamu na wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa na kuwataka wapiganaji wote kuwalinda kwa mujibu wa sheria za kimataifa.

Mtu mmoja auwawa na mabaki ya droni Urusi

Ukraine imekuwa ikifanya mashambulizi kudhibiti uhasama wa UrusiPicha: Iryna Rybakova/93rd Separate Mechanized Brigade Kholodnyi Yar/AFP

Mwanamume mmoja ameuliwa na mabaki ya droni iliytunguliwa katika eneo la kusini la Urusi. Ukraine imekuwa ikifanya mashambulizi katika eneo hilo kujibu mashambuli ya Urusi.

Mabaki ya ndege isiyo na rubani iliyodunguliwa kusini mwa Krasnodar Krai yamemuua mwanamume mmoja. Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na gavana wa eneo hilo la UrusiVeniamin Kondratyev mapema leo.

Mwanamume huyo aligongwa na mabaki ya ndege isiyo na rubani alipokuwa kwenye roshani ya jengo la ghorofa katika kijiji cha Sauk-Dere katika wilaya ya Krymsk.

Vipande vya ndege zisizo na rubani zilizoharibiwa pia vilianguka kwenye eneo la biashara na katika maeneo kadhaa katika eneo hilo lakini hakuna majeraha yoyote yaliyoripotiwa.

afghanistanafricaalbaniaalgeriaAmericaamerican-samoaandorraangolaanguillaantarcticaantigua-and-barbudaargentinaarmeniaarubaarushaaustraliaaustriaazerbaijanbahamasbahrainbangladeshbarbadosbelarusBelgiumbelizebeninbermudabhutanboliviabosnia-and-herzegovinabotswanaBoukinafasobrazilbrunei-darussalambulgariaburkina-fasoburmaburundicaliforniacambodiacamerooncanadacape-verdecayman-islandscentral-african-republicChadchicagochilechinachristmas-islandcocos-keeling-islandscolombiacomoroscongocook-islandscosta-ricacote-divoire-ivory-coastCroatiacubacyprusczech-republicdarsalaamdemocratic-peoples-rep-north-koreademocratic-republic-of-the-congo-kinshasadenmarkdjiboutidodomadominicadominican-republicdr-congodubaieast-timor-timor-lesteecuadoregyptegyptyel-salvadorenglandequatorial-guineaequitorial-guineaeritreaestoniaeswatiniethiopiafalkland-islandsfaroe-islandsfederal-states-of-moldovafijifinlandFloridafrancefrench-guianafrench-polynesiafrench-southern-territoriesgabongazageorgiagermanyghanagibraltargomaGreecegreenlandgrenadaguadeloupeguamguatemalaguineaguinea-bissauguyanahabarihaitiholy-seehondurashong-konghoustonhungaryicelandindiaindonesiaIowairaniran-islamic-republic-ofiraqirelandisraelitaliaitalyivory-coastjamaicajapanjordankaratukazakhstankilimanjarokinshasakiribatikiswahilikoreakosovokuwaitkyrgyzstanlaolatvia-lebanon-lesotho-liberia-libya-liechtenstein-lithuania-luxembourgLebanonliberiamacaumadagascarmalawimalaysia-maldivesMalimaltamarshall-islands-martinique-mauritania-mauritiusmassechutesmayottemazingirambeyamerumexicomiamimicronesiamonaco-mongolia-montenegromontserratmoroccomozambique-myanmarmtwaramwanzanamibianaurunepalnetherlandsnetherlands-antillesnevadanew-caledonianew-zealandnewyorknicaraguanigernigerianiuenorth-macedonianorthern-mariana-islandsnorwayomanpakistanpalaupalestinepalestinian-territoriespanamapapua-new-guineaparaguaypeoples-democratic-republicperuphiladhephiaphilipiansPhilippinespitcairn-islandpolandpoliticsPortugalpuerto-ricoqatarrepublic-ofrepublic-of-brazzavillerepublic-of-south-koreareunion-islandromaniaRussiarussian-federationrwandasahara-occidentalsaint-kitts-and-nevissaint-luciasaint-vincent-and-the-grenadinessamoasan-marinosao-tome-and-principesaudi-arabiasaudiarabiascotlandSenegalserbiaseychellessierra-leoneSingaporesingidaslovakia-slovak-republicsloveniasolomon-islandssomaliasouthafricaspainsri-lankasudansurinameswaziland-eswatiniswedenswitzerlandsyriasyrian-arab-republictaborataiwan-republic-of-chinatajikistantanzaniatexasthailandthe-gambiatibettimor-leste-east-timortogotokelautongatorontotrinidad-and-tobagotunisiaturkeyturkmenistanturks-and-caicos-islandstuvaluugandaunited-arabs-emiratesunited-kingdomunited-statesuruguayuzbekistanvancovervanuatuvatican-city-state-holy-seevenezuelavietnamvirgin-islands-britishvirgin-islands-u-swallis-and-futuna-islandswallis-and-futuna-islandswallis-et-futunawashington-dcwestern-saharayemenzambiazambiezimbabwe

CantonaDigital
CantonaDigital

Listen Live Radio Fortune Africa
Ukweli Na Burudani.

-Be ready to be Impacted, Inspired & Empowered.

-Keep watching our Channels

Cantona Cast Television,

Fortune Television Network (FTN)

Donation
Paypal https://www.paypal.com/donate/?hosted_button_id=6EKXMLNW8W6A2&fbclid=IwY2xjawQxeChleHRuA2FlbQIxMABicmlkETFRdkNBRndpclRDQTB5bXZZc3J0YwZhcHBfaWQQMjIyMDM5MTc4ODIwMDg5MgABHq960uGsyU3ABRIBc2h-iXGhHATvuEqe55gFsQ-rDb0fT-Z7SIQ3TV8LnkpD_aem_ybU2SvBlvyqrVsS9NAczRw

An attitude determines an altitude.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025

5,388 posts
0 followers

Fediverse Followers


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a Reply