
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa
Na Cantona Joseph April 03, 2026 13:08 (EAT)


Nchini Kuwait, shambulizi la Iran limesababisha moto mkubwa katika kiwanda cha kusafisha mafuta.Picha: Stringer/Anadolu Agency/IMAGO
Iran imeendeleza mashambulizi yake katika maeneo mbalimbali ya Mashariki ya Kati usiku wa kuamkia leo. Huko nchini Kuwait, shambulizi la Iran limesababisha moto mkubwa katika kiwanda cha kusafisha mafuta.
Iran imeendeleza mashambulizi yake katika maeneo mbalimbali ya Mashariki ya Kati usiku wa kuamkia leo. Huko nchini Kuwait, shambulizi la Iran limesababisha moto mkubwa katika kiwanda cha kusafisha mafuta.
Marekani na Isreal pia zimefanya mashambulizi ya anga nchini Iran wakati vita hivyo vikikaribia wiki yake ya tano ya mapigano tangu kuanza kwake Februari 28.
Katika hatua nyingine, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limepanga kupiga kura leo Ijumaa kuhusu pendekezo la Bahrain ambalo linalenga kujadili hatua mbalimbali za kufuata ili kufunguliwa kwa mlango bahari wa Hormuz ambao umefungwa na Iran.
Bahrain imependekeza azimio la kuruhusu mataifa kutumia nguvu kuhakikisha usafiri wa kimataifa unaendelea, lakini pendekezo hilo linaonekana kuligawa Baraza la Usalama hata kabla ya kupigiwa kura.
Viwanda Ujerumani vyageukia uzalishaji wa vifaa vya ulinzi

Shirika la kusimamia maslahi ya Viwanda na Biashara nchini Ujerumani (DIHK)Picha: Fabian Sommer/dpa/picture alliance
Utafiti uliofanywa na jarida moja la habari za biashara nchini Ujerumani umebaini kwamba karibu theluthi moja ya makampuni ya viwanda yameona fursa katika mifumo yao ya kibiashara kwenye sekta ya usalama na ulinzi.
Shirika la kusimamia maslahi ya Viwanda na Biashara nchini Ujerumani (DIHK) limesema sekta ya viwanda nchini Ujerumani katika kipindi hiki imegeukia zaidi kwenye uzalishaji wa vifaa vya ulinzi.
Utafiti uliofanywa na jarida moja la habari za biashara nchini Ujerumani umebaini kwamba karibu theluthi moja ya makampuni ya viwanda yameona fursa katika mifumo yao ya kibiashara kwenye sekta ya usalama na ulinzi.
Rainer Kambeck ambaye ni mtaalam katika shirika hilo amesema kwamba utafiti huo umeonyesha wazi ukuaji katika sekta ya ulinzi na hali hiyo imechangiwa na migogoro ya kikanda na ya kisiasa inayoendelea duniani.
Uchambuzi maalum wa DIHK unaonyesha kuwa kampuni moja kati ya sita za viwanda nchini Ujerumani tayari imeunganishwa katika mnyororo wa thamani kwenye sekta ya ulinzi.
Sekta ya utengenezaji wa magari ndiyo inayoongoza kwa asilimia 36.
Ibrahim Traore: Wananchi lazima msahau kuhusu demokrasia

Kiongozi wa kijeshi wa Burkina Faso, Ibrahim TraorePicha: Mikhail Tereshchenko/TASS/ZUMA/picture alliance
Akitolea ufafanuzi kauli yake, Traore amesema kwamba watu wa Burkina Faso wanahitaji kusahau suala hilo sababu msingi wa demokrasia yenyewe sio kwa ajili yao.
Kiongozi wa kijeshi nchini Burkina Faso Kapteni Ibrahim Traore amewaambia wananchi wa taifa hilo la Afrika Magharibi kwamba lazima wasahau kuhusu demokrasia. Traore amesema hayo katika mahojiano yaliyotangazwa kwenye televisheni ya kitaifa nchini humo ya RTB.
Akitolea ufafanuzi kauli yake, Traore amesema kwamba watu wa Burkina Faso wanahitaji kusahau suala hilo sababu msingi wa demokrasia yenyewe sio kwa ajili yao.
Itakumbukwa kwamba kiongozi huyo alichukua madaraka kwa njia ya mapinduzi ya kijeshi mnamo Septemba 2022 baada ya kuiangusha serikali nyingine ya kijeshi, na tangu wakati huo amezuia sauti za wapinzani.
Serikali ya kijeshi ilivunja tume ya uchaguzi ya nchi hiyo mwaka jana na kisha mwezi Februari. Bunge lililoongozwa na wanajeshi pia lilipiga marufuku vyama vyote vya siasa, ambavyo shughuli zake zilikuwa zimesimamishwa tangu 2022. Hata hivyo, Umoja wa Mataifa umeitaka Burkina kubatilisha uamuzi wa kupiga marufuku vyama vya siasa na kukomesha ukandamizaji.
Urusi yaushambulia mji wa Kharkiv wa Ukraine mfululizo

