
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa
Na Cantona Joseph April 02, 2026 05:08 (EAT)


Uzinduzi wa misheni ya mwezi ya NASA Artemis IIPicha: Brendan McDermid/REUTERS
Wanaanga wa chombo cha Artemis II wanaelekea mwezini baada ya kurushwa katika safari ya kwanza ya NASA ya mwezini miongo mitano tangu safari ya kwanza ya Apollo.
Shirika la anga la Marekani, NASA, limeanzisha safari mpya ya kihistoria kuelekea mwezini kwa kurusha chombo cha Artemis II kikiwa na wanaanga wanne.
Safari hiyo ni ya kwanza ya binadamu kuuzunguka mwezi ndani ya zaidi ya nusu karne tangu enzi za programu ya Apollo.
Roketi kubwa ilirushwa kutoka kituo cha Safari za anga cha Kennedy, huku maelfu ya watu wakishuhudia tukio hilo muhimu.
Kikosi hicho kinajumuisha Wamarekani watatu na Mkanada mmoja, na ni safari ya kwanza yenye mchanganyiko mkubwa zaidi wa watu—ikiwemo mwanamke na mtu wa rangi.
Wanaanga hao watachukua siku kumi, wakipita karibu na mwezi na kusafiri umbali mkubwa zaidi kuwahi kufikiwa na binadamu kabla ya kurejea duniani.
NASA inasema mafanikio ya safari hii ni hatua muhimu kuelekea lengo la kurejesha binadamu mwezini katika miaka michache ijayo na hatimaye kuanzisha makazi ya kudumu.
Tetemeko la 7.4 Indonesia latishia tsunami, mawimbi hatari

Indonesia imekuwa ikikumbwa na matetemeko ya ardhi ambayo wakati mwingine pia husababisha tsunamiPicha: Iryanda Mardanuz/DW
Tetemeko hilo lilisababisha tahadhari ya tsunami kutolewa kwa maeneo ya Indonesia pamoja na nchi jirani za Ufilipino na Malaysia.
Tetemeko kubwa la ardhi lenye ukubwa wa 7.4 limetokea katika Bahari ya Molucca kaskazini mwa Indonesia, karibu na kisiwa cha Ternate, kulingana na Shirika la Utafiti wa Jiolojia la Marekani.
Tetemeko hilo lilisababisha tahadhari ya tsunami kutolewa kwa maeneo ya Indonesia pamoja na nchi jirani za Ufilipino na Malaysia.
Hakuna taarifa za mara moja kuhusu majeruhi, lakini mitetemeko midogo ya baadae yenye ukubwa hadi 5 imeripotiwa.
Mamlaka za Indonesia zimeitaka baadhi ya miji, ikiwemo Ternate na Tidore, kujiandaa kwa uwezekano wa uokoaji wa dharura, huku baadhi ya majengo yakiripotiwa kuharibika.
Tetemeko hilo lilitokea katika kina cha takribani kilomita 35 na kitovu chake kikiwa karibu kilomita 120 kutoka Ternate.
Maafisa wa tahadhari ya tsunami wamesema mawimbi hatari yanaweza kutokea ndani ya umbali wa kilomita 1,000 kutoka eneo la tukio.
Moto na milipuko kambi ya kijeshi Burundi vyaua watu 13

Jeshi limesema milipuko hiyo ilisababishwa na hitilafu ya umeme na kwamba hali imedhibitiwa kikamilifuPicha: Ju Yinhe/Xinhua/IMAGO
Watu 13 wamefariki na wengine 57 kujeruhiwa kufuatia mlipuko mkubwa uliosababishwa na moto katika kambi ya kijeshi nchini Burundi.
Jeshi limesema moto huo ulizuka usiku katika ghala la kuhifadhia vifaa vya kijeshi na kusababisha milipuko kadhaa baada ya risasi na mabomu kulipuka.
Msemaji wa jeshi, Gaspard Baratuza, amesema chanzo cha moto huo ni hitilafu ya umeme, akisisitiza kuwa hakukuwa na shambulio lolote dhidi ya kambi hiyo.
Tukio hilo lilitokea katika eneo la Musaga, nje kidogo ya jiji la Bujumbura, ambapo wakazi walikimbia kwa hofu huku milipuko ikisikika kwa umbali mkubwa.
Maafisa wamewataka wananchi kutoa taarifa kuhusu mabaki ya milipuko ambayo hayajalipuka, wakati hali ikianza kurejea kawaida.
Italy yaopoa miili 19 ya wahamiaji waliokufa baharini

