Shirika la ndege la Korea mbioni kudhibiti athari ya kupanda kwa bei ya mafuta

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Na Cantona Joseph Imechapishwa : March 31, 2026 13:00 (EAT)

Vocalize Pre-Player Loader
.

Shirika la ndege la Korea Kusini, Korea linasema kuwa linachukua hatua za dharura kukabiliana na athari za kupanda kwa bei ya mafuta ya ndege na kuzorota kwa uchumi kutokan na vita vya Iran.

Makamu mwenyekiti wa shirika hilo la ndege Woo Ki-hong aliwaambia wafanyakazi katika nyaraka zililozoonekana na BBC kwamba bei ya nishati imeongezeka zaidi ya mara mbili ya ile iliyowekwa kwenye mpango wa biashara wa shirika hilo, na kusababisha “kuongezeka kwa gharama ya mafuta ya kila mwezi”.

Shirika litachukua “hatua za kupunguza gharama” kuanzia mwezi Aprili ili kuimarisha utendakazi wa shirika hilo, msemaji wa Korea Air alisema Jumanne.

Bei ya mafuta ya ndege ilipanda hadi takribani dola 200 (£151.45) kwa pipa tarehe 20 Machi, zaidi ya mara mbili ya ilivyokuwa mwezi Februari, kulingana na takwimu za hivi punde za Chama cha Kimataifa cha Usafiri wa Anga.

Mafuta ghafi yanauzwa kwa zaidi ya 50% ya juu kuliko kabla ya vita kuanza, na kufanya bei ya mafuta ya ndege kuongezeka.

.
Maelezo ya picha,Celine Dion

Céline Dion ametangaza kurejea jukwaani, ikiwa ni miaka minne baada ya kugundulika kuwa na ugonjwa usiotibika ambao uliathiri sauti yake na uwezo wake wa kutembea.

Nyota huyo, anayejulikana kwa nyimbo kama vile My Heart Will Go On na Because You Loved Me, ataimba kwa siku 10 katika ukumbi wa Paris La Défense Arena mbele ya mashabiki 40,000 mnamo Septemba na Oktoba.

Tangazo hilo lilikuja siku ya 58 kusherehekea kuzaliwa kwake. Katika ujumbe kwenye ukurasa wake wa Instagram, Dion alitaja kurudi kwake kama “zawadi bora zaidi ya maisha yangu”. “Niko tayari kufanya hivi,” aliwaambia mashabiki. “Ninajisikia vizuri, nina nguvu, ninahisi msisimko, ni wazi, [na] bila shaka, wasiwasi kidogo.”

Akizungumzia hali yake ya kiafya, Dion alisema: “Ninaendelea vizuri, ninasimamia afya yangu, ninahisi vizuri. Ninaimba tena, hata kucheza dansi kidogo. “Lakini sina budi kukuambia jambo muhimu sana: Katika miaka hii michache iliyopita, kila siku ambayo imepita, nilihisi maombi na msaada wako, fadhila na upendo wako. Aliendelea: “Ninawashukuru ninyi nyote. Siwezi kusubiri kuwaona tena.”

Mpango wa Iran kutoza ushuru meli kupita Mlango – Bahari wa Hormuz waidhinishwa

.

Kamati ya bunge nchini Iran imeidhinisha mipango ya kutoza ushuru meli zinazopita Mlango-Bahari wa Hormuz, kwa mujibu wa shirika la habari la Fars linaloshirikiana na Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC).

Imeripoti kuwa mjumbe wa tume ya usalama wa taifa amethibitisha kuidhinishwa kwa mpango huo, ambao pia utazifanya meli za Marekani na Israel zikizuiliwa kupita katika mkondo huo wa bahari.

Inaongeza kuwa, chini ya mpango huo, nchi nyingine ambazo zimeshiriki katika vikwazo dhidi ya Iran pia zitazuiliwa.

Shirika la habari la AFP liliripoti kuwa mfumo huo mpya wa ushuru ulitangazwa kwenye televisheni ya taifa ya Iran, ambayo ilisema Iran itautekeleza kwa ushirikiano na Oman.

Takribani asilimia 20 ya mafuta ghafi duniani husafirishwa kupitia njia muhimu ya meli ambayo iko kati ya Iran na Oman.