Zimamoto mjini Kharkiv, Ukraine wakipambana kuuzima moto uliotokana na shambulio la UrusiPicha: Sofiia Gatilova/REUTERS
Mamlaka katika mji wa Kharkiv mashariki mwa Ukraine imesema leo kuwa mji huo umeendelea kukabiliwa na mashambulizi ya anga ya mfululizo kutoka Urusi kwa zaidi ya siku moja sasa.
Mamlaka katika mji wa Kharkiv mashariki mwa Ukraine imesema leo kuwa mji huo umeendelea kukabiliwa na mashambulizi ya anga ya mfululizo kutoka Urusi kwa zaidi ya siku moja sasa.
Kupitia mtandao wa kijamii wa Telegram, gavana wa kijeshi wa mji huo, Oleh Syniehubov, ameandika kwamba mashambulizi ya makombora na droni yaliyoulenga mji huo yamejeruhi na kuharibu majengo ya makaazi na ofisi.
Mji huo ambao ni wa pili kwa ukubwa nchini Ukraine, ulikuwa na idadi ya watu milioni 1.4 kabla ya vita, uko umbali wa takriban kilomita 40 tu kutoka mpaka wa Urusi. Kwa mujibu wa mamlaka nchini Ukraine ni kwamba leo siku ya Ijumaa Kuu zinatimia siku 1,500 tangu uvamizi wa Urusi Februari mwaka 2022.
Kwa upande wa Urusi, Wizara ya Ulinzi huko Moscow imeripoti kwamba droni 192 za Ukraine zilidunguliwa siku ya Alhamisi.
Bei ya vyakula ziliongezeka maradufu mwezi Machi

FAO imesema bei za vyakula zimepaa zaidi mwezi MachiPicha: AFP
Katika ripoti tofauti, FAO iliongeza kwa asilimia chache utabiri wake wa uzalishaji wa nafaka duniani wa 2025 hadi tani bilioni 3.036 zitakazorekodiwa.
Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa limesema leo kwamba bei za vyakula duniani zilipanda mwezi Machi hadi kiwango cha juu zaidi tangu Desemba, na kuashiria ongezeko la mara ya pili mfululizo la kila mwezi.
Kielelezo cha bei ya chakula cha FAO, ambacho hupima mabadiliko katika masoko ya bidhaa za chakula zinazouzwa kimataifa, kilikuwa na wastani wa alama 128.5 mwezi Machi, ongezeko la asimilia 2.4 kutoka kiwango chake kilichorekebishwa cha mwezi uliopita wa Februari.
Katika ripoti tofauti, FAO iliongeza kwa asilimia chache utabiri wake wa uzalishaji wa nafaka duniani wa 2025 hadi tani bilioni 3.036 zitakazorekodiwa. Utabiri huo unamaanisha kwamba kutakuwa na ongezeko la asilimia 5.8 mwaka huu ukilinganisha na mwaka uliopita.
Iran, Israel zaendelea kushambuliana licha ya madai ya Trump

Uharibifu baada ya mvua ya makombora ya Iran kurushwa kuelekea Israel, katika muktadha wa mgogoro kati ya Marekani, Israel na Iran, katika mji wa Petah Tikva, Israel tarehe 2 Aprili 2026.Picha: Ammar Awad/REUTERS
Iran na Israel zimeendelea kushambuliana kwa makombora na droni, wakati Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa likitarajiwa kupiga kura kuhusu mlano-bahari wa Hormuz.
Iran imeendelea kurusha makombora kuelekea Israel na nchi za Ghuba, ikisisitiza kuwa bado ina uwezo mkubwa wa kijeshi na akiba ya silaha, licha ya kauli ya Rais wa Marekani Donald Trump kwamba uwezo wa kijeshi wa taifa hilo umedhoofishwa pakubwa.
Kwa upande mwingine, Israel imesema imemuua kamanda mwandamizi wa Iran, Jamshid Eshaghi, katika shambulio lililofanyika Tehran, hatua inayoongeza shinikizo kwa uongozi wa kijeshi wa Iran.

