Pakistan kuwa mwenyeji wa mazungumzo ya amani kati ya Saudi Arabia, Uturuki na Misri

Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Na Cantona Joseph Imechapishwa : March 28, 2026 16:44 (EAT)

Vocalize Pre-Player Loader

s

Waziri wa mambo ya nje wa Pakistan Ishaq Dar anasema nchi hiyo itawapokea mawaziri wa mambo ya nje wa Saudi Arabia, Uturuki na Misri mjini Islamabad kuanzia tarehe 29-30 Machi.

Watafanya “majadiliano ya kina”, ikiwa ni pamoja na juhudi za “kupunguza mvutano katika eneo hilo”, anaandika katika taarifa iliyochapishwa kwenye mtandao wa kijamii X.

Wizara ya mambo ya nje ya Misri sasa imetoa taarifa inayothibitisha kwamba waziri wake wa mambo ya nje amesafiri hadi mji mkuu wa Pakistan kwa mazungumzo hayo.

Pakistan imekuwa ikifanya juhudi za kuchukua jukumu la upatanishi katika eneo hilo.

Kando na hilo, imejitolea kuandaa mazungumzo kati ya Marekani na Iran – lakini bado hakuna uthibitisho wowote kama yatafanyika.

Mapema wiki hii, Dar alisema “mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja” yanafanyika kupitia “ujumbe unaowasilishwa na Pakistan”.

Trump pia alichapisha picha ya chapisho la X kutoka kwa Waziri Mkuu wa Pakistan Shehbaz Sharif mapema wiki hii, akichapisha kwenye Truth Social.

Katika chapisho hilo, Sharif alisema Pakistan “iko tayari” kuandaa mazungumzo.

Houthi yashambulia Israel kwa mara ya kwanza tangu vita ya Iran ianze

s

Waasi wa Houthi wanaoungwa mkono na Iran nchini Yemen wamesema wameishambulia Israel kwa mara ya kwanza tangu kuanza kwa vita kati ya Iran, Marekani na Israel, wakidai kurusha makombora ya balistiki kulenga maeneo nyeti ya kijeshi ya Israel.

Kundi hilo limesema lilirusha makombora kadhaa yakilenga “maeneo nyeti ya kijeshi ya Israel” ikiwa ni sehemu ya kujibu mashambulizi yanayodaiwa kufanywa dhidi ya Iran pamoja na Lebanon, Iraq na maeneo ya Palestina.

Houthi wameongeza kuwa mashambulizi yao yataendelea hadi kile walichokiita “uchokozi” dhidi ya pande zote utakapotamatika.

Taarifa hiyo imekuja baada ya jeshi la Israel kusema limefanikiwa kuzuia kombora lililorushwa kutoka Yemen kuelekea Israel.

Wakati huo huo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Marco Rubio, amesema Marekani inatarajia kumaliza operesheni za kijeshi ndani ya wiki chache zijazo, huku mvutano ukiendelea kuongezeka katika eneo hilo.

Huenda kombora la Marekani lilitumika katika shambulio lililosababisha vifo Iran – Wataalamu

xcv

Wataalamu wa silaha wanasema huenda makombora ya kisasa ya Marekani yalitumika katika shambulio baya lililolenga eneo la makazi nchini Iran mwezi uliopita, kwa mujibu wa uchambuzi wa video za tukio hilo.

Wataalamu hao walisema kuwa kifaa cha kurushwa kilichoonekana kwenye video ya shambulio dhidi ya majengo ya makazi katika mji wa kusini wa Lamerd kinafanana na kombora la Precision Strike Missile (PrSM).

Silaha hiyo ni kombora jipya la masafa marefu linalotumiwa na jeshi la Marekani.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya serikali ya Iran, watu wasiopungua 21 waliuawa katika mashambulizi mawili yaliyolenga mji huo siku hiyo, yakigonga majengo ya makazi pamoja na ukumbi wa michezo ulioko umbali wa takribani mita 300.