Wahamiaji wengi hutumia boti zisizo na viwango kufanza safari hatari za kwenda Ulaya kupitia bahari ya Mediterania, ambayo ni hatari sana.Picha: Marcel Beloqui Evardone/SIPA/picture alliance
Waliookolewa, wakiwemo watoto watano, walipelekwa katika kisiwa cha Lampedusa nchini Italia, huku watu watatu wakiripotiwa kupotea.
Watu 19 wamefariki dunia na wengine 58 kuokolewa baada ya boti ya wahamiaji kuharibika katika Bahari ya Mediterania ikitokea Libya kuelekea Ulaya.
Waliookolewa, wakiwemo watoto watano, walipelekwa katika kisiwa cha Lampedusa nchini Italia, huku watu watatu wakiripotiwa kupotea.
Kwa mujibu wa Shirika la Kimataifa la Uhamiaji, IOM, wengi wa waliofariki walikufa kwa baridi kali baada ya kukaa baharini kwa siku kadhaa.
Shirika la uokoaji la Sea-Watch limesema vifo hivyo ni sehemu ya ongezeko la ajali baharini, likikadiria zaidi ya watu 100 wamefariki ndani ya siku tatu zilizopita.
Takwimu zinaonyesha kuwa hadi sasa mwaka huu, zaidi ya watu 640 wamepoteza maisha katika njia ya kati ya Mediterania, ikiwa ni miongoni mwa viwango vya juu zaidi katika miaka ya hivi karibuni.
Marekani yamuondolea vikwazo kaimu Rais wa Venezuela

Rais Delcy Rodriguez amesema hatua ya Marekani kuomdolea vikwazo ni muhimu kwa uhusiano.Picha: Juan Barreto/AFP
Marekani imeondoa vikwazo dhidi ya kaimu rais wa Venezuela, Delcy Rodríguez, hatua inayotafsiriwa kama mabadiliko makubwa ya sera ya Washington kuelekea Caracas.
Hatua hiyo, iliyotangazwa na Wizara ya Fedha ya Marekani, inaashiria kutambuliwa rasmi kwa uongozi wa Rodríguez baada ya kuondolewa madarakani kwa kiomngozi wa nchi hiyo, Nicolás Maduro.
Hakuna sababu rasmi iliyotolewa kuhusu uamuzi huo, lakini unaonekana kuwa sehemu ya juhudi za kurejesha uhusiano wa kidiplomasia kati ya mataifa hayo mawili.
Rodríguez,ambaye aliwekewa vikwazo mwaka 2018, amepongeza hatua hiyo akisema ni mwanzo wa kuimarika kwa mahusiano na kufungua milango ya uwekezaji na maendeleo ya kiuchumi nchini humo.
Marekani pia inatarajia kushirikiana na serikali mpya ya Venezuela kuongeza uzalishaji wa mafuta na rasilimali nyingine, huku nchi hiyo ikiwa na akiba kubwa zaidi ya mafuta duniani.
Tiger Woods akataa kuwa nahodha wa Marekani Ryder Cup 2027

Tiger Woods alishinda mataji makubwa 15 ya mchezo wa gofu kabla ya kuanza kukumbwa na misukosuko ya kimaisha.Picha: Mike Blake/REUTERS
Tiger Woods amekataa kuiongoza timu ya Marekani Ryder Cup 2027 ili kuzingatia afya yake, baada ya ajali ya gari na tuhuma za kuendesha akiwa amelewa.
Nyota wa gofu Tiger Woods amekataa kuwa nahodha wa timu ya Marekani katika mashindano ya Ryder Cup ya mwaka 2027.
Chama cha PGA cha Amerika kimesema Woods amechukua uamuzi huo ili kuzingatia afya yake na ustawi wa muda mrefu.
Hatua hiyo inakuja baada ya Woods kushtakiwa kwa kuendesha gari akiwa amelewa kufuatia ajali ya barabarani wiki iliyopita, ingawa hakupata majeraha.