Mashambulizi ya Marekani na Israel dhidi ya Iran yameendelea pia kusababisha uharibifu mkubwa wa miundombinu ya kijeshi, kiuchumi na kiraia.Picha: Iranian Red Crescent Society/Handout/REUTERS
Nchini Lebanon, mashambulizi ya Israel dhidi ya makundi yanayoungwa mkono na Iran yameripotiwa kuua watu 27 ndani ya saa 24 zilizopita.
Wakati huo huo, mashambulizi ya anga ndani ya Iran yamelenga miundombinu muhimu, ikiwemo daraja linaloripotiwa kuwa refu zaidi katika Mashariki ya Kati, na kusababisha vifo na majeruhi.
Iran imekosoa mashambulizi hayo, ikisema kulenga miundombinu ya kiraia hakuwezi kuilazimisha kusalimu amri.
Kwingineko waasi wa Kihouthi nchini Yemen wamethibitisha kurusha makombora kuelekea Israel, kwa kushirikiana na Iran na kundi la Hezbollah.
afghanistan, africa, albania, algeria, America, american-samoa, andorra, angola, anguilla, antarctica, antigua-and-barbuda, argentina, armenia, aruba, arusha, australia, austria, azerbaijan, bahamas, bahrain, bangladesh, barbados, belarus, Belgium, belize, benin, bermuda, bhutan, bolivia, bosnia-and-herzegovina, botswana, Boukinafaso, brazil, brunei-darussalam, bulgaria, burkina-faso, burma, burundi, california, cambodia, cameroon, canada, cape-verde, cayman-islands, central-african-republic, Chad, chicago, chile, china, christmas-island, cocos-keeling-islands, colombia, comoros, congo, cook-islands, costa-rica, cote-divoire-ivory-coast, Croatia, cuba, cyprus, czech-republic, darsalaam, democratic-peoples-rep-north-korea, democratic-republic-of-the-congo-kinshasa, denmark, djibouti, dodoma, dominica, dominican-republic, dr-congo, dubai, east-timor-timor-leste, ecuador, egypt, egypty, el-salvador, england, equatorial-guinea, equitorial-guinea, eritrea, estonia, eswatini, ethiopia, falkland-islands, faroe-islands, federal-states-of-moldova, fiji, finland, Florida, france, french-guiana, french-polynesia, french-southern-territories, gabon, gaza, georgia, germany, ghana, gibraltar, goma, Greece, greenland, grenada, guadeloupe, guam, guatemala, guinea, guinea-bissau, guyana, habari, haiti, holy-see, honduras, hong-kong, houston, hungary, iceland, india, indonesia, Iowa, iran, iran-islamic-republic-of, iraq, ireland, israel, italia, italy, ivory-coast, jamaica, japan, jordan, karatu, kazakhstan, kilimanjaro, kinshasa, kiribati, kiswahili, korea, kosovo, kuwait, kyrgyzstan, lao, latvia-lebanon-lesotho-liberia-libya-liechtenstein-lithuania-luxembourg, Lebanon, liberia, macau, madagascar, malawi, malaysia-maldives, Mali, malta, marshall-islands-martinique-mauritania-mauritius, massechutes, mayotte, mazingira, mbeya, meru, mexico, miami, micronesia, monaco-mongolia-montenegro, montserrat, morocco, mozambique-myanmar, mtwara, mwanza, namibia, nauru, nepal, netherlands, netherlands-antilles, nevada, new-caledonia, new-zealand, newyork, nicaragua, niger, nigeria, niue, north-macedonia, northern-mariana-islands, norway, oman, pakistan, palau, palestine, palestinian-territories, panama, papua-new-guinea, paraguay, peoples-democratic-republic, peru, philadhephia, philipians, Philippines, pitcairn-island, poland, politics, Portugal, puerto-rico, qatar, republic-of, republic-of-brazzaville, republic-of-south-korea, reunion-island, romania, Russia, russian-federation, rwanda, sahara-occidental, saint-kitts-and-nevis, saint-lucia, saint-vincent-and-the-grenadines, samoa, san-marino, sao-tome-and-principe, saudi-arabia, saudiarabia, scotland, Senegal, serbia, seychelles, sierra-leone, Singapore, singida, slovakia-slovak-republic, slovenia, solomon-islands, somalia, southafrica, spain, sri-lanka, sudan, suriname, swaziland-eswatini, sweden, switzerland, syria, syrian-arab-republic, tabora, taiwan-republic-of-china, tajikistan, tanzania, texas, thailand, the-gambia, tibet, timor-leste-east-timor, togo, tokelau, tonga, toronto, trinidad-and-tobago, tunisia, turkey, turkmenistan, turks-and-caicos-islands, tuvalu, uganda, united-arabs-emirates, united-kingdom, united-states, uruguay, uzbekistan, vancover, vanuatu, vatican-city-state-holy-see, venezuela, vietnam, virgin-islands-british, virgin-islands-u-s, wallis-and-futuna-islands, wallis-and-futuna-islands, wallis-et-futuna, washington-dc, western-sahara, yemen, zambia, zambie, zimbabwe
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.