Afrika: Hitaji la Dola Efu 15 kuingia Marekani kwa ajili ya kombe la dunia

Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Na Cantona Joseph Imechapishwa : March 26, 2026 06:07 (EAT)

Vocalize Pre-Player Loader

Sera mpya iliyopanuliwa na utawala wa Rais wa Marekani Donald Trump, huenda ikawafanya wasafiri kutoka nchi tano za Afrika zilizofuzu Kombe la Dunia la mwaka huu kuweka dhamana ya hadi dola elfu 15 ili kuingia Marekani kwa ajili ya mashindano hayo.

Donald Trump - Rais wa Marekani.
Donald Trump – Rais wa Marekani. © Kevin Lamarque / Reuters

Kwa mujibu wa sera hii, mashabiki toka kwenye nchi hizo watalazimika kulipa kwanza kiasi hicho cha fedha kama dhamana na viza ya kuruhusiwa kuingia Marekani na kisha kurejeshewa baada ya kuwa umeondoka kwenye taifa hilo.

Mpango huu wa majaribio ulitangazwa mwaka 2025 na ulizilenga nchi za bara la Afrika, mashariki ya Kati, Latini Amerika na baadhi kutoka ukanda wa Asia, wiki iliyopita wizara ya mambo ya nje ikitaja orodha mpya yan chi 50 ambazo raia wake watatakiwa kuweka dhamana hiyo.

TANGAZO

https://www.paypal.com/donate/?hosted_button_id=6EKXMLNW8W6A2&fbclid=IwY2xjawQu3lFleHRuA2FlbQIxMABicmlkETFDaHJMNDVrZUx6VXRNY3NUc3J0YwZhcHBfaWQQMjIyMDM5MTc4ODIwMDg5MgABHj3J-oZN3HqbjD7V9XaumO03MtdAKWqx7SIqWHSUUr8BWukkOEEpeLne6xWt_aem_1WY6FZPnX5UmceUPLC_RAg

Chini ya utaratibu huu raia wa AlgeriaCape Verde, Ivory Coast, Senegal na Tunisia ambazo zote zimefuzu kucheza fainali za kombe la dunia la mwaka huu, mashabiki wao watalazimika kwanza kulipa fedha hiyo kabla ya kupewa viza.

Kuelekea fainali hizi zitakazochezwa kwenye nchi ya Marekani, Mexico na Canada, kumekuwa na wasiwasi kuhusu ubaguzi wa mashabiki toka katika baadhi ya nchi, wadai wakilitaka shirikisho la soka duniani, FIFA kuiomba Marekani kulegeza makataa hayo.

Michuano hii inatarajiwa kuanza kutumia vumbi kuanzia Juni 11 hadi Julai 19, ambapo fainali itachezwa Marekani kwenye uwanja wa MetLife huko New Jersey.

Mapendekezo yaliowasilishwa na Marekani yanapitiwa na mamlaka: Iran

Katika mahojiano na televisheni ya kitaifa, Waziri wa mambo ya kigeni wa Iran Abbas Araqchi, aliweka wazi kuwa mapendekezo ya Marekani ya kumaliza vita yanapitiwa na mamlaka ya juu jijini Tehran.

Abás Araqchi, Waziri wa mambo ya kigeni wa Iran.
Abás Araqchi, Waziri wa mambo ya kigeni wa Iran. AP – Khalil Hamra

Licha ya kuthibitisha kwamba nchi yake inapitia mapendekezo ya Marekani, alisistiza kuwa ujumbe wanaoupokea kupitia kwa wapatanishi hauwezi kuchukuliwa kama mazungumzo.

Matamshi yake Araqchi yalionyesha nia ya Tehran kufanya mazungumzo ya kumaliza mapigano iwapo marsharti yake yatazingatiwa.

Alisisitizia msimamo wa Tehran kwamba ujumbe wanaopata kutoka kwa Marekani kupitia kwa wapatanishi sio mazungumzo kama inavyodaiwa na Marekani.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Israeli Channel 12, mpango wa Rais Trump uliowasilishwa hwa Iran kupitia kwa Pakistani unajumuisha, Shuguli katika vinu vya nyukilia vya Natanz, Fordow na Isfahan zitasitishwa na vinu hivyo kuharibiwa.

Shirika la nishati ya Atomiki (IAEA) litapewa nafasi ya kufuatilia kwa uwazi shughuli zinazohusiana na nyukilia nchini Iran miongoni mwa mengine.

Marekani inashauriana peke yake kuhusu vita: Tehran

Iran imepokea mpango wa mapendekezo 15 kutoka kwa Marekani kuhusu namna ya kumaliza vita vinavyoendelea Mashariki ya Kati, huku Tehran ikisema Marekani inashauriana peke yake kuhusu kumaliza vita.

Spika wa bunge la Iran Mohammad Bagher Ghalibaf, ni miongoni mwa watu wenye ushawishi mkubwa zaidi katika siasa za Iran
Spika wa bunge la Iran Mohammad Bagher Ghalibaf, ni miongoni mwa watu wenye ushawishi mkubwa zaidi katika siasa za Iran © ICANA NEWS AGENCY / AFP

Ripoti zinasema kuwa, Iran imepokea mapendekezo hayo kutoka kwa Pakistan ambayo, imesema iko tayari kusaidia kufanikisha mazungumzo hayo.

