Wakenya 16 hawajulikani waliko baada ya kujiunga na jeshi la Urusi

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Na  Cantona Joseph April 03, 2026 7:08 (EAT)

Vocalize Pre-Player Loader
Jamaa za wale wanaosema walilaghaiwa kupigania Urusi wamekuwa wakiitaka serikali ya Kenya kuingilia kati.
Maelezo ya picha,Jamaa za wale wanaosema walilaghaiwa kupigania Urusi wamekuwa wakiitaka serikali ya Kenya kuingilia kati.

Wakenya 16 wametoweka nchini Urusi baada ya kujiunga na jeshi la nchi hiyo, na wengine 47 wamerejea nyumbani kutoka vitani nchini Ukraine, Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya Musalia Mudavadi ameimbia kikao cha kamati ya Bunge la Seneti.

Wengine 38 kwa sasa wako katika hospitali tofauti za Urusi chini ya vizuizi vya ufikiaji Mudavadi aliongeza kusema.

Idadi ya Wakenya waliotoweka nchini Urusi imeongezeka kutoka 10 hadi 16 ndani ya saa 24 zilizopita.

Bado haijabainika ikiwa wamefariki au wako hai.

Waziri huyo pia alikadiria kuwa Wakenya 165 wanashiriki kikamilifu katika operesheni za kijeshi, na kufanya jumla ya walioshiriki katika mzozo wa Ukraine kufikia zaidi ya 250.

Mudavadi alisema idadi hiyo huenda ikawa kubwa zaidi.

Aliongeza kuwa Wakenya wawili wanazuiliwa nchini Ukraine kama wafungwa wa kivita.

Mudavadi pi alisema walioajiriwa wametia saini kandarasi za kuhudumu kama maafisa wa usafirishaji au kufanya majukumu ya kivita.

“Kinyume na ripoti zilizopo, Wakenya wengi walijiunga na jeshi la Urusi kwa hiari,” Mudavadi aliambia kamati ya wabunge.

Baadhi ya mashirika yenye makao makuu nchini Kenya, Urusi, Qatar na Umoja wa Falme za Kiarabu yalihusika na usajili huo, kwa mujibu wa waziri Mudavadi.

Kenya imeanzisha uchunguzi kuhusu usajiliwa kwa raia wake kupigana vita nchini Ukraine kinyume cha sheria.

Waziri wa Ulinzi Pete Hegseth amtaka Mkuu wa Majeshi kuachia ngazi

Randy George
Maelezo ya picha,Mkuu wa Jeshi la Marekani Randy George

Waziri wa Ulinzi wa Marekani Pete Hegseth amemtaka Mkuu wa Majeshi Randy George kuachia wadhifa wake, kulingana na CBS News, mshirika wa habari BBC wa Marekani.

Msemaji Mkuu wa Pentagon Sean Parnell alisema katika taarifa yake kwenye mitandao ya kijamii kwamba George “atastaafu kutoka wadhifa wake kama Mkuu wa 41 wa Wanajeshi mara moja”.

Mkuu wa Jeshi kawaida huhudumu kwa kipindi cha miaka minne.

George, afisa wa kijeshi ambaye alihitimu kutoka chuo cha kijeshi cha West Point, aliteuliwa kwa jukumu hilo mnamo 2023 na Rais wa zamani Joe Biden.

Mabadiliko ya hivi punde yanakuja baada ya Trump kusema katika hotuba yake kwa taifa kwamba vita vya Marekani na Israel dhidi ya Iran vinatarajiwa kumalizika “hivi karibuni”.

George aliwahi kuwa afisa wa jeshi katika Vita vya kwanza vya Ghuba na katika migogoro ya hivi majuzi nchini Iraq na Afghanistan.

Haijabainika kwa nini alitakiwa kuondoka. “Tunashukuru kwa utumishi wake, lakini ulikuwa wakati wa mabadiliko ya uongozi katika Jeshi,” afisa mkuu wa ulinzi ambaye hakutajwa jina aliiambia CBS.

Msemaji wa Pentagon Parnell alisema: “Idara ya Vita inashukuru kwa miongo kadhaa ya utumishi wa Jenerali George kwa taifa letu. Tunamtakia kila la heri anapostaafu.”

Nafasi yake itachukuliwa na Makamu Mkuu wa Jeshi Jenerali Christopher LaNeve ambaye atakuwa kaimu mkuu wa majeshi, kulingana na vyombo vya habari vya Marekani.

Kushambulia miundo mbinu ya raia hakutaifanya Iran kusalimu amri – Araghchi

Abbas Araghchi

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Abbas Araghchi amesema kulengwa kwa daraja la B1 kwenye barabara kuu ya Tehran-Kaskazini hakutaifanya nchi hiyo kusalimu amri.

Bwana Araghchi aliandika kwenye Mtandao wa X: “Kulenga miundombinu ya kiraia, ikiwa ni pamoja na madaraja ambayo ujenzi wake bado unaendelea, kamwe hakutawashinikiza Wairani kusalimu amri… Kila daraja na kila jengo litajengwa upya kwa ustadi zaidi; lakini jambo ambalo kamwe halitarekebishwa ni uharibifu unaofanywa kwa na Marekani.”

Saa kadhaa zilizopita, Donald Trump alichapisha video ya shambulio la Marekani dhidi ya daraja hilo kwenye mtandao wake wa kijamii, akiandika: “Ni wakati wa Iran kufikia makubaliano kabla ya muda kuwapa kisogo na kuiacha nchi ikiwa imesambaratika.”

Marekani yashambulia daraja kuu la Iran

.