Kamandi ya kijeshi ya Marekani inayosimamia operesheni za Mashariki ya Kati (Centcom) haijatoa maoni kuhusu tukio hilo.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2026

afghanistanafricaalbaniaalgeriaAmericaamerican-samoaandorraangolaanguillaantarcticaantigua-and-barbudaargentinaarmeniaarubaarushaaustraliaaustriaazerbaijanbahamasbahrainbangladeshbarbadosbelarusBelgiumbelizebeninbermudabhutanboliviabosnia-and-herzegovinabotswanaBoukinafasobrazilbrunei-darussalambulgariaburkina-fasoburmaburundicaliforniacambodiacamerooncanadacape-verdecayman-islandscentral-african-republicChadchicagochilechinachristmas-islandcocos-keeling-islandscolombiacomoroscongocook-islandscosta-ricacote-divoire-ivory-coastCroatiacubacyprusczech-republicdarsalaamdemocratic-peoples-rep-north-koreademocratic-republic-of-the-congo-kinshasadenmarkdjiboutidodomadominicadominican-republicdr-congodubaieast-timor-timor-lesteecuadoregyptegyptyel-salvadorenglandequatorial-guineaequitorial-guineaeritreaestoniaeswatiniethiopiafalkland-islandsfaroe-islandsfederal-states-of-moldovafijifinlandFloridafrancefrench-guianafrench-polynesiafrench-southern-territoriesgabongazageorgiagermanyghanagibraltargomaGreecegreenlandgrenadaguadeloupeguamguatemalaguineaguinea-bissauguyanahabarihaitiholy-seehondurashong-konghoustonhungaryicelandindiaindonesiaIowairaniran-islamic-republic-ofiraqirelandisraelitaliaitalyivory-coastjamaicajapanjordankaratukazakhstankilimanjarokinshasakiribatikiswahilikoreakosovokuwaitkyrgyzstanlaolatvia-lebanon-lesotho-liberia-libya-liechtenstein-lithuania-luxembourgLebanonliberiamacaumadagascarmalawimalaysia-maldivesMalimaltamarshall-islands-martinique-mauritania-mauritiusmassechutesmayottemazingirambeyamerumexicomiamimicronesiamonaco-mongolia-montenegromontserratmoroccomozambique-myanmarmtwaramwanzanamibianaurunepalnetherlandsnetherlands-antillesnevadanew-caledonianew-zealandnewyorknicaraguanigernigerianiuenorth-macedonianorthern-mariana-islandsnorwayomanpakistanpalaupalestinepalestinian-territoriespanamapapua-new-guineaparaguaypeoples-democratic-republicperuphiladhephiaphilipiansPhilippinespitcairn-islandpolandpoliticsPortugalpuerto-ricoqatarrepublic-ofrepublic-of-brazzavillerepublic-of-south-koreareunion-islandromaniaRussiarussian-federationrwandasahara-occidentalsaint-kitts-and-nevissaint-luciasaint-vincent-and-the-grenadinessamoasan-marinosao-tome-and-principesaudi-arabiasaudiarabiascotlandSenegalserbiaseychellessierra-leoneSingaporesingidaslovakia-slovak-republicsloveniasolomon-islandssomaliasouthafricaspainsri-lankasudansurinameswaziland-eswatiniswedenswitzerlandsyriasyrian-arab-republictaborataiwan-republic-of-chinatajikistantanzaniatexasthailandthe-gambiatibettimor-leste-east-timortogotokelautongatorontotrinidad-and-tobagotunisiaturkeyturkmenistanturks-and-caicos-islandstuvaluugandaunited-arabs-emiratesunited-kingdomunited-statesuruguayuzbekistanvancovervanuatuvatican-city-state-holy-seevenezuelavietnamvirgin-islands-britishvirgin-islands-u-swallis-and-futuna-islandswallis-and-futuna-islandswallis-et-futunawashington-dcwestern-saharayemenzambiazambiezimbabwe

CantonaDigital
CantonaDigital

Listen Live Radio Fortune Africa
Ukweli Na Burudani.

-Be ready to be Impacted, Inspired & Empowered.

-Keep watching our Channels

Cantona Cast Television,

Fortune Television Network (FTN)

Donation
Paypal https://www.paypal.com/donate/?hosted_button_id=6EKXMLNW8W6A2&fbclid=IwY2xjawQxeChleHRuA2FlbQIxMABicmlkETFRdkNBRndpclRDQTB5bXZZc3J0YwZhcHBfaWQQMjIyMDM5MTc4ODIwMDg5MgABHq960uGsyU3ABRIBc2h-iXGhHATvuEqe55gFsQ-rDb0fT-Z7SIQ3TV8LnkpD_aem_ybU2SvBlvyqrVsS9NAczRw

An attitude determines an altitude.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025

5,310 posts
0 followers

Fediverse Followers


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a Reply