Hata hivyo, tangu vita kuanza, njia za kuvuka mipaka zimeshuka kwa karibu asilimia 95, kulingana na kampuni ya ujasusi ya baharini ya Kpler.

afghanistanafricaalbaniaalgeriaAmericaamerican-samoaandorraangolaanguillaantarcticaantigua-and-barbudaargentinaarmeniaarubaarushaaustraliaaustriaazerbaijanbahamasbahrainbangladeshbarbadosbelarusBelgiumbelizebeninbermudabhutanboliviabosnia-and-herzegovinabotswanaBoukinafasobrazilbrunei-darussalambulgariaburkina-fasoburmaburundicaliforniacambodiacamerooncanadacape-verdecayman-islandscentral-african-republicChadchicagochilechinachristmas-islandcocos-keeling-islandscolombiacomoroscongocook-islandscosta-ricacote-divoire-ivory-coastCroatiacubacyprusczech-republicdarsalaamdemocratic-peoples-rep-north-koreademocratic-republic-of-the-congo-kinshasadenmarkdjiboutidodomadominicadominican-republicdr-congodubaieast-timor-timor-lesteecuadoregyptegyptyel-salvadorenglandequatorial-guineaequitorial-guineaeritreaestoniaeswatiniethiopiafalkland-islandsfaroe-islandsfederal-states-of-moldovafijifinlandFloridafrancefrench-guianafrench-polynesiafrench-southern-territoriesgabongazageorgiagermanyghanagibraltargomaGreecegreenlandgrenadaguadeloupeguamguatemalaguineaguinea-bissauguyanahabarihaitiholy-seehondurashong-konghoustonhungaryicelandindiaindonesiaIowairaniran-islamic-republic-ofiraqirelandisraelitaliaitalyivory-coastjamaicajapanjordankaratukazakhstankilimanjarokinshasakiribatikiswahilikoreakosovokuwaitkyrgyzstanlaolatvia-lebanon-lesotho-liberia-libya-liechtenstein-lithuania-luxembourgLebanonliberiamacaumadagascarmalawimalaysia-maldivesMalimaltamarshall-islands-martinique-mauritania-mauritiusmassechutesmayottemazingirambeyamerumexicomiamimicronesiamonaco-mongolia-montenegromontserratmoroccomozambique-myanmarmtwaramwanzanamibianaurunepalnetherlandsnetherlands-antillesnevadanew-caledonianew-zealandnewyorknicaraguanigernigerianiuenorth-macedonianorthern-mariana-islandsnorwayomanpakistanpalaupalestinepalestinian-territoriespanamapapua-new-guineaparaguaypeoples-democratic-republicperuphiladhephiaphilipiansPhilippinespitcairn-islandpolandpoliticsPortugalpuerto-ricoqatarrepublic-ofrepublic-of-brazzavillerepublic-of-south-koreareunion-islandromaniaRussiarussian-federationrwandasahara-occidentalsaint-kitts-and-nevissaint-luciasaint-vincent-and-the-grenadinessamoasan-marinosao-tome-and-principesaudi-arabiasaudiarabiascotlandSenegalserbiaseychellessierra-leoneSingaporesingidaslovakia-slovak-republicsloveniasolomon-islandssomaliasouthafricaspainsri-lankasudansurinameswaziland-eswatiniswedenswitzerlandsyriasyrian-arab-republictaborataiwan-republic-of-chinatajikistantanzaniatexasthailandthe-gambiatibettimor-leste-east-timortogotokelautongatorontotrinidad-and-tobagotunisiaturkeyturkmenistanturks-and-caicos-islandstuvaluugandaunited-arabs-emiratesunited-kingdomunited-statesuruguayuzbekistanvancovervanuatuvatican-city-state-holy-seevenezuelavietnamvirgin-islands-britishvirgin-islands-u-swallis-and-futuna-islandswallis-and-futuna-islandswallis-et-futunawashington-dcwestern-saharayemenzambiazambiezimbabwe

CantonaDigital
CantonaDigital

Listen Live Radio Fortune Africa
Ukweli Na Burudani.

-Be ready to be Impacted, Inspired & Empowered.

-Keep watching our Channels

Cantona Cast Television,

Fortune Television Network (FTN)

Donation
Paypal https://www.paypal.com/donate/?hosted_button_id=6EKXMLNW8W6A2&fbclid=IwY2xjawQxeChleHRuA2FlbQIxMABicmlkETFRdkNBRndpclRDQTB5bXZZc3J0YwZhcHBfaWQQMjIyMDM5MTc4ODIwMDg5MgABHq960uGsyU3ABRIBc2h-iXGhHATvuEqe55gFsQ-rDb0fT-Z7SIQ3TV8LnkpD_aem_ybU2SvBlvyqrVsS9NAczRw

An attitude determines an altitude.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025

5,344 posts
0 followers

Fediverse Followers


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a Reply