Hata hivyo, mpango huo haujawekwa wazi, lakini ripoti za ndani zinaeleza kuwa baadhi ya mambo yanayopendekezwa ni kuwa, Iran iachane kabisa na mradi wa Nyuklia, ili vikwazo vyote vya kiuchumi ilivyowekewa viondolewe.

Waziri mmoja wa Israeli amesema  mapendekezo hayo yanaonekana maridadi kwenye makaratasi, lakini hana uhakika iwapo Iran itaikubali.

Katika hatua nyingine, jeshi la Iran limepuuzilia mbali mapendekezo ya Marekani na kuahidi kuendelea kupigana.

Licha ya jitihada hizi za kuwepo kwa mazungumzo, wanajeshi wa Marekani na Israli wameendelea kuishambulia Iran, ambayo pia imeendelea kurusha makombora yake nchini Israeli.

afghanistanafricaalbaniaalgeriaAmericaamerican-samoaandorraangolaanguillaantarcticaantigua-and-barbudaargentinaarmeniaarubaarushaaustraliaaustriaazerbaijanbahamasbahrainbangladeshbarbadosbelarusBelgiumbelizebeninbermudabhutanboliviabosnia-and-herzegovinabotswanaBoukinafasobrazilbrunei-darussalambulgariaburkina-fasoburmaburundicaliforniacambodiacamerooncanadacape-verdecayman-islandscentral-african-republicChadchicagochilechinachristmas-islandcocos-keeling-islandscolombiacomoroscongocook-islandscosta-ricacote-divoire-ivory-coastCroatiacubacyprusczech-republicdarsalaamdemocratic-peoples-rep-north-koreademocratic-republic-of-the-congo-kinshasadenmarkdjiboutidodomadominicadominican-republicdr-congodubaieast-timor-timor-lesteecuadoregyptegyptyel-salvadorenglandequatorial-guineaequitorial-guineaeritreaestoniaeswatiniethiopiafalkland-islandsfaroe-islandsfederal-states-of-moldovafijifinlandFloridafrancefrench-guianafrench-polynesiafrench-southern-territoriesgabongazageorgiagermanyghanagibraltargomaGreecegreenlandgrenadaguadeloupeguamguatemalaguineaguinea-bissauguyanahabarihaitiholy-seehondurashong-konghoustonhungaryicelandindiaindonesiaIowairaniran-islamic-republic-ofiraqirelandisraelitaliaitalyivory-coastjamaicajapanjordankaratukazakhstankilimanjarokinshasakiribatikiswahilikoreakosovokuwaitkyrgyzstanlaolatvia-lebanon-lesotho-liberia-libya-liechtenstein-lithuania-luxembourgLebanonliberiamacaumadagascarmalawimalaysia-maldivesMalimaltamarshall-islands-martinique-mauritania-mauritiusmassechutesmayottemazingirambeyamerumexicomiamimicronesiamonaco-mongolia-montenegromontserratmoroccomozambique-myanmarmtwaramwanzanamibianaurunepalnetherlandsnetherlands-antillesnevadanew-caledonianew-zealandnewyorknicaraguanigernigerianiuenorth-macedonianorthern-mariana-islandsnorwayomanpakistanpalaupalestinepalestinian-territoriespanamapapua-new-guineaparaguaypeoples-democratic-republicperuphiladhephiaphilipiansPhilippinespitcairn-islandpolandpoliticsPortugalpuerto-ricoqatar Norrbottens lanrepublic-of-brazzavillerepublic-of-south-koreareunion-islandromaniaRussiarussian-federationrwandasahara-occidentalsaint-kitts-and-nevissaint-luciasaint-vincent-and-the-grenadinessamoasan-marinosao-tome-and-principesaudi-arabiasaudiarabiascotlandSenegalserbiaseychellessierra-leoneSingaporesingidaslovakia-slovak-republicsloveniasolomon-islandssomaliasouthafricaspainsri-lankasudansurinameswaziland-eswatiniswedenswitzerlandsyriasyrian-arab-republictaborataiwan-republic-of-chinatajikistantanzaniatexasthailandthe-gambiatibettimor-leste-east-timortogotokelautongatorontotrinidad-and-tobagotunisiaturkeyturkmenistanturks-and-caicos-islandstuvaluugandaunited-arabs-emiratesunited-kingdomunited-statesuruguayuzbekistanvancovervanuatuvatican-city-state-holy-seevenezuelavietnamvirgin-islands-britishvirgin-islands-u-swallis-and-futuna-islands

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2026

.

CantonaDigital
CantonaDigital

Listen Live Radio Fortune Africa
Ukweli Na Burudani.

-Be ready to be Impacted, Inspired & Empowered.

-Keep watching our Channels

Cantona Cast Television,

Fortune Television Network (FTN)

Donation
Paypal https://www.paypal.com/donate/?hosted_button_id=6EKXMLNW8W6A2&fbclid=IwY2xjawQxeChleHRuA2FlbQIxMABicmlkETFRdkNBRndpclRDQTB5bXZZc3J0YwZhcHBfaWQQMjIyMDM5MTc4ODIwMDg5MgABHq960uGsyU3ABRIBc2h-iXGhHATvuEqe55gFsQ-rDb0fT-Z7SIQ3TV8LnkpD_aem_ybU2SvBlvyqrVsS9NAczRw

An attitude determines an altitude.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025

5,285 posts
0 followers

Fediverse Followers


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a Reply