Gari la Woods lilipinduka ingawa hakujeruhiwa, na ikagundulika kuwa alikuwa amelewa.Picha: Martin County Sheriff’s Office/dpa/picture alliance
Polisi waliripoti dalili za ulevi na walipata dawa aina ya hydrocodone ndani ya gari lake, ambayo hutumika kutibu maumivu makali.
Woods, mshindi wa mataji makubwa 15, alikuwa akitarajiwa kuiongoza timu ya Marekani katika mashindano hayo yatakayofanyika Ireland, lakini sasa hatakuwepo kutokana na changamoto zake za kiafya.
afghanistan, africa, albania, algeria, America, american-samoa, andorra, angola, anguilla, antarctica, antigua-and-barbuda, argentina, armenia, aruba, arusha, australia, austria, azerbaijan, bahamas, bahrain, bangladesh, barbados, belarus, Belgium, belize, benin, bermuda, bhutan, bolivia, bosnia-and-herzegovina, botswana, Boukinafaso, brazil, brunei-darussalam, bulgaria, burkina-faso, burma, burundi, california, cambodia, cameroon, canada, cape-verde, cayman-islands, central-african-republic, Chad, chicago, chile, china, christmas-island, cocos-keeling-islands, colombia, comoros, congo, cook-islands, costa-rica, cote-divoire-ivory-coast, Croatia, cuba, cyprus, czech-republic, darsalaam, democratic-peoples-rep-north-korea, democratic-republic-of-the-congo-kinshasa, denmark, djibouti, dodoma, dominica, dominican-republic, dr-congo, dubai, east-timor-timor-leste, ecuador, egypt, egypty, el-salvador, england, equatorial-guinea, equitorial-guinea, eritrea, estonia, eswatini, ethiopia, falkland-islands, faroe-islands, federal-states-of-moldova, fiji, finland, Florida, france, french-guiana, french-polynesia, french-southern-territories, gabon, gaza, georgia, germany, ghana, gibraltar, goma, Greece, greenland, grenada, guadeloupe, guam, guatemala, guinea, guinea-bissau, guyana, habari, haiti, holy-see, honduras, hong-kong, houston, hungary, iceland, india, indonesia, Iowa, iran, iran-islamic-republic-of, iraq, ireland, israel, italia, italy, ivory-coast, jamaica, japan, jordan, karatu, kazakhstan, kilimanjaro, kinshasa, kiribati, kiswahili, korea, kosovo, kuwait, kyrgyzstan, lao, latvia-lebanon-lesotho-liberia-libya-liechtenstein-lithuania-luxembourg, Lebanon, liberia, macau, madagascar, malawi, malaysia-maldives, Mali, malta, marshall-islands-martinique-mauritania-mauritius, massechutes, mayotte, mazingira, mbeya, meru, mexico, miami, micronesia, monaco-mongolia-montenegro, montserrat, morocco, mozambique-myanmar, mtwara, mwanza, namibia, nauru, nepal, netherlands, netherlands-antilles, nevada, new-caledonia, new-zealand, newyork, nicaragua, niger, nigeria, niue, north-macedonia, northern-mariana-islands, norway, oman, pakistan, palau, palestine, palestinian-territories, panama, papua-new-guinea, paraguay, peoples-democratic-republic, peru, philadhephia, philipians, Philippines, pitcairn-island, poland, politics, Portugal, puerto-rico, qatar, republic-of, republic-of-brazzaville, republic-of-south-korea, reunion-island, romania, Russia, russian-federation, rwanda, sahara-occidental, saint-kitts-and-nevis, saint-lucia, saint-vincent-and-the-grenadines, samoa, san-marino, sao-tome-and-principe, saudi-arabia, saudiarabia, scotland, Senegal, serbia, seychelles, sierra-leone, Singapore, singida, slovakia-slovak-republic, slovenia, solomon-islands, somalia, southafrica, spain, sri-lanka, sudan, suriname, swaziland-eswatini, sweden, switzerland, syria, syrian-arab-republic, tabora, taiwan-republic-of-china, tajikistan, tanzania, texas, thailand, the-gambia, tibet, timor-leste-east-timor, togo, tokelau, tonga, toronto, trinidad-and-tobago, tunisia, turkey, turkmenistan, turks-and-caicos-islands, tuvalu, uganda, united-arabs-emirates, united-kingdom, united-states, uruguay, uzbekistan, vancover, vanuatu, vatican-city-state-holy-see, venezuela, vietnam, virgin-islands-british, virgin-islands-u-s, wallis-and-futuna-islands, wallis-and-futuna-islands, wallis-et-futuna, washington-dc, western-sahara, yemen, zambia, zambie, zimbabwe
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.