Rais wa Marekani Donald Trump ametangaza kushambiliwa kwa daraja la B1 la Iran, iliyojengwa hivi karibuni ambayo ilikuwa inaunganisha mji wa Karaj na mji mkuu Tehran.

Trump aliongeza: “Tuliripua madaraja yao makuu matatu jana usiku. Yanaharibiwa …”

Video inaonyesha moto na moshi ukifuka juu ya daraja hilo, nasehemu ya katikati ikiwa imeachana.

Watu wanane wameripotiwa kuuawa na wengine 100 kujeruhiwa katika shambulio hilo

Daraja la B1, ambalo halikuwa halijaanza kutumika linatajwa kuwa mojawapo ya madaraja marefu zaidi katika Mashariki ya Kati. Lina urefu wa mita 1,050 na nguzo zenye urefu wa mita 136, kulingana na ripoti ya vyombo vya habari vya serikali ya Iran.

afghanistanafricaalbaniaalgeriaAmericaamerican-samoaandorraangolaanguillaantarcticaantigua-and-barbudaargentinaarmeniaarubaarushaaustraliaaustriaazerbaijanbahamasbahrainbangladeshbarbadosbelarusBelgiumbelizebeninbermudabhutanboliviabosnia-and-herzegovinabotswanaBoukinafasobrazilbrunei-darussalambulgariaburkina-fasoburmaburundicaliforniacambodiacamerooncanadacape-verdecayman-islandscentral-african-republicChadchicagochilechinachristmas-islandcocos-keeling-islandscolombiacomoroscongocook-islandscosta-ricacote-divoire-ivory-coastCroatiacubacyprusczech-republicdarsalaamdemocratic-peoples-rep-north-koreademocratic-republic-of-the-congo-kinshasadenmarkdjiboutidodomadominicadominican-republicdr-congodubaieast-timor-timor-lesteecuadoregyptegyptyel-salvadorenglandequatorial-guineaequitorial-guineaeritreaestoniaeswatiniethiopiafalkland-islandsfaroe-islandsfederal-states-of-moldovafijifinlandFloridafrancefrench-guianafrench-polynesiafrench-southern-territoriesgabongazageorgiagermanyghanagibraltargomaGreecegreenlandgrenadaguadeloupeguamguatemalaguineaguinea-bissauguyanahabarihaitiholy-seehondurashong-konghoustonhungaryicelandindiaindonesiaIowairaniran-islamic-republic-ofiraqirelandisraelitaliaitalyivory-coastjamaicajapanjordankaratukazakhstankilimanjarokinshasakiribatikiswahilikoreakosovokuwaitkyrgyzstanlaolatvia-lebanon-lesotho-liberia-libya-liechtenstein-lithuania-luxembourgLebanonliberiamacaumadagascarmalawimalaysia-maldivesMalimaltamarshall-islands-martinique-mauritania-mauritiusmassechutesmayottemazingirambeyamerumexicomiamimicronesiamonaco-mongolia-montenegromontserratmoroccomozambique-myanmarmtwaramwanzanamibianaurunepalnetherlandsnetherlands-antillesnevadanew-caledonianew-zealandnewyorknicaraguanigernigerianiuenorth-macedonianorthern-mariana-islandsnorwayomanpakistanpalaupalestinepalestinian-territoriespanamapapua-new-guineaparaguaypeoples-democratic-republicperuphiladhephiaphilipiansPhilippinespitcairn-islandpolandpoliticsPortugalpuerto-ricoqatarrepublic-ofrepublic-of-brazzavillerepublic-of-south-koreareunion-islandromaniaRussiarussian-federationrwandasahara-occidentalsaint-kitts-and-nevissaint-luciasaint-vincent-and-the-grenadinessamoasan-marinosao-tome-and-principesaudi-arabiasaudiarabiascotlandSenegalserbiaseychellessierra-leoneSingaporesingidaslovakia-slovak-republicsloveniasolomon-islandssomaliasouthafricaspainsri-lankasudansurinameswaziland-eswatiniswedenswitzerlandsyriasyrian-arab-republictaborataiwan-republic-of-chinatajikistantanzaniatexasthailandthe-gambiatibettimor-leste-east-timortogotokelautongatorontotrinidad-and-tobagotunisiaturkeyturkmenistanturks-and-caicos-islandstuvaluugandaunited-arabs-emiratesunited-kingdomunited-statesuruguayuzbekistanvancovervanuatuvatican-city-state-holy-seevenezuelavietnamvirgin-islands-britishvirgin-islands-u-swallis-and-futuna-islandswallis-and-futuna-islandswallis-et-futunawashington-dcwestern-saharayemenzambiazambiezimbabwe



CantonaDigital
CantonaDigital

Listen Live Radio Fortune Africa
Ukweli Na Burudani.

-Be ready to be Impacted, Inspired & Empowered.

-Keep watching our Channels

Cantona Cast Television,

Fortune Television Network (FTN)

Donation
Paypal https://www.paypal.com/donate/?hosted_button_id=6EKXMLNW8W6A2&fbclid=IwY2xjawQxeChleHRuA2FlbQIxMABicmlkETFRdkNBRndpclRDQTB5bXZZc3J0YwZhcHBfaWQQMjIyMDM5MTc4ODIwMDg5MgABHq960uGsyU3ABRIBc2h-iXGhHATvuEqe55gFsQ-rDb0fT-Z7SIQ3TV8LnkpD_aem_ybU2SvBlvyqrVsS9NAczRw

An attitude determines an altitude.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025

5,344 posts
0 followers

Fediverse Followers


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